Social Icons

Pages

Friday, July 29, 2011

Mood Swings....

Mood Swings sijui nizitafsiri vipi kwa Kiswahili... Labda niseme ni kubadilisha hisia mara kwa marra.. For Example leo una furaha and unacheka na kufurahi with everyone, Kesho ni mnuno mwanzo mwisho. Kwa wanawake wengine tunapokaribia our "special days" hua tunakua sana na mood swings.
Kwa mimi personally, mood swings zangu zinakuja siku yoyote, anytime... Yaani niweza niamke sijiskii kuongea na anyone and kiukweli that day labda nitawajibu maboss wangu tu wataponiuliza some questions. But for wenzangu - wanakoma! Some days niko extra happy! I hug and smile at everyone. My mood swings haziishi kwenye hisia tu, inashuka kwenye hadi mavazi yangu. I might have a week ya hasira - ntavaa hovyo hovyo vululu vululu! I might even wear gauni za kushindia home na kwenda nazo ofisini! My hair? You dont want to know! Yeah its that bad! But when I'm extra happy daaah!!! Utanitaka! Ntavunja kabati!
Swali langu linakuja... Je, wewe kama mwanamke - hua unasumbuliwa na mood swings? Na labda za kwako zinatiririka hadi wapi? Share nasi... Have a beautiful weekend - my fellow beutiful Woman...
xoxo

Wednesday, July 27, 2011

Welcome....

Welcome kwenye blog hii.. Kama jina la blog linavyosoma, itakua zaidi inaongelea Mwanamke pamoja na Changamoto, maendeleo na maisha ya mwanamke in total... Lugha itakayotumika humu itakuwa Swanglish... Si unajua tena Kiswahili kuna upungufu kidogo kwenye maneno kadha wa kadha...
Mimi kama mwanamke wa Karne ya 21 nimepitia mengi, ila nina uhakika wewe binafsi, mke wako, mama yako, dada yako au hata rafiki wako wa kike atakua ameyapitia haya haya au kuna mwanamke that she knows aliyepitia the same experience.
Nianze tu kwa kukukaribisha hapa... Na kukuomba uwafahamishe na wenzio kuhusu blog hii. Tutapata muda mwingi tu wa kuweza kuhabarishana na kushare kuhusu mambo tofauti tofauti yanayomkabili mwanamke wa Kitanzania na Wakiafrika kwa ujumla.
I'll be honest, ndo kwanza naanza blogging, so nakuomba ntapokosea feel free kunikosoa na ntapopatia dont hesitate kunisifia, itanijenga sana sana..
Welcome and asante sana in advance....

Yours Truly,
Barbara Hassan
 

Sample text

Sample Text

Sample Text