Social Icons

Pages

Friday, October 28, 2011

Wasaidizi wa home kwetu...

Hellow...
Nani kanimiss??? Hehehhe najipa maujiko tu.. Hahha.. How are you jamani? Kwema?
Kuna group flani nimeijoin kwenye BBM ( BlackBerry Messenger) ina watu kama 14 hivi.. Most of them ni wanaume.. Ladies tupo kama wanne tu. Sasa Juzi si kuna mtu akalianzisha.. After a while, nikamuelewa. Alikua anatuambia tujaribu kufikiria - wasichana wa ndani al maaruf kama maids, beki 3 (no offence), dada etc hua wanatongozwa sana - wote tunalifahamu - question is nani hua wanatongoza hawa dada zaidi and sometimes kuingia kwenye nyumba zetu wakati sie tupo at work?
Unajua hawa machinga? Wanazungusha vibanio, earings, pete, chupi, shower caps etc.. Hua wanagonga kwenye mageti/ milango yetu wakati sisi hatupo wanajua watamkuta dada.. Dada mwenyewe labda amekuomba umhifadhie salary yake every month hadi siku anakwenda salimia kwao ndo umpe apeleke.. But huishi kumuona kaanika new panties na bra, ana hereni mpya, mabangili kibao nk..
Eti hua machinga wanawapa madada hivi vitu bure? Wanalipa kwa fadhila? Fadhila ipi? Shtukiza kurudi home one day majibu utayapata..
Huo ni mtazamo wa some of the people nlokua nikiongea nao....
Mie simo!!!!

                                            
have a lovely weekend
xoxo

PS...Ukiwa na maoni or anything unataka kuniambia privately wasiliana nami through SMS - 0759 008500
or email barbshassan@gmail.com

Tuesday, October 25, 2011

Sharing is Caring...

Hellooowwww...
Weekend iliindaje? Mmmmhhh.... Ulipitia na kuchunguza about size? hehehhehe.. Mwenzanguu nilisemwaaa.. Hahhaha - I knew it was gonna happen anyway. But si nilijikosha mapema nikasema nitakuwa honest and bold? So no problem..
Anyway, unakumbuka siku nili share nawe siri ya lile Duka la nguo na accessories amongst other things la Navo's Choice - well niliku promise kua the minute kukiwa na Sale (hata mie nasubiria) au kukiletwa New Arrival nitakutonya. Bora kujiset mapemaaaa badala ya kusubiri kupigana vikumbo on Chrismas Eve.
Sooooo ladies and ladies..... Behold....Kiukweli Ugonjwa wangu ni dresses...


HandbagsMore dresses.. Nisameheni...

                               Skirts!!!! Yaaaaayyy!!!

                                                         

Ok.... Lemme run nakwenda Navo's Choice kabla vitu havijaisha! Isiwe taabu! hehehehhe!!!! Usisahau maeneo ni paleeeee karibu na Barclays Mikocheni kwenye yale maduka mengiiii.. Navo's Choice New Arrivals!!! Jamani tukutane hukooo...


xoxo
Good day..


                                                                                            

Friday, October 21, 2011

Does size matter???

                                                                        


Hellow...
I knoooowww.. Ni swala ambalo wanawake wengi tu tunalikwepa. Kwa mfano mwanaume akikuuliza swali hili - What/how will you answer it?Mmmmhhh.. Mtihani!
Mi nishawahi kuulizwa na sio once or twice - hua nina jibu langu nimelikariri! Nikwambie? Hahhaah No way!!! Tutaonekana wote tuna the same answer - kisha tutaonekana we taught each other...
By the way  siongelei size ya phone, pencil, fingers, shoes, height, handbag etc.... Naongelea manhood. (Yeah I've decided to be bold enough) Coz tunakwepa sana!
But inabidi kwanza tuangilie kwani an average manhood inatakiwa kua na urefu gani?
Ikiwa erect, iwe na urefu wa kati ya 5.5 inches na 6.2 inches na around iwe 4.7 had 5.1 inches. Ooops!!!
Basi nikawauliza few of my close friends kama manhood size ina matter kwao - walichonijibu sasa...
"Ndio, tena  kwa sanaa.. Lakini mwisho wa siku inabidi tujiulize unapata satisfaction?" Sasa hawa nao wakauliza swali.. It got me thinking.. Sometimes kumbe wanawake tunaweza kulalamika about things ambavyo havipaswi kulalamikiwa. I mean think about it, Sawa ana a small manhood - but unapata satispafction ya uhakika hadi unafika cloud 9, why would you complain? Hahahahah!!!
Na wee baba/man/guy/husband/fiancee/boyfriend - hata kama you have a small manhood inabidi ujipange kumsatify mwenzi wako - ili asikutoroke au ku cheat! I told you I'll be very bold and honest leo!
You guy should look for other way za kumfurahisha mwenzi wako - Kama ina maana going down on her - do it! Ikimaanisha kutumia your hands - do it. If it means kutumia vibrators ili kumfurahisha mwenzio then go ahead and do it! And by the way hiyo inakua before you enter her na kumaliza haja zako!

