Social Icons

Pages

Monday, June 25, 2012

Hook Me Up....


                                           

Hellow....
Kwema? How was the weekend? Yangu ilikua poa tu nashukuru.. Nililala weekend nzima! Nimekuja ofiisini asubuhi nikiwa sooo refreshed...
Anyway I know wanawake wote tuna girl friends, mashosti wengi wengi tu, wengine tuko nao closer kuliko wengine. Na pia kwa vile mie ni mwanamke na pia nina friends nina uhakika yatakuwa yameshawahi kukutokea haya. When una boy friend, na shosti wako yuko single - wengi wao hua wanaomba uwa hook up na rafiki za boy friend wako, au hata labda na kaka yako, uncle na kadhalika!
What do we expect? Labda hua tunadhani kwa vile labda your boy friend ana vigezo na tabia njema then marafiki zake pia watakua the same? Au tunataka kuunganishwa (kua hooked up) ili twende on double dates?
Personally, all the hook ups ambazo nishawahi kupata hazikufaa. Nilikimbia mwenyewe!!! Wanakua sio what you expected...

Hii ni tabia ambayo wanawake wengi tunayo, tusidanganyane... Swali ni kua - does the relationship work hata ukiwa hooked up? Ishawahi kutokea kwako na upo na huyo mtu till now? Au iliishaje? Ningependa kujua tu.... Let's share...

Funguka...

Email me - barbshassan@gmail.com
or SMS -0 +255 759 008500

xoxo

Thursday, June 21, 2012

Mamaangu ni Rafiki Yangu...


                                       


Mambo zenu?
Personally mimi sikupata bahati ya kuwa karibu na mamangu mzazi kwa sababu alifariki nikiwa mdogo, ila nililelewa na bibi (mamake mama) na mama mkubwa. Ambao hawa walinilea kama mwanao kabisa na mimi nikawapenda, kuwaheshimu na kuwa karibu nao kama mama zangu kabisa. Kile ambacho ningetakiwa kumwambia my mum nilikua nawaambia wao, na kile ambacho nilitakiwa nimpe mama yangu niliwapa wao. Niliwaonea sana wivu wale waliokua wakipeta na mama zao wazazi, akija shule "mamangu hivi, mamangu vile."  But nilizoea baada ya muda.
Anyway my point kwa leo ni kuwa my son sikuweza kua karibu naye kwa sababu I was busy na chuo na kazi. Mara nyingi nilikua sipo nyumbani. Yeye akawa close to my kid sister Eugenia. Hapa pia nikawa na wivu, nilitamani kweli niwepo home mara nyingi ili niwe closer to my son. Lakini nilikua namtafutia future kwa hiyo nikavumilia tu.
Baada ya kupata mtoto wa pili Ashley, nikasema hapa ndipo. Huyu sasa kaja wakati I'm settled, so nitajaribu niwezavyo kuwa very close to her. Na imetokea hivyo. Wanasaikolojia wanasema kuwa wakati wa kutengeneza bond na mwanao kama mzazi ni toka akiwa mdogo. Akishafikisha miaka 12 kama hakuna bond basi sahau. Right now nashukuru Mungu because my daughter ananiambia kila kitu, chochote anchowaza, chochote anachopitia. Yaani akitoka shule tunakaa chini anaanza kunielezea ilivyokua shule siku hiyo, what she learned, marafiki zake, walimu wake, ananiimbia. Na usiku kabla hatujalala anasali with me, ananiambia hadithi za shule - au mara nyingine mi ndo namuelezea. She wants to know about my colleagues at work, kama nina vikao the next day, yaani ratiba yangu nzima. Wakati she is only 5. Sio kua najisifia but namshukuru tu Mungu kua at least - baada ya kukosa kuwa close na mama mzazi, my kid sister na my son - Mungu amenipa another chance.
Je wewe, mama yako ni rafiki yako? Hua munaenda saluni pamoja? Harusini? Munapika wote? Munapiga story/umbea? Je, hua unapata chance hata kwenda for dinner wewe tu na mama yako? Kuongea about maisha ulikotoka na unapokwenda? Na siongelei right now tu ila hata zamani wakati unakuwa. Kiukweli hakuna rafiki kama mama, mama aliyekuzaa, mama aliyekupa unconditional love, mama atakaye stand by you hata kama wewe umekosea, mama atakayesimama katikati pindi baba anapotaka kukuchapa, mama anayeweza kufa kwa ajili yako.
Tuwape mama zetu chance ya kuwa close na sisi, na hata kama hukuweza kufanya before na bado yu hai, unaweza kuanza sasa. And from her utaweza kujifunza how to be close to your own children.
Kwa leo ni hayo tu... Nimetoa yangu ya moyoni...

xoxo

Kwa maoni au story yako - Email - barbshassan@gmail.com
or SMS - +255 759 008500

Wednesday, June 13, 2012

Jamani - Balaaaa

Jamani jamani.. Mimi kama mwanamke wakati namnyonyesha mwanangu nilikua naona aibu kutoa nyonyo mbele za watu. Sasa imajin na utu uzima huu eti nimtolee mwanaume nyonyo hadharani anyonye kwa raha zake. Coz kwake sio chakula!!! HAHhhhahahahah..
Kumeingi mtindo huu mpya nchini Ghana wakaka watanashati wadogo wadogo kiumri wakienda out kwenye clubs wananyonya maziwa ya madem zao nje nje bila aibu!
Swali - I know hao wanaume hawataona aibu kihivyo, lakini kwa wadada je? Na hizo night clubs kwa nini wasiwakatalie kufanya hivi?
Je, wewe unaweza kuthubutu to do the same?

