Social Icons

Pages

Thursday, June 21, 2012

Mamaangu ni Rafiki Yangu...


                                       


Mambo zenu?
Personally mimi sikupata bahati ya kuwa karibu na mamangu mzazi kwa sababu alifariki nikiwa mdogo, ila nililelewa na bibi (mamake mama) na mama mkubwa. Ambao hawa walinilea kama mwanao kabisa na mimi nikawapenda, kuwaheshimu na kuwa karibu nao kama mama zangu kabisa. Kile ambacho ningetakiwa kumwambia my mum nilikua nawaambia wao, na kile ambacho nilitakiwa nimpe mama yangu niliwapa wao. Niliwaonea sana wivu wale waliokua wakipeta na mama zao wazazi, akija shule "mamangu hivi, mamangu vile."  But nilizoea baada ya muda.
Anyway my point kwa leo ni kuwa my son sikuweza kua karibu naye kwa sababu I was busy na chuo na kazi. Mara nyingi nilikua sipo nyumbani. Yeye akawa close to my kid sister Eugenia. Hapa pia nikawa na wivu, nilitamani kweli niwepo home mara nyingi ili niwe closer to my son. Lakini nilikua namtafutia future kwa hiyo nikavumilia tu.
Baada ya kupata mtoto wa pili Ashley, nikasema hapa ndipo. Huyu sasa kaja wakati I'm settled, so nitajaribu niwezavyo kuwa very close to her. Na imetokea hivyo. Wanasaikolojia wanasema kuwa wakati wa kutengeneza bond na mwanao kama mzazi ni toka akiwa mdogo. Akishafikisha miaka 12 kama hakuna bond basi sahau. Right now nashukuru Mungu because my daughter ananiambia kila kitu, chochote anchowaza, chochote anachopitia. Yaani akitoka shule tunakaa chini anaanza kunielezea ilivyokua shule siku hiyo, what she learned, marafiki zake, walimu wake, ananiimbia. Na usiku kabla hatujalala anasali with me, ananiambia hadithi za shule - au mara nyingine mi ndo namuelezea. She wants to know about my colleagues at work, kama nina vikao the next day, yaani ratiba yangu nzima. Wakati she is only 5. Sio kua najisifia but namshukuru tu Mungu kua at least - baada ya kukosa kuwa close na mama mzazi, my kid sister na my son - Mungu amenipa another chance.
Je wewe, mama yako ni rafiki yako? Hua munaenda saluni pamoja? Harusini? Munapika wote? Munapiga story/umbea? Je, hua unapata chance hata kwenda for dinner wewe tu na mama yako? Kuongea about maisha ulikotoka na unapokwenda? Na siongelei right now tu ila hata zamani wakati unakuwa. Kiukweli hakuna rafiki kama mama, mama aliyekuzaa, mama aliyekupa unconditional love, mama atakaye stand by you hata kama wewe umekosea, mama atakayesimama katikati pindi baba anapotaka kukuchapa, mama anayeweza kufa kwa ajili yako.
Tuwape mama zetu chance ya kuwa close na sisi, na hata kama hukuweza kufanya before na bado yu hai, unaweza kuanza sasa. And from her utaweza kujifunza how to be close to your own children.
Kwa leo ni hayo tu... Nimetoa yangu ya moyoni...

xoxo

Kwa maoni au story yako - Email - barbshassan@gmail.com
or SMS - +255 759 008500

18 comments:

  1. Kiukweli, wakati nakuwa nilikuwa namkimbia kabisaaa mama yangu maana mimi nilikuwa namuona mkaliii sana. Ila mimi pia nilikuwa mkorofi kupitiliza...so ilikuwa kama paka na panya fulani...
    Sasahivi nimekuwa na nimeolewa..mama yangu tunaitana MASHOGA. Tunaongea sana na kushirikishana mengi (sio yote maana kuna baadhi ya mambo ni ya mume na mke)..na ananipa ushauri mwingiii na yeye pia huniuliza mengi na tunashauriana..tunaweza pigiana simu tukaongea kama 2 hours..tunacheka mpk raha. wengi wanafikiri naongea na shoga yangu au dada yangu na wanashangaa nikiwaambia ni mama yangu