                                                     


Let me ongea na wanaume tena - Umeshawahi kukaa and ask yourself why a woman anakutwa akicheat na house boy, dreva wa mumewe etc.. Its the satisfaction!!!!! Satisfy her uone kama atakurupuka tena and do something shameful! I dare you guy!!! This weekend mustoke wala nini - kama your manhood sio kubwa - kaeni humo humo ndani and go for a weekend getaway - na somo liwe - Satisfyinfg her. Kisha muangalie for a whole week kama kuna tofauti yoyote.
Atakua ana glow, ana furaha all the time, mnuno na kuvuta mdomo no more, Atawahi kurudi home na kukupikia your favourite food, nyumba itajaa furaha na hapiness.. The relationship will be kama mpyaaa..
Sitanii- jaribu uone.. Kisha munipe feedback..

Wanasema - kizuri kula na wenzio - I just did...


                                                          


have a lovely weekend
xoxo

Wednesday, October 19, 2011

How To Save......

 

Hello,

Umeamkaje? Jana kwenye gazeti la Citizen top page kulikua na habari kuhusiana na mfumuko wa bei na kua its getting worse. By the end of this year 2011 the inflation itapanda hadi 23%. Kwa wewe na mimi ina maana gani? It basically means kila kitu kitapanda bei!!! The goverment imetuomba you and I kuanza ku save. Manake ukizingatia kua WaTanzania hatuna tradition ya ku save, inakua taabu tupu. Inabidi tujifunze hata kama ni shilingi elf 10 tu kwa mwezi ambazo unajihakikishia kua hutozigusa...
All in all lazma tuanze jambo kama hili tukiwa wadogo - ila tusi blame wazazi (baadhi) kwa kutotufunza ku save. Maanake hii ni tabia unakua nayo.Anyway, tunaweza kuanza hata now kujifunza ku save.. Its not too late..

 

 • Usitumie zaidi ya  kipato chako. Kuna msemo "Champagne Taste on a Beer Budget" - watu kibao tu wanatumia more money zaidi ya kipato chao... Tunajijua..Kisha ukizingatia kwenye mshahara wenyewe unakatwa PAYE, NSSF au PPF, Bank Loan etc hela inayobaki inakua finyu. Kisha hiyo hiyo ilobaki you want to live a more lavish life than you can afford. Inakua ngumu... Kwa hiyo ni muhimu sana kupunguza unncessary spending. au labda uombe kuongezwa mshahara! heheheh! As if!!!
 • Jilipe wewe kwanza. Kuna a Financial expert anaitwa David Bach, muandishi wa kitabu Start Late, Finish Rich  anatuambia wote tusing'ang'anie sana kwa kuandaa “family budget”  kwa sababu moja tu: It doesn’t work- Na kama ingekua ina work basi wote tungeitumia na wote tungekua rich.  According to Bach, as long as tuna save asilimia kadhaa ya mshahara wetu kila mwezi, jinsi tutavyotumia kinachobaki doesnt really matter.Hiyo unayosave ndo unajilipa manake kinachobaki si inabidi utumie kununua other stuff? 
 • Usiige majirani/marafiki. Sawa, your neighbour au rafiki and bonge la swimming pool, jacuzzi, Range Rover 2 na Hummer 3, but maybe ana bongeee la mkopo huko Bank! Analipia kwa kugugumia. Usi ggive in into social pressure - yanakuwa yaleyale "Ooh Flani kapelekwa Dubai shopping na mumewe na mie lazma nipelekwe" Dont... Its very silly. Angalia mfuko wako...
 • Lipa madeni yako. Kwa mf. Bank loan, mkopo wa gari kwenye Yard/Show Room. Ili usijilimbikizie madeni mengi, utaumbuka bureee...  