Have a lovely day,
xoxo

Maoni Email - barbshassan@gmail.com
SMS - +255 759 008500

Tuesday, June 12, 2012

Shopping...


            
(Photo courtesy of Fotosearch)
                   
Hello,
I know hua unafanya shopping za namna tofauti tofauti.... Na kama sio kila mara at least mara moja kwa mwezi. Shopping ya chakula, ya vitu vya nyumbani kama (mashuka, vyombo nk), shopping ya nguo, accesories nk. Sijui kama hua unaandika list ya vitu unavyoenda kununua or not. I always do. Kwa sababu nisipoandika najikuta nanunua vitu nisivyohitaji na kusahau vile muhimu.

Anyway hilo ni la siku nyingine. Kwa leo nataka niongelee watu ambao na wao wanafanya shopping, mara nyingi inakuwa wanawake wenzetu. Specifically wakati tunafanya shopping za nguo, accessories, viatu, nywele. Wapo ambao hawajui wanachotaka na wengine hawajui kuchagua. Kwa hiyo wanakua wanaotea kukuangalia waone unachagua nini kisha wanadandia na hata kudiriki kukunyang'anya mkononi. "Oohh jamani nilikua natafuta sana sketi ya rangi hii" au " "uuuwwiii yaani nimesubiria sana kupata nywele za namna hii" Kisha anajifanya anaangalia angalia anakibeba na kwenda kulipia. Wanakuacha wewe umetoa macho hujui hata kinachoendelea. Kwa kweli I dont like hii tabia kabisa. Why utumie macho yangu kuona vitu vizuri? Mie ishanikuta sana. So hua nikiwashtukia watu wa na namna hii nitazunguka tu kwenye hilo duka bila kuchagua kitu hadi waondoke. Manake watanizingua nijikute nagombana nao bure.
Kama hauko sure na unachohitaji kwa nini usimuombe msaidizi kwenye duka husika akusaidie? That's why wapo pale.

Hata kwenye Supermarkets mtu anakuja hajui alichofuata, anakufuata nyuma kama mkia, ukienda section ya chakula yupo nyuma yako, ya sabuni - huyu hapa, ya toys - bado yumo. Kila utachochukua na yeye anabeba. Na anaweza akakuuliza kabisa - eti hii shampoo ni nzuri eeh? Mie hua hata sijibu. Kwani alikua akitumia shampoo ya aina gani all through?
Anyway, yashakukuta? If yes ulifanya nini?
Funguka...

Kwa maoni Email me - barbshassan@gmail.com
or sms - +255 759 008500


Siku njema
xoxo

Thursday, June 7, 2012

Women In Balance...

Usipitwe mdau wa wanawakenisisi. Haya si ndio mambo yenyewe sasaaaa... See you!!!!

XOXO

Kwa maoni - Email me - barbshassan@gmail.com
or SMS - +255 759 008500

Monday, June 4, 2012

Nisaidie...


                                        

Hello Barbara,
Im sorry na share nanyi stress zangu jumatatu.. But sikujua nitapata wapi usaidizi. Mi ni mdada nimeolewa na nina watoto wawili wavulana. Mmoja ana miaka 7 na mdogo ana miezi 8. Naishi na mume wangu pamoja na mtoto wa babangu mdogo (cousin wangu) ambaye hunisaidia kazi za nyumbani ila hua namlipa mshahara.
Amekua akifanya kazi vizuri tu, kunisaidia kulea wanangu na hata kuwasaidia na homework pindi ambapo mimi na mume wangu tunachelewa kufika nyumbani.

Juzi ijumaa cousin wangu alitoa kali ya mwaka. Mimi pamoja na mume wangu tulikua kazini, na mwanangu wa kwanza alikua shuleni. Cousin wangu alibaki na mtoto mdogo kama kawaida. Cha kushangaza niliporudi  nyumbani mida ya saa 10 na nusu nilikuta mlango wa nyumbani ukiwa wazi. Nikaingia nikamuita cousin yangu bila majibu. Kuingia chumba cha watoto nikamkuta mwanangu mdogo kalala kwenye kitanda chake akiwa mwenyewe na wa moto ajabu. Amejikojolea, kujinyea na machozi yamekauka katika macho yake.

Nikaenda kwa jirani kuuliza kama wamemuona dada, wakasema aliondoka toka asubuhi. Si ndo mie kushtuka. Dada wa nyumba ya jirani akanambia amemuona bar ya jirani. Na wakasema wamemskia mwanangu akilia siku nzima. Imagine mtoto wangu kumbe alikua hajala, hajaogeshwa, hajabadilishwa pampers siku nzima. Nilisikitika sanaaaa. Nikampikia mtoto na kumlisha, nikamuogesha akalala. Nikakaa kumsubiri dada, aliingia nyumbani saa 12. Yuko njwiii kalewa balaaa...
Hivi kweli angenambia nini nimuelewe? Alishindwa nini kununua pombe na kukaa anywe ndani ya nyumba huku akimuangalia mtoto? Ni unyama wa namna gani huu?
Sasa leo nimeshindwa hata kwenda ofisini niko nyumbani. Sijui nitaanzia wapi kutafuta dada mwingine. Naomba please wadau wa blog hii munisaidie..

Claire
Dar Es Salaam..

 

Sample text

Sample Text

Sample Text