Social Icons

Pages

Wednesday, February 29, 2012

Wimbo Wednesday...( What makes you happy?)

Kama binadamu tunapitia mambo mengi sanaaaaa... huzuni, furaha and in between... ambavyo hivi husababishwa na different things. What makes you happy? Wewe kama wewe? Kuna wengine wakiachika kwenye ndoa wanaona rahaaa isiyo kifani wakati wengine wanatafuta ndoa, wengine wakitoa mimba wanaona raha coz wanaona wamejiepusha na mengi wakati wengine wanatafuta watoto, wengine wakistaafu kazi au wakiacha au kuachishwa wanaona wamefika baada ya kuchoshwa labda na an evil boss au kuchoka kuamka alfajiri na kushinda kazini badala ya ku spend time with their families, wengine wanatafuta kazi kwa udi na uvumba! We become happy kwa namna tofauti tofauti. Wengine wakipata mpenzi wengine wakiachika ndo wanafurahi coz labda ilikua a depressing relationship. Wengine wakinenepa duuuu furaha mwanzo mwisho, wengine wanafanya diet wapungue. Anyway pointi utakua umeipata. Lazma una lako jambo that if it happens unajua fika utakua the happiest person in the world.
Mimi pamoja na ku experience yote hayaaa... kama wewe... Nikiskia wimbo nikaupenda nakua sooo excited, nakua na furaha isiyo kifani. Nataka nimsikilizishe everyone who can lend me their ear.. That's why nimeanzisha Wimbo Wednesday ambapo hata wewe utakua na chance ya kuchagua wimbo wako na kutoa sababu why uwekwe humu. Video ikiwepo na ikikubali kua uploaded nitaweka ila ikikataa either nitaweka link ya the video au I'll stick to lyrics.
Kwa kuanzia - wema huanzia nyumbani. So leo nitachagua mie.. Huu wimbo I admit nimechelewa kuujua. Nimeskilizishwa on saturday by a close friend na nikaupenda wimbo huu kupita kiasi. If this song was a man, I'd make love to it all the time... (oops) Jamaa mdogo tu from America ndo kaimba amezaliwa 1987. Kisanii anafahamika kwa jina la Frank Ocean. Wimbo unaitwa Novacane.

                                       


NOVACANE
I think I started something
I got what I wanted
did-didn't I
can't feel nothing
superhuman
even when I'm fckg
viagra popping
every single record
auto tuning
zero emotion
muted emotion
pitch corrected
computed emotion
I blame it on the
model broad with the Hollywood smile
stripper booty and rack like wow
brain like Berkeley
met her at Coachella
I went to see jigga
she went to see z-trip
perfect
I took a seat on the ice cold lawn
she handed me a ice blue bong
whatever
she said she wanna be dentist really badly
she's in school paying
for tuition doing porn in the valley
at least you working
but girl I can't feel my face
what are we smoking anyway
she said don't let the high goto waste
but can you taste a little taste of

Novacane
baby baby
Novacane baby I want you
f me good
f me long
f me numb
love me now when I'm gone love me none
love me none love me none
numb numb numb numb

sink full of dishes
pacing in the kitchen
cocaine for breakfast
yikes
bed full of women
flip on a tripod
little red light on shooting
i'm feeling like
stanley kubrick
this is some visionary shit
been tryna film pleasure with my eyes wide shut
but it keeps on moving
I blame it on the
model broad with the hollywood smile
stripper booty with the rack like wow
I'll never forget ya
you put me on a feeling I never had
never had never had
and ever since
I've been tryna get it back pick it up and put it back
now I'm something like the chemist on campus
but there's no drug around
quite like what I found in you

I still can't feel my face
what am I smoking anyway
she said don't let the high go to waste
but can you tast a little taste of

novacane
baby baby
novacane baby I want you
f me good
f me long
f me numb
love me now when I'm gone love me none
love me none love me none
numb numb numb numb
novacane novacane novacane novacane novacane
for the pain for the pain for the pain for the pain for the pain
novacane novacane novacane novacane novacane
for the pain for the pain
novacane novacane

pretty girls involved with me
making pretty love to me pretty
pity pity
all the pretty girls involved with me
making pretty love to me pretty
pity pity
I can't feel a thing
I can't feel
can't feel a thing
I can't feel a thing

can't feel feel feel feel her
I can't feel feel her
novacane novacane novacane
I can't feel feel her
for the pain
for the pain
for the pain
I can't feel feel her
feel her feel her oh
novacane novacane-cane
            video on - http://www.youtube.com/watch?v=TMfPJT4XjAI

Enjoy your wednesday...
Kesho Tatua Thursday

Email me - barbshassan@gmail.com
Au SMS - +255 759 008500

Tuesday, February 28, 2012

Stori....