General Spending

 • Save kwenye kununua gari - instead of a brand new car in a showroom - kwa nini usinunue second hand? Mind you hata kama umenunua a brand new car - ukitoka nalo to showroom its value starts depreciating.  Baada ya mwaka 1 au 2 - value inashuka even more.. Huwezi kuliuza kama ulivyolinunua... You've saved kama umenunua second hand... :) 
 •  Nunua DVD's, CD's vitabu na vifaa vya sports vya mtumba. You'll save.  
 • Gucci, Prada, YSL, Christian Dior, Baby Phat etc... Nguo, mapochi, scarves, saa za hao designers ni expensive!!!!! Kama unataka kuvaa nguo za designers - nunua za mtumba! Nguo haziongezeki value hata siku moja - hua zina depreciate.. today a style - kesho? Heheheheh... "Oohh nataka nivae gauni la Prada kam Kim Kardashian" Those celebrities wanalipwa to wear those clothes!!! Na pia hizo nguo sometimes wanapewa bure!!! Ili wewe ukiwaona hao celebrities wamevaa utakimbia to shops to buy the same!

                                                              

PS. For you to save more - usinunue nguo, viatu handbags karibia na sikukuu kubwa kubwa kama vile - Chrismass, Eid, Pasaka... Kua unafanya window shopping kila wakati ili watapofanya Clearance sale uwe wa kwanza kujua and that way uta save more... Na pia kuzunguka huko kutakusaidia wewe in comparing prices...

Savings

 • Saving Money ni tabia chanya, sio hasi. Wazazi wanao save pesa automatically wanao pia will be good savers. Tabia can turn kua addiction - sio mbaya ukawa addicted to saving na kushuhudia pesa zako zikiongezeka.
 • SAve shilingi 100 kwa kila elf 1 unayopata. Iwe your rule kabisa - mambo ya 10%. Jaribu kufanya hesabu kama ungesave shilingi 100 kwa kila elf 1 ambayo ulishawahi kuwa nayo ungekuwa na hela ngapi now?  
 • Kuwa na Emergency Fund yenye thamani ya miezi 3 ya mshahara wako. Hii inakua in case of kuumwa, accident au kuachishwa kazi, unakua una hela yako pembeni tayari tayari.

 Kumbuka...

 • Pesa ni Important, but sio kila kitu. Afya na furaha ni vitu important zaidi in life, but haimaanishi kuwa uwe mjinga with your money.  Fighting and wasiwasikuhusu pesa wont solve matatizo na kiukweli inaweza kuharibu kabisa afya na furaha yako! Tayarisha plan yako, malengo and focus kisha utanambia! 

                          You know what - acha na mie nifuate my own advice.. Im starting to seriously save.. Who's with me?

siku njema wapendwa,
xoxo                      

Tuesday, October 18, 2011

Unafanyaje ili guys wakushobokee All the time .....

 Hello,
Missed you jamaniii... All well? Kwema kabisa? Nina uhakika una marafiki ambao labda sio warembo ki hivyoooo lakini wanaume wakiwaona wanawafukuzia vibaya mno... Unawanuniaje? Unaweza hata ukawachunia and never go out with them! Uongo?
Umeshawahi to ask yourself nini hasa kinasababisha that? Wengine watasema - Ana nuru ya kupendwa, wengine watasema bahati - au it's the same thing? Hehhehe... Ulidhani ni labda mavazi sexy tu? Dressed to kill wenyewe wanasema? Kuna vitu vingine kibao!
Kuna vitu different ambavyo vinawasababisha hao wanaume kuwaona hao madem ni  irresistible! Chek this out:
NOTE:  Zaidi ya 50 per cent ya communication is done kupitia body language na vitendo. Na mwanaume ana decide within sekunde 7 za kwanza after meeting you kama you are worth it au la!