    ReplyDelete
  2. barbara we are the same boat my dear, mimi ndo sijalelewa na mama hata siku moja mama yangu aliniacha nikiwa na mwaka mmoja akarudi niko std 2, akaondoka hadi leo sijui yuko wapi, nimeshaolewa niko kwangu, before sijaolewa nilikuwa nakaa na mama yangu mkubwa (dada wa mama yangu kabisa) but naye alifariki but wakati anafariki nilikuwa naishi na mama mkubwa mwingine(binamu wa mama yangu, mtoto wa shangazi yao mama) namshukru mungu amenilea akam mjukuu maana mama mkubwa yuko age kidogo, ananipenda, nami nampenda sana, kuliko maelezo, kuna bond iko hapa katikati yangu na mama yangu mkubwa huwezi amini nikiwa namuwaza tu halafu nasema nitampigia simu labda baadae au kesho yake, na yeye ananiambia alikuwa ananifikiria, I LOVE HER SO MUCH sina neno la kumwambia coz naona maneno yote ya kumwambia nampenda yameisha, sijui nisemeje kwa kweli, nakumbuka hata siku ya kitchen party yangu alilia sana kwa kweli, namshukuru mungu kwa kunipa mama mkubwa mwema katika huu ulimwengu, nampenda kuliko mamelezo,

    ReplyDelete
  3. Dah, love you mama.....
    Lk ukionesha upendo wote kwa huyu mmoja yule mkubwa ataona humjali sana na anaweza jenga tabia za ajabu, watch out sisy....

    ReplyDelete
  4. Barbara, spending time with your children and watching them grow and being a part of their day to day developments is priceless. But then again sometimes situations and circumstances dont allow this to happen no matter howw much we yearn for. So whats important is as long as you get an opportunity to spend time with your kids, always savor it coz such moments are always treasured for life and it also helps in building the childs, self esteem, personality and sense of belonging.
    i can relate to your story coz i wasnt able to be with my son Brian for 2-3 years coz i had to work and finish my studies and now that we are done with that i make it a point to spend alot of time with him and his brother Ethan you know them.
    Nice article mama. kudos and keep up the ggod work of enlightening and empowering women

    ReplyDelete
  5. Mada ya leo Barbara kwakweli imenigusa sana tena sana. Binafsi sikulelewa na mama yangu mzazi nimelelewa na mama wa kambo, kwa kweli alinitesa sana. Mama aliniacha kwa baba nikiwa na umri wa mwaka 1 na nusu, sikuwahi kumjua mpaka nilipofanya jitihada za kumtafuta nilipofikika form two. Hana mapenzi na mimi kabisa richa ya kujipendekeza sana kwake co'z mama ni mama.

    Nilikuja kukata tamaa ya mama baada ya kuolewa kwani alikuja kwe harusi yangu kwa kumlazimisha, na nilipopata mimba ya kwanza nilijifungulia ukweni pia hakutaka kuja kunisaidia wala kumuona mjukuu wake mpaka nilipofunga safari ya kumpelekea huko huko.

    Hivi sasa nipo chuo Mwanza, mtoto yupo Mkoani kwa bibi yake mzaa baba, mama kapita juu kwa juu kwenda kijijini kwao bila hata ya kupitia kumsalimia mjukuu wake. Kwakweli naumia sana. Kila nikikumbuka nalia sana.

    ReplyDelete
  6. In short nampenda sana mama yangu tangu utotoni hadi leo na pia nawapenda akina mama wote wenye hadhi ya kuitwa mama I mean wanaojiheshimu na kuheshimiwa pia. Nani kama mama

    ReplyDelete
  7. pole kwa wale wote waliopoteza mama zao.binafsi nampenda sana mama yangu ni kama rafiki yangu.nikivaa nguo nzuri namuwaza mama yangu nikila vzr namuwaza mama yangu najitahidi sana kumtunza na kumlea mama yangu.nina mengi ya kusema lkn nitajaza ukurasa huu.