                                                   

Hi, kwema?
Weekend nilikua na washkaji zangu. Tumekaa na kupiga sana story. Sikumbuki how but tukaanza kuongea kuhusu madada wa nyumbani. One of my friends akaanza kutusimulia story ya dada wa rafiki yake....
Kuna mdada kaolewa na anaishi na her husband na watoto. Yeye na mumewe wanafanya kazi, watoto wanaenda school, so wakahitaji usaidizi wa dada atakayekua anawasaidia kazi za nyumbani - kupika, kufua, kufagia na kupiga deki nk... Sasa basi familia hii wakawa kila siku asuhubi wanaamka wamechoookaaaaa.... Watoto wanasinzia shuleni na wakubwa kazini. They always wondered how and why.
Yule mama wa familia akaenda kumueleza a friend of hers - rafiki akamwambia you never know labda munalimishwa usiku. Anyway twende nikupeleke kwa mganga akucheki. Wakaenda. Kufika mganga akamwambia "dada wenu wa kazi amekua akiwaamsha usiku na kuwafanyisha kazi zoooote. Mnachota maji, mnafua, mnafagia nyumba nzima nk. Yule mama ndo akafunguka macho hapoooo.Na kuanza kukumbuka kuwa wamekua wakishangaa how they wake up saa 11 alfajiri na kumkuta dada keshamaliza kazi zooote. Daaah.. Hii siyo ya kucheka kabisa.
Sasa huyu mama kwa kua alikua keshafunguliwa macho, usiku wa manane wakaamshwa na yule dada yao. Yule hapo ana ufahamu mzuri tu na anaona na anajua kinachotokea. But akajifanya mjinga. Dada akakaa kwenye kochi na kunyoosha miguu huku akiwa command. Wewe kachote maji, wewe kafue, wewe kaoshe bafu, wewe kapige deki. Yule mama akashindwa kuvumulia na kuanza kupiga kelele. Familia nzima ikazuinduka na majirani kufurika. Ndipo akawasimulia wakampa dada mkong'oto na kumpeleka polisi. I dont know hatma yake iliishia wapi.
Jiangalie na wewe. Usije kuta na wewe unafanyishwa kazi usiku kucha na your dada. Tafakari chukua hatua and pray a lot.

                             
                                              
PS. From now kila jumatano tutakua na "Wimbo Wa Wednesday" Ntakua nakuchagulia wimbo mmoja (haujalishi kama ni mpya au wa zamani na from anywhere in the world) upate kuuskiliza kwa siku hiyo...

Kwa maoni na maswali au kama unataka kutokeza kwenye Tatua Thursday feel free to:
send an email - barbshassan@gmail.com
au sms - +255 759 008500

have a lovely day..
xoxo

Friday, February 24, 2012

Tatua Thursday - On a Friday...

                                              


Hello..
Jana ilibidi nikakutane na mtu ambaye alihitaji tumsaidie kutatua tatizo lake hapa. Ni rafiki yangu wa kike for many years (jina kapuni). Alipokua University alikua na relationship with an amazing guy. And walielewana na kupendana sana sana sanaaa... Tatizo likaja kwenye dini - Demu mwislamu, jamaa ni christian, so automatically wazazi wakakataa hadi jamaa akubali kusilimishwa. The guy hakua tayari kwa hilo so mahusiano yakakatishwa!!!
Waliumia sana wote wawili, but wakasema Life Goes On. The lady is very very beautiful so baada ya muda si mrefu akapata another guy. I met the guy - alikua mwenye heshima, intelligent, funny, loving and caring. My friend aka fall in love and so did the guy (he's muslim). The guy aka propose after a year, rafiki yangu aka accept, ndoa ikafungwa. I wished them all the best in their marriage. Sijaongea na my friend deeply kwa miaka kama miwili. Yaani ni ile juu juu tu, mambo vipi.. She gave birth to a son, now ana miaka 2 na nusu.
Sasa juzi nikawa nachat naye.. Tukajuliana hali then nikamuuliza vipi shem wangu hajambo? Akanijibu "Hamna tena shem, tumeachana." Nilistuka! Nikamwambia - But you guys were soo happy and so in love, what went wrong?
Akaniambia - "Barbara 'usichokijua kweli ni sawa na usiku wa kiza. I rushed kwenye ile marriage. Ningekaa zaidi kwenye relationship ningemjua my ex husband vizuri."
Nikamwambia - Yote kwa yote mamiii.. Hujafikisha 30 umeshakua divorced, what have you planned for the future na mtoto je?
Akanijibu - " Hata usiende huko because I'm pregnant na my ex husband nasubiria mtoto wa 2, ila nimechoka sana so whatever goes poa tu. Ila siwezi kumrudia . Nitawalea wanangu mwenyewe."
I was very disappointed kwa sababu yule shem wangu siku ya kwanza kukutana naye I liked him na nikamwambia my friend huyu anakufaa because anakuelewa sana.. Kumbeeeeee
Sasa jana ndo nikaenda kuongea na my friend kwa undani zaidi.. Akasema
"Shem wako alianza kwanza having affairs, sio mara 1 wala 2. Kama hiyo haitoshi si unajua mi nina biashara zangu? Akaanza kuniibia hela na hata my jewellery. Kitu nakiweka nikirudi hakipo. Wakati mi na yeye tu ndo tuna funguo za chumbani kwetu. Kali kuliko zote ni nilipogundua kuwa anatumia drugs!!!!"