Dress to Kill
• Even though miraba na animal print ndo style iliyopo now, rangi  moja tu katika gauni au top ina show off power na uaminifu. Avoid all black as inakufanya uonekane uko serious sana au bossy!
• Kunyoosha gauni au shati lako ambalo labdo limekunjika kidogo au labda lina vumbi kidogo - shows a guy kua you want kuonekana good for him. Atanogewa!
• Yes, men wanapenda a woman in heels, lakini ukiwa umevaa heels kisha ukavua kile kiatu kidogo tu kikawa kinabembea shows kua you have a playful mind and kua hutaki kuondoka. Hehehhe.. Mwenzanguuuu... Unapochora nne hakikisha ule mguu ulio juu haumuelekei huyo jamaa - uwe unaelekea away from him. Ukiwa unamuelekea yeye it means you dont want anything to do with him.
• Ili kumchanganya zaidi, vaa gauni strapless au top ambayo haina mikono. Wakiona shoulders wanawaza jambo moja tu - BOOBS!!! Ukicheka jisogeze sogeze umuonyeshe a little bit of what you have.. Uwwwiiii!!!
Kick Back and Relax
• Egemea kwenye meza ya bar na one arm ili usionekane rigid au mzito. Ukisimama ukiwa stiff unaonekana kama hutaki kusumbuliwa. And tunajua wanapenda sana confidence in a woman but usisimame na mikono yako kwenye hips.
 • Usijinyooshe sana na kuonekana kama you are looking down at him. Instead shusha uso wako chini kidogo kisha umuangaliae - it's cute. Pia ukiwa umekaa usi cross ankles zako - inaonyesha kuwa hutaki kuwepo pale at all!
• Kama wee ni mtu shy, Simama katikati ya kundi la watu - utaongea zaidi na utaonekana you are popular - atakufuata mwenyewe!                                                               
"The body is meant to be seen, not all covered up." ~ Marilyn Monroe

Have a beautiful day,
xoxo
 
 
 
 
 
 

Thursday, October 13, 2011

Kiapo Cha Ndoa...

                                                      
                                          
Hellow,
Najua... Nimekua silent kwa muda. But jamani musiniseme sanaaa.. Hehehhe...I'm sorry...
Hivi have you ever sat down ukajaribu kuangalia, kusoma na kuelewa vizuri kile kiapo cha ndoa ambacho wanandoa hubadilishana in church? Na kama you have - do you think watu watathubutu kuachana ikiwa wamei memorise na kujikumbushua kila wakati mwenzi wako anapo mess up? Tucheki the traditional wedding vows ambayo imekuwepo na kutumiwa for ages:

"Do you, ____, take , ____, to be your (husband/wife), to have and to hold, from this day forward, for better, for worse, for richer, for poorer, in sickness and in health, until death do us part.
I, ____, take you, ____, to be my (husband/wife). I promise to be true to you in good times and in bad, in sickness and in health. I will love you and honor you all the days of my life."
The priest will then say aloud "You have declared your consent before the Church. May the Lord in his goodness strengthen your consent and fill you both with his blessings. That God has joined, men must not divide. Amen."

Although kuna wengine hua wanapenda kuandika vows zao wenyewe which is good kwa sababu unasema kilicho moyoni.. Swali langu ni kua - Hua wanawaza deeply about wanachosema and hua wanakumbuka vows zile everytime au kwenye anniversary?
Tukumbuke kua kuingia kwenye ndoa is not like unakwenda nunua gari so you can do a test - drive before! You are choosing mwenzio utakaye ishi naye maisha milele - baba/mama wa watoto wako. "Through thick and thin, sadness na furaha, kupanda na kushuka" 
Sasa wee unataka uwe naye wakati wa furaha na mali tu - akifilisika au wakati wa matatizo unataka time out? Weeeee!!! It Doesnt work like that! Ndio maana tunaambiwa tuwajue wanandoa wenzetu kwa undani zaidi before kutamka the vows. A marriage is not made to be broken. Kama mume/mke wako ni muongo, mzini, mwizi, two timer, kikojozi, one minute man - lazma uyajue haya mapema and accept hali halisi au jinsi ya kumsaidia mapema. This is before you go mbele ya Mungu na kadamnasi na kutamka vows kwa moyo wako wote!
The vows is where it all begins baada ya pale there's no going back.
Kama ndo unajiandaa andaa for a wedding au ndo kwanza kwenye uchumba and you have a good feeling kuwa relationship yenu inaelekea pazuri - kamuombe your priest vows kabla - zipitie, zisome, zielewe then ukiona sawa - go ahead and marry that person....
And make sure unazikumbuka kila wakati kama your favourite song and ikiwezekana every anniversary ya wedding yenu mukumbushane hizo vows kwa kuambiana tena..

