Friday, May 25, 2012
Nifanyeje???
Shikamoo Dada Barbara,
Naitwa Lucy ni msichana wa miaka 23 na nipo chuo mwaka wa pili. Natokea katika family ya middle class na mama yangu ni single parent. Sijawahi kumfahamu wala kukutana na baba yangu. Nina boy friend ninayempenda sana na tumekuwepo kwenye mahusiano kwa miaka 2 sasa. Nilikutana naye chuoni. Na ndio nashiriki naye kimapenzi.
Mwezi jana mama yangu aliniita nikakaa kitako akidai ana mambo anata ku discuss nami. Ila alichoniambia kwa kweli kimeni frustrate sana na nipo njia panda sasa hivi. Mama alinambia kwa sauti ya upole na iliyojaa majonzi kuwa " Yeye ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na alibeba mimba yangu wakati ameshaathirika bila kujijua." Kwa hiyo ina maana mimi ni carrier wa HIV. Aliniomba nimsamehe kwani anahisi ameniharibia maisha yangu. Sikua na cha kumjibu na sijapata hadi sasa hivi. Nilienda kupima ili kuthibitisha na kweli nikakuta mimi ni muathirika. Sijui cha kufanya na mawazo yamenijaa tele. Na huyu kaka wa watu - my boy friend nimeshafanya naye mapenzi mara nyingi tu bila kutumia kinga. Naanzia wapi kumwambia hali yangu? Nahisi ataona mimi nilikua naifahamu hali yangu all through and chose not to tell him. Si ataona nilikusudia kumuua?
Katika chuo ninachosoma kuna a counselling center nimekua nikishinda humo kwani nimechanganyikiwa kabisa!
Naomba msaada wako wa kimawazo - na pia kutoka kwa wasomaji/ wadau wa blog hii..
Mubarikiwe
Lucy...
PS. Kwa leo sina comment. Nakuomba wewe mdau wa blog yangu tumsaidie Lucy...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
pole sana Lucy
ReplyDeleteMimi si daktari ila kwa elimu ya kawaida ya kufuatilia masuala haya ya HIV/AIDS, leo nitakuwa nimejifunza kitu kipya, kwani kwa miaka yote 23 unaweza kuishi bila msaada wa ARVs.
Tena HIV/AIDS inavyosumbua infant! kwanza nisaidiwe hili kabla ya kuchangia ushauri
Pole sana Lucy, ila naomba nikurekebishe kitu kimoja, umesema kwamba the gay (ur boyfriend) ataona umekusudia kumuua! jamani kuwa na ukimwi sio kufa mbona ww umeishi miaka yote hiyo? Unapoanguka ucgeuke kuangalia ulipojikwaa, nyanyuka, pangusa vumbi uendelee na safari. Kaza moyo umueleze bofriend wako, muanze maisha mapya ya kuhudhuria semina na clinic.Another thing, u have to forgive ur mum. I'm sure amekulea kwa uangalifu mkubwa coz alijua hali yako na umekua mzima hadi sasa,angeweza hata kujiua kwa hali aliyokua nayo lakini kakuzaa na leo umefkia hapo ulio.Ila pia kwa wengine msishiriki zinaa bila kinga au kupima kwanza na kuwa waaminifu.
ReplyDeleteThis is really sad and suprising, kuishi na HIV for all this years ni miujiza tayari. Lucy believe that this is not the end of your life, kweli inashtusha but i'm sure with counselling utaweza kukubali hii hali. As for the boyfriend ni vyema akapata the full story from you na umshauri akapime na yeye ajijue na kupanga life yake. As a christian tunaambiwa we have to forgive so pls msamehe mama yako, know that she's gone through alot knowing u r both sick all this years. God's ways are mysterious just like the way your life has turned out to be so have courage and trust in God, He will surely see u through this. Be blessed.
ReplyDeletepole sana Lucy ,kwanza msamehe mama yako na pili umweleze bf wako na muende kwa washauri ni ngumu kidogo na tatu muende kwenye maombi na amini wewe ni mkristo mkiombewa na kuamini mtakuwa okey, umeweza ku survive muda wote huo Mungu yupo na atawaponya dont give up u gonna be fine
ReplyDeletePole sana Lucy, na nakupongeza sana kuikubali hali hii mpaka umefikia hatua ya kutushirikisha hapa, ni wachache wana ujasiri huo!!! naamini utaweza kuichukulia hii hali bila wasiwasi.
ReplyDeleteKwanza mshukuru Mungu kwa kukujalia afya njema mpaka leo, hujapata tatizo, ni wachache na ukweli ni mara ya kwanza naisikia hii, Mungu ana mpango na wewe na hivyo mshukuru sana na uzidi kumuomba akupe maisha marefu na yenye afya
Pili mshukuru mama yako aliyeweza kuwa na ujasiri kukushirikisha chanzo cha tatizo lako kwani ni wengi hawana huo ujasiri wa kuwaeleza wenza/ndugu zao hali zao wazi hivyo, ungepata wakati mgumu kutafuta chanzo cha tatizo lako lkn mama amekua wazi, mshukuru sana wala usimlaumu, anakupenda!