                          
Nilishusha pumzi. Anyway here's a lady hajafikisha hata miaka 30. Ana mtoto mwenye miaka 2 na nusu na ni mja mzito. From the same guy. Yeye swali lake ni - watu watamchukuliaje? Anaogopa atasemwa na watu kuwa since ametoka familia bora basi watu wataona yeye ndo alikua akimpelekesha jamaa na hata labda kum introduce kwa hizo drugs because alisoma nje.
At times like this ndo tunaonyesha upendo kwa marafiki zetu. Kama this friend of mine right now, she needs love, care and understanding.
Mawazo and advice yako itakua very appreciated.

Much love.
xoxo

Tuesday, February 21, 2012

Swali Kwako...

                                                       

Mambo...
Mara nyingi tukiongea katika Society kuhusu abuse - kinachokujia akilini hapo hapo ni abuse kwa wanawake from wanaume na abuse ya watoto from wazazi... But kuna abuse ambazo hazimulikwi kabisa- abuse to men.... Na kinachoumiza zaidi nikua apart from wanaume hawa kuwa baba, babu, uncle, cousin, kaka nk  sisi wanawake wanaotuamini na kutuheshimu ndo wa kwanza kuwacheka na kuwasema kuwa wanastahili etc.., They are silent victims. Manake research zinaonyesha kuwa almost asilimia 45 ya wanaume walioko kwenye ndoa wanakuia abused na wake zao... Wengi wakiwa hawana pa kushtakia, hawana wa kumueleza na hawawezi to fight back manake watajisababishia tatizo kubwa zaidi..
Anyway swali leo ni kwako.. Ni sababu zipi hasa hupelekea wanawake (mke, girlfriend, mistress) kum abuse mpenzi wake?                           

Ukiwa una tatizo ambalo unahitaji advice katika Tatua Thursday - feel free kutuma emal -
barbshassan@gmail.com au sms +255 759 008500

have a lovely day,
xoxo

Friday, February 17, 2012

Wangu Wa Makeri - Unamfahamu???

Hellow,
Leo my colleague Gerald Hando amenikumbushia mwanamke huyu Wangu Wa Makeri. He took me way back nlipokua shule and nilisoma kwenye vitabu vya history about this "superwoman" aliyekuwa anachukiwa na all men folk wa Kenya kwa jinsi alivyowadhalilisha na kuwatesa wanaume! Unamfahamu Wangu Wa Makeri?
               

                                        