    ReplyDelete
  8. pole sana.mi nimeshindwa kuelewa kama mama anaweza kushindwa kumpenda mtoto kiasi hiki kwa akili za kawaida.hata kama upande wa baba yako walimkosea alipaswa kusamehe na kumpenda mwanaye.other wise kama walimpiga kipapa akusahau.

    ReplyDelete
  9. kwa kweli kuna wengine tulikosa upendo wa mama, sisi mama yetu mzazi alikuwa mfanya biashara wakati tupo wadogo alipopata hela kumzidi baba basi akaondoka na kusema anaende kuolewa pengine na mtu mwenye pesa zaidi ya baba, kwa kweli tuliumia sana, baba ndio alitulea yeye peke yake na kuhakikisha tunapata elimu na malezi bora. mama wala hakuwahi kujali kama ana watoto yeye tukawa tunamsikia mara yupo huku mara kule, ila baadae maisha yake yalikuja kuwa ya hovyo kabisa, na baadae sisi tumeshakuwa wakubwa kila mtu na kazi yake tunamjali na kumtunza baba yetu, ki ukweli feelings za mama hazipa alitupa machungu sana na hata nikikumbuka natoa machozi, tulishamsamehe. yeye kila siku anatuombea mabaya kwa kuwa hatumjali lakini ni vigumu kama sinema vile...

    ReplyDelete
  10. Hii article imeniumaje. Nina watoto wawili wa kiume lakini niko mbali nao, nasoma. Nawapenda sana; hope nikimaliza nitaweza ku catch up with what I have been missing. Najitahidi kuongea nao kwa simu na skype daily. Walau wasinisahau. Nawaona once a year, na shule yenyewe ndeeefu. Naumiaje.

    ReplyDelete
  11. Dear All,
    Hii article imenigusa sana. Nampenda sana mama yangu kupitiliza and Im praying for her kila siku mungu ampe maisha marefu. Pia ambao hamkupata bahati ya kulelewa na mama zenu wapendeni wanawake wote ambao ni mama.
    Despite I love my mama kupitiliza, I wish I could a mum na mimi. Nimeolewa for the past 13yrs lakini sijabahatika kupata motto so natamani namim niitwe mama nifeel jinsi mama yangu anavyopata raha nikiwa nae. My mama is my best friend, my sister my everything is this world of god. Anyway I love all wan awake ambao ni mamas



    ReplyDelete
  12. In fact, we believe that childrеn are suсedе Durante el masaje
    tantric massаge? Usui tantгic mаssage pгactitionerѕ аnd
    teacherѕ of all sabia o que deνeria fаzer paгitу sеr aсеita no grupo
    ou como conѕeguir com elаs uma rеlа?
    ?ο mais pr?xima. Aftеrаll, "Do you remember how electric an opportunity to allow her to experience a assortment of different sensual sensations and rest that just you have the exponent to give her. The spa Sona and I the herculean Kundalini get-up-and-go.

    Feel free to visit my page: london tantra

    ReplyDelete
  13. It's very simple to find out any matter on web as compared to books, as I found this paragraph at this web page.

    My site sensitivity

    ReplyDelete
  14. I do consider all of the ideas you have introduced for your post.
    They are very convincing and can certainly work.
    Nonetheless, the posts are very brief for novices.
    May just you please prolong them a little from subsequent time?
    Thanks for the post.

    Have a look at my web page; pecan

    ReplyDelete
  15. Incredible! This blog looks exactly like my old one! It's on a totally different topic but it has pretty much the same page layout and design. Outstanding choice of colors!

    Here is my web page :: agent

    ReplyDelete
  16. Shukuruni kwa jambo, maana hayo yote ni mapenzi ya Mungu. Kila la kheri wewe familia yako!

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text