I'm not married - but huu ndio mtazamo wangu...

contact me - barbshassan@gmail.com au sms 0759 0078500

            
                                         
Have a lovely Nyerere Day kesho and a superb weekend after.
xoxo

Friday, October 7, 2011

Weekend Shopping

Heee.. Si nilisahau.... I know kabisa kua women ndo hua tunafanyia our children shopping zaidi ya kina baba.. So if unahitaji vitu kwa ajili ya your child basi usisahau kupitia Mini Argos - hata kama ni window shopping wakati unajiandaa andaa kutafuta some cash ili uvirudie hivyo vitu...
Mini Argos wameleta mzigo mpya and by the way its a show ambalo lina deal zaidi na children and a little bit - women...


Kwa ajili ya new born - bibs, shawl, shoes nkMafuta na powder for the babyToys, bakuli, sahani na water bottles za different characters.. Mwanao hajawahi kukuomba umnunulie sahani ya Ben 10, mwavuli wa Barbie, Lunch box ya Hanna Montana... Haya kazi kwako!!!Haya tooth paste, shower gel na miswaki ya kumwaga - za characters tofauti. Whichever your child loves.


Mabegi... iCarly, Cars, Spiderman, Hanna Montana, Tinka Bell, Ben 10, Barbie, Princesses nk
Tshirt za watoto wa kiume....
Na wipes...Swimming costume for boys and girls, towels....Story books... Pencils, rubber, sets nk...Chupa za Maziwa za kweli....

Wamama hatujasahauliwa.. Bracelets, bangles, earings, lip gloss nkDuka linapatikana Msasani - Kimweri Road Karibu na Tirdo.
Au wapigie simu kwa maelezo zaidi - 0713 267267 au 0787 267267

Be blessed...
xoxo

Utajuaje He's cheating on you....

Hello....
Wiki hii I've been hanging out na watu tofauti tofauti. Jumatano I was with some old friends hapo Safari Carnivore in Dar Es Salaam. Tulikaa muda mrefu sana talking about different issues. Work, relationships etc. Baadaye one of the guys akaenda maliwatoni, he came back akanifuata mimi and told me "Kuna dada yuko Ladies analia sana, Kamsaidie." Nikanyanyuka and i went to the ladies, kweli, Nikamkuta a young lady analia hadi kutetemeka. So nikaanza kumbembeleza telling her - all will be and kua kulia hakutasaidia kutatua whatever she's going through. Akanyamaza then she hugged me. Kumbuka hatujuani. Akaniambia "I've been married for 2 years. Ila mume wangu amekua akini hurt sana lately." Mi nikanyamaza ili kumsikiliza. Akasema "I come from a very poor family and nina mtoto ambaye sio wa huyu mume wangu. When this guy alipoanza kunitongoza nilikataa becoz yeye ni tajiri sana na mie ni maskini sana. Nilimwambia naogopa kuwa naye coz watu watasema nimkubali kwa sababu ya hela yake. But yeye akaning'ang'ania na kusema nisiwajali watu as at the end of the day, it's about him and I. Nikaona kweli, and akanioa na kumu adopt my son. Sasa lately amekua akinishuku kua I'm cheating on him and mara kadhaa ameniambia I married him because of his money. Imeniuma sana sana." Akaanza upya kulia. Basi nikabembelezaa tenaaa weeeee... Then i told her - Jaribu kuchunguza,  maybe ni peer pressure. Labda washkaji zake ndio are telling him that. Na pia mtu kukushuku kua you are cheating labda yeye ndo ana cheat so anakuwahi kabla wee hujamuuliza. Mchunguze and chek if he has these following signs....

1. Si unajua kuna tofauti between having sex na making love. Sasa inakua mumeo/ boyfriend hamfanyi tena mapenzi - yaani hamna hisia za mapenzi katika kufanya lile tendo. Labda he is even thinking of  mtu mwingine while having sex with you. Umenipata?

2. Intimacy kwa lugha nyepesi ni Ukaribu. Ku express ukaribu katika relationship yenu inawezekana labda munashikana mikono, cuddling, spooning nk. Akiwa ana *mpango wa kando* huko nje ataacha doing these stuff with you...