Wangu wa Makeri alikua leader wa kwanza wa Kike katika kabila la Kikuyu nchini Kenya. Zama hizoooo wakati wa wakoloni.  According to the legend, wanawake wa Kikikuyu walikua wakiolewa - mume anakua anakumiliki, kwa hiyo however atavyojisikia kuku treat ndivyo atafanya. Na pia akiamua kuwa utapata kipigo kila siku - ndo hivyo itakavyokua.. Si kakutolea mahariiii? (SO SAD)
Kwa hiyo, Wangu Wa Makeri alipoteuliwa na wakoloni kua mkuu wa Wilaya, akatoa machungu yake yote kwa niaba ya wanawake wooooote wa Kikuyu.... Oooohhh don't mess with a woman scorned!!! You will taste her wrath!!!! Anyway, soooo baada tu ya kupata that cheo Wangu Wa Makeri akawaonjesha hell wanaume! To pay back kwa mateso walokua wanapata wanawake at that time...
Alizaliwa mwaka 1856 mma cheo cha ukuu wa wilaya alipata mwaka 1901. Ilikua haijawahi kutokea kabisa mwanamke kupata a high cheo like that. Wangu aliwaumbua sana wanaume. Inasemekana alikua anawapanda kama farasi, yaani mwanamume gets on all fours kisha Wangu anampandia juu, na huyo mwanamume anaanza kutambaa kama mtoto! Aliwatumia kama viti na pia sehemu ya kutuliza her legs.. Pia katika mapenzi alikua anamchagua yule amtakaye, na kumfanyia vile atakavyo. Ole wako usimridhishe! Cha moto utakiona!! Alikua akichukua hadi wanaume zaidi ya wawili and have sex with them kwa wakati mmoja.. Ulidhani vimeanza juzi hivi?? Mbona loong time mambo haya yapo?
Ila hii tabia yake made her achukiwe sana na wanaume manake alikua anapitiliza kuwatesa na kuwaaibisha men. And kumbuka alikaa madarakani for 35 years!!! Miaka yote hii akifanya atakavyo. Duuuuu.. Wanaume walikoma wakati huo! In the end, kilichosababisha kunyang'anywa cheo pamoja na kifo chake was mgongano kati ya Wakikuyu na wakoloni.
That is Wangu wa Makeri!!! Reputation yake ya kua na many lovers na hamu ya kukalia wanaume vichwani bado inatumiwa kama weapon till today katika vita ya gender, wakisema kua any woman who loves power and money katokea kwa ukoo wa Wangu wa Makeri!!!
 PS- kwa maoni, advice, maswali na mengineyo - wasiliana nami -
 barbshassan@gmail.com or sms - +255 759 008500
                                                
Wishing you a lovely weekend..
xoxo

Thursday, February 16, 2012

Tatua Thursday....

                                    
Mambo vipi Barbara?
Naitwa Alice. I'm in a fix!!! Nilikua ndani ya relationship na kijana niliyempenda sana sana.. Tulianza toka tukiwa form 3 and tulikuwa wote for approximately miaka 8. Ila miaka miwili ya mwisho alikua Ulaya ambapo alienda kumaliza masomo yake. Nilivumilia kuwepo kwenye long distance relationship. Kumbe huku mi nikawa najibana and kujitahidi kuwa faithful mwenzangu huko alikua anajiachia na wanawake tofauti tofauti ambapo baadaye nilikuja kuona picha kibao katika facebook yake. Nikaona why niendelee kupoteza muda nikimsubiria mtu ambaye ni dhahiri kuwa amesha move on. Manake mawasiliano yalikua hamna tena - wakati alikua akinipigia baada ya kila siku mbili. Anyway, nilimpigia kumwambia kuwa tu end mahusiano yetu ila akawa hapokei simu wala kujibu e mail wala sms. Ilinibidi kufanya maamuzi mwenyewe. Nikaamua  mi na yeye basi! Nikaingia kwenye mahusiano na mtu mwingine anayenipenda kwa dhati na ananijali kupindukia. Ninawa na furaha tele moyoni. Baada ya mwaka akanichumbia na kuleta mahari kwa wazazi wangu. Sasa hivi tumeoana na tunaishi kwa furaha sana na tayari tuna mtoto mmoja mchanga.
Kivumbi kilitifuka siku yule boyfriend wa zamani aliporudi nchini. Alinitafuta ofisini kwangu na hadi nyumbani kwa fujo za kila namna, akisema nimlipe kwa kumpotezea muda na kumuumiza kisaikolojia. Analeta mambo ya huko Ulaya. Sasa kati yangu mimi na yeye nani anatakiwa kumdai mwenziwe. Anyway amekua akinipigia simu hadi saa 6 za usiku, sms zisizoisha, leo ananidai kesho ananiambia baby come back!
Tunakoelekea huyu bwana atanisababishia niachwe na mume wangu. Ni kama anafanya kusudi kuniharibia ili nirudi kwake. Na mie sitaki na nimeshamwambia mara kibao. Uzuri ni kuwa nilishwambia mume wangu story zake kabla hata yeye kurudi. Now nachanganyikiwa. yeye alikua na chance na mimi na akaipoteza mwenyewe, now kwa nini anifuate fuate na kuniharibia? Anajua jinsi gani nilivyoumia na kulia kila siku? Atanilipa machozi niliyoyamwaga muda wote huu nilipokua nalia juu yake? Nimechoka! Kwa nini inakua ngumu mwanamume kukubali kuachwa? Naomba ushauri.. Nifanyeje?

