Tuesday, March 6, 2012
Wasaidizi wa home kwetu - Part 2
Mambo...
Last week niliambiwa story ikanifanya nipate goose bumps. Manake mimi kama mwanamke na mama, hii story inaweza hata kunitokea mimi muda wowote ule.
Ni huko Kimara in Dar Es Salaam. A mother of two children ni mfanya biashara, ili aweze kufuatilia biashara zake ikabidi atafute mdada wa kazi. Alifanikiwa to get one na wamekaa kwa muda pamoja. Sasa hiyo last week yule mama karudi nyumbani mchana, kakuta mwanaye mdogo anaumwa sana. Akamkimbiza hospital. Kufika wakampeleka Emergency. After uchunguzi kidogo Doctors found out yule mtoto kapewa sumu. The poor child akaaga dunia. Yule mama akachanganyikiwa. Mwanaye kala wapi hiyo sumu and kapewa na nani? Akamshuku house girl moja kwa moja because wanae hawala sehemu nyingine yoyote. Akarudi nyumbani kufika, mtoto mkubwa yupo all alone. Akamuuliza dada yuko wapi? Mtoto anagaragara chini anaumwa tumbo akilia. Mama akamchukua na huyo na kumkimbiza hospital ile ile ya kwanza. After uchunguzi akakutwa na yeye alilishwa sumu. Likafumuka. Wakaita polisi. Dada nyumbani hayupo kabeba all her stuff.. Ila kasahau picha zake. Kwa hiyo polisi wangali wanamtafuta.
So ikaja kugundulika kuwa yule dada alipika chakula cha usiku akakitia sumu. Yeye mwenyewe hakula siku hiyo akidai kuwa she had an early dinner. Kwa hiyo family nzima walilishwa sumu. Ila kwa vile yule mtoto aliyefariki ndio mdogo kuliko wote sumu ilimzidi nguvu and she passed away.
Seriously, iliniogopesha sana. Hivi huyo dada unayeishi naye unamjua kwa kiasi gani? Je hua unamkwaza mara kwa mara kwa kumgombeza na hata maybe kumpiga? Je, unajua kwao au ndugu zake? Unajua back ground yake? Jiulize kisha tafakari na uchukue hatua...
Kuwasiliana nami email: barbshassan@gmail.com
au Sms - +255 759 008500
much love..
xoxo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
dah, mbona hizi story za wadada ni noma, ukifikiria sana utashindwa hata kufanya kazi, lkn cha msingi ni kumjali tu kama ndugu yako, jamani tumeacha watoto home na huyo dada, na hamna mtu mwingine, kwa hiyo tukirudi home tukakuta salama, thanks be to God!
ReplyDeletelkn cha msingi ni kutrace na kujua background yake, ndugu etc ili ajue unajali,
pole sana kwa huyo mama.........
Mungu atusaidie na kwa kuwa ndie muweza atunusuru kwa yote.Pole kwa mama!! Ila katika kitu mie hua simkubalii dada ni kukataa kula chakula alichopika mwenyewe. maana haileti picha nzuri......NIMEOGOPA KUPITA KIASI.
ReplyDeleteElmmy
Pole sana mama wa kimara, cha msingi wakina mama hawa wadada wa nyumbani ni kuishi nao kama ndugu na si kuwabagua na kuwatusi kila kukicha.kikubwa pia ni kumuomba Mungu kwa ajili ya uwepo wake katika maisha yetu ya kila siku na atatuepusha na mengi!
ReplyDelete