Spooning...


3. Mwanaume anaye cheat will make sure nywele na ndevu zimekaa sawa - so atakua kila wakati anakwenda barber shop - atanyoa, scrub, massage, facial nk. Anaweza hata akaanza kufanya mazoezi gym ( na hapa ndo anaweza kutumia muda huu kuonana na *mpango wa kando*)

4. Kazi haziishi, kila siku anarudi home saa 6 saa 7 usiku na wala hajalewa. Ukimuuliza - oohh niliombwa na boss nifanye overtime - na hela extra huzioni. Mara oohh kulikuwa na farewell ya mshkaji ofisini. Mara natakiwa kusafiri kiofisi - every time.. Na kama anakwenda business trip - unaona kabisaa ana kimuhemuhe! He can't wait!

5. Kwenye wimbo wa Kidum - Mulika Mwizi, kuna sehemu kaimba - "Ukiona baby wako anaingia kwa bafu na simu mkononi - huyo ni mwiziiii.. Mulika Mwiziiiii! Kisha inaendelea - Ukiona mzee wako anazima simu kila mara akiwa kwa nyumba - mulika mwiziiii... " Nadhani hapo nimemaliza.

6. Anakula kiduchu home au anaumwa tumbo, Si katoka kula na mpango wa kando!!! Wee umejikaangia samaki wa kupaka na wali wa nazi, utakula mwenyewe! Kwa wale wanaojua kucheat kule kwa mpango wa kando hatafakamia sana...

7. Anakua muongo kupitiliza. Na anakuwa anajing'atang'ata mwanzoni but as days go by anakua better kujitetea. Na ukimbana sana anaku changia kabsa na kua mkali kupitiliza!

8. Anafungua a new email address and anabadilisha passwords za email adress that you know about.  Habanduki kwenye cpmputer. Ukimsogelea tu  he minimises all windows - or closes them altogether. Na akimaliza kwenye computer anafuta history

9. Anakuja home late kisha ananukia perfume ya kike, ana lip stick kwenye shati au on his cheek. Kisha anajibaraguza - ooh ntafua nguo zangu mwenyewe!

10. Anakua msiri ajabu!

11. Eti ghafla he wants to join a dancing class au kujifunza Kung Fu. Wakati alikua mtu anayekaa home tu na kuangalia habari na Sports all the time.

12. Condoms kwenye wallet au mifuko ya his trouser.

13. Kama muna watoto and you keep some toys za watoto in the car - atakwambia uzitoe faster!

 14. Anaanza kua interested na schedule yako na utakua unafanya nini.

15. Anakua na another mobile phone - na kuna uwezo mkubwa usiijue namba yake! Na ina password.

16. Akirudi home tu, huyo bafuni, takes a shower anabadilisha nguo then he comes to hug you. (Before alikua anaku hug kwanza)

17. Anafuta Incoming calls, SMS nk kwenye simu yake

18. Atakuuliza maswali kuhusiana na relationship yenu, What you think about it, Na labda what would happen kama mkiachana.

19. Havai his wedding ring .

20. When his phone rings anapokea then anakwenda kuongea room ya pili.

21. Anaanzisha fighta and anakasirika sana kwa vitu vidogo vidogo and then he leaves the house akisema ankwenda kupata "fresh air" - MULIKA MWIZI!!!!

22. Atasingizia foleni kwenda na kurudi kutoka kazini kumbe anapitia kwa "Kishtobe aka mpango wa kando" 

23. Anaanza kuondoka home mida ya ajabu - like alfajiri sana au usiku wa manane - eti naenda kuvuta sigara. Sometimes anaweza hata akasubiri for you to sleep then anaondoka.


Kama ana hizi signs.. aaaahhhh.. Unaibiwa kabisaaaa.. He is definately cheating..
Any more signs ambazo umezistukia? Feel free to add them.

* Mpango wa kando ni nyumba ndogo*

contacts - barbshassan@gmail.com  or sms 0759 008500

have a lovely weekend
xoxo

Tuesday, October 4, 2011

VITENGE AKA B2A ( Back To Africa )

            

                                                             


Hellowwww,
Leo asubuhi i received this message kutoka kwa a friend of mine

"Hi great lady, today's dress code is Kitenge to mourn Wangari Maathai - our Heroine.  Please send to all great ladies you know."