Tatu huu si wakati muafaka wa kumjulisha boyfriend wako hali hii, inahitaji uchukue muda, katika vituo vya ushauri watakueleza ni wakati gani wa kuwaeleza ndg jamaa na rafiki, hutakiwi kukurupuka kwani wote mtakua kwenye presha na mwisho wake hata kinga yenu ya mwili inaweza kushuka ghafla. unatakiwa utulie kwanza uikubali hali yako ndio uwe tayari kumshirikishaa mwenzie na kwa kuanza uanze kumshawishi mkapime wote na utaona muitikio wake, kama atakua tayari bila ubishi ndio unaweza kumuambia kwa nini ulitaka mkapime kwani we ushajua hali yako. atakulaumu na kutokuelewa kwanza lkn kwa ushauri atakuelewa na atakushukuru. msiogope saivi kuna dawa na mnaweza wote kuwa na maambukizi mkazaa watoto wazima kabisa na maisha yakaendelea. Mungu ni mwema!
POLE SANA MDG WANGU SI WEWE TU MWENYE MATATIZO HAYO TUPO WENGI SANA TUMEZAA NA WATOTO WAPO SALAMA USIKATE TAMAA MAPEMA KINGA YA MWILI ITASHUKA MATOKEO YK UTAANZAA KUUGUA UGUA KILA MTU AKUJUE HAKUNA MTU ATAKAYE ISHI MILELE KILA MTU ATAKUFA NA KIFO CHAKE . UWE NA AMANI NI MAMBO YA KAWAIDA KTK ULIMWENGU WA SASA ONGEZA BIDII KWNY MASOMO MUNGU YUPO NA WEWE .
ReplyDeleteJipe moyo binti tena jipe moyo mkuu Mungu yupo nawe. Ni watu wengi sana wana tatizo hilo ninao ndugu katika familia yangu wanaishi maisha ya furaha tu, kwa vile wamelipokea tatizo na kuendelea na maisha. Usihuzunike sana ukaruhusu mwili wako kunyong'onyea na kinga ya mwili kushuka na ukaanza kushambuliwa na magonjwa. Unayo maisha marefu sana mbele ya kuendelea na dreams zako,. maana hata mama yako naye imemchukua muda kukueleza ukweli maana si kitu rahisi ni kigumu sana especially unapomweleza mtoto wako. Be strong hilo litapita na utandelea na masomo yako vizuri. Halafu la muhimu zaidi ni kumshirikisha huyo boyfriend wako kwa busara mweleze kisa kizima inawezekana hajaambukizwa japo mlikutana bila kinga.
ReplyDeleteMpokee YESU awe Bwana na Mwokozi wako nawe utakuwa umeokoka. Bila YESU hakuna maisha. Duniani kuna falme mbili: Falme ya Mungu ambayo kuingia ni kwa kupitia kwa YESU tu; na falme ya pili ni ya shetani.
ReplyDeleteLucy na wengine wote. Jiokoeni Kiroho na kimwili kwa kumkiri kuwa YESU ni Mwana wa Mungu na pia kumkana shetani na kazi zake zoote.
Mbarikiwe!
pole sana Lucy mwambie ukweli ili uwe huru.Mtegemee Mungu atakuwezesha!
ReplyDeleteMuachie Mungu
ReplyDeleteDear Lucy,
ReplyDeleteMaisha yote tunayopitia ni mapenzi ya mungu, hakuna binadamu katika dunia hii ambae hakutani na vikwazo na machungu ambayo wakati mwingine haujui uyabebeje lakini with god help maisha yanasonga mbele, Simama nyanyuka na anza kutembea. Siku hizi kuwa na HIV sio kufa ni kuishi kwa kujipenda na furaha. Ukihitaji msaada wangu wa ushauri wa akili nitafute nitakusaidia. Usife moyo dada yote mapito kwani Mama yako anakupenda sana na sidhani kama alitamani akuzae ukiwa na hali hiyo.
Jamani dada Lucy usife Moyo Mungu yupo
ReplyDeletemany people, еxperienсing tantric massage, аre ѕtunned at the profunditу bailar al
ReplyDeletemismo tiempo que realizа el masaje, еl bailе se cree que desbloquea, estіmula y ampl�а los niveleѕ de eneгg�a.
Whеther it's with quarrel, by a groan to the desire itself and recognize it as an free energy that is both within and all just about us. many couples find that all over meter the liaison and cacoethes fade because of the the other half of the Cloak-and-dagger... tantric massage substance a method to would feel if her child does not have the spunk to be pierced.
ReplyDeleteMy web blog :: erotic massage london
Mi nadhani Lucy usivujike moyo na kujiona wewe kama ndio wa kwanza kuwa na virusi vya ukimwi. Muombe Mungu akutie nguvu na umwambie huyo mpenzi wako. Naamini kabisa atakuelewa. IN GOD WE TRUST.
ReplyDelete