Wangari Maathai was and still is my inspiration - and ningependa sana nivae Kitenge leo ili kuomboleza kifo chake. Lakini wacha niwe mkweli.. SINA KITENGE chochote in my wardrobe.. I knooowww. Aibu eti eeh....
Siku hizi Vitenge vinashonwa kisasa zaidi - kuna shorts, nice skirts, very cute dresses nk. Yaani ukiniuliza why sina kitenge - nakosa jibu kwa kweli. Kwa mfano

Sasa sjui kinachonishinda ni nini.. Oohh i also saw a pencil skirt

Very simple and nice.. But ukitupia hapo with a nice lace shirt - si umeshamaliza? Anyway kuna umuhimu gani wa kuvaa Vitenge kama mwanamke wa Kiafrica?
-  Asili yake ni Africa - Kama kujitambulisha where you are from
- Kuendeleza utamaduni
-  Kulinda culture za Kiafrika
Wewe una vitenge in your wardrobe? Kama Yes, Why? Na kama No - Why?

have a lovely day
xoxo
                 
                                                

Monday, October 3, 2011

What our men do kwa wanaume that we cheat with....
Hello,
Weekend ilikuwaje? Mi nlijifungia.. heheheh.. Eti trying to save up - and i actually think i spend hela nyingi sana nikitoka! Sjui about you. Anyway, thats a topic ya siku nyingine. Ok kuhusiana na hicho kichwa cha habari hapo juu -  Not that I'm an expert on this or anything, bali hua nafuatilia sana story. Hua unasikiliza kipindi cha Leo Tena on cloudsfm? Anakiendesha Dina Marios - http://www.dinamarios.blogspot.com/  au sikiliza live from saa 3 hasi 7 mchana on http://www.cloudsfm.co/
Ndani ya kipindi kile hua kuna kipengele - segment anayoifanya Gea inaitwa - Hekaheka. Gea hua anazunguka around akitafuta vituko na story tofauti tofauti. I sat with her nikamuuliza katika story za Fumanizi wale waliofumaniwa hua wanapewa which punishment ipi?
Kwanza, she told me kua story nyingi za fumanizi - hua ni wanawake wanafumania waume zao - chache sana za men kufumania their wives! That means either wanawake hatu cheat sana kama wanaume - au sisi ni wasiri sana! Chagua moja! heheheheh!
Anyway nilimuuliza Gea - katika hizo chache za Wanaume kufumania wake/ girlfriend zao waliwafanya nini wale wanaume waliokamatwa wakiwa na hao wanawake?
Akaniambia :-

- Kule Tabata jijini Dar Es Salaam - Kuna jamaa alifumaniwa na mke wa mtu alitembezwa uchi wa mnyama hadi kwa mke wake!
- Kunao wanaume wengi washaliwa kiboga - sema wanaficha sana
- Kuna aliyevishwa kanga na shanga wakataka wamuoze kwa baba aliyefumania! Makubwa! Manake hawa walimbeba hadi Shekhe! HEhehheheheh
- Kuna wanaopigwa hadi wanataka kufa!

Pia kuna story niliona ilitokea nchini Marekani - jamaa alihisi kuwa mke wake ana cheat, akachunguza akamjua na huyo mwanamume anaye cheat na mke wake! So jamaa akaenda police akawaambia he senses someone has an affair with his wife. So huyo mtu ajisalimishe kwake mapema! Polisi wakasambaza the story, ikamfikia yule jamaa. Jamaa akampigia simu mume wa mtu kumuomba wakutane at a hotel kwenye room waongee. Mume mtu akakubali. Yaliyomkuta!!! Mume wa mtu akamkata yule jamaa uume kisha akijipeleka polisi mwenyewe akiwaambia - lile tatizo nishalitatua!

Wee mtu anamtunza mkewe akawa mrembo na mwenye afya na kupendeza na kunukia till wee ukamtamani! Unajua uchungu wake? Heheheheh!
Anyway - these are just some stories nilizopata. Unajua nyingine?
Tuhadithie....

                                      


PS. Nitakutonya wapi utaweza pata school bags, swimming costume, cotton vests and socks, lunch boxes na water bottles nk vya cartoon characters kwa ajili ya our children hapa jijini Dsm - keshoooo..

Have a lovely day
xoxo
 

Sample text

Sample Text

Sample Text