Ps... Karibu umsaidie Alice kwa kutoa maoni yako. Na kama una tatizo ambalo ungependa litokee kwenye Tatua Thursday feel free kunitumia email - barbshassan@gmail.com au sms +255 759 008500

xoxo

Tuesday, February 14, 2012

Happy Valentines Day...

                       
                                  

Hallo...
Kwa wewe ambaye ushaulizwa na mpenzi wako "Will You Be My Valentine" ,

                  

 Kwa wewe ambao bado unaotea ni nini utapewa as a Valentine gift leo, Kwa wewe ambaye leo ni kama siku ya kawaida tu because your lover anakua romantic mwaka mzima, Kwa wewe ambaye leo hii unataka ujionyeshe upendo to yourself, your children, wazazi au marafiki, Kwa wewe ambaye hata huna habari kama leo ni Sikukuu ya Wapendanao - Im Wishing you A Happy Valentines Day and Im Wishing You All The Best Katika Maisha Yako Ya Mapenzi...   lots of hugs,
xoxo                                

Monday, February 13, 2012

A tribute to Whitney Houston - A tribute to my mama......

                                        


Mambo...
Kifo cha Whitney Houston kilinistua and it's basically because the late Susan Kilembika (my biological mother) alikua anampenda Whitney vibaya mnoooo.. Kwa hiyo it brought fresh memories of kifo cha mama... Ila nakumbuka sana mama alikua anaandika nyimbo za Whitney kwenye vitabu ( hii tabia ilianza looong time)... Na nyimbo za Whitney zilikua zinachezwa all the time in my mum's house.. Automatically nikakua nikiimba nyimbo za Whitney - tena bila kukosea the lyrics...
Kuna kipindi - when i turned 18 nilitaka kuwa msanii (in fact nili record wimbo mmoja_ usiulize uko wapi) - guess who inspired me - Whitney.... She has been a part of my life... Kiukweli hata wewe - wakati ulikua unapitia problems in your love life, au furaha isiyoelezeka - whose songs zilikua zinaring in your head kama sio wewe kuziimba aloud - in your car, in the bathroom.nk. Movie ya Bodyguard uliiangia how many times?


                                                    
Unakumbuka zamaaaniii watu walikua wanasema kuna beef between Whitney na Janet Jackson? Eti wanamng'ang'ania Bobby Brown? Then fans wa Whitney wakafurahi sana - eti Whitney ndo alishinda hivyo vita and thus getting married to Bobby Brown!! Heheheh.. It seems like jana tu all these things happened.
Anyway kwa jinsi my mum alivyokua anampenda Whitney I hope since hakuwahi kumuona Live hapa duniani - Kua ataweza kumuona na kupiga naye story in heaven. I pray for these two angels...

                                     
                                                      (My mama and I)

R.I.P Whitney Houston
R.I.P Susan Kilembika

P.S - I'll keep singing Whitney's songs - coz at the same time namkumbuka mama... My favourites - Greatest Love of All, How Will I know, All The Man That I Need, I Wanna Dance With Somebody, Where DO Broken Hearts Go, Didint We Almost HAve It All, Saving All My Love For You, I'm Your Baby Tonight, So Emotional and IIIIIIIIIIIIIIII Wiiiilll Alwaaaaaaayyyyyssss Looooveeee Yooouuuuuuuuuuuu.....
And one of her quotes that moved me to tears.. " I'm either my best friend or my worst enemy."

hugs...

Thursday, February 9, 2012

Tatua Thursday....

"Hello Barbara... Nimevutiwa sana na swala la wanaume kulalamika kuhusu zawadi tunazowapa wakati wa Valentine. Kwa kweli mie wa kwangu alikua anaishia kupata - key holder, pen, tai, vest na boxer. Ila yeye huniletea zawadi kubwa kubwa kama hereni za dhahabu, pete ya tanzanite, wakati mwingine hela, laptop nk. Naomba ushauri wa nini nimnunulie mume wangu wa miaka 10 chenye thamani ya penzi lake kwangu na uvumilivu wa kupokea ma boxer muda wote huu pasi kulalamika.
Irene"

                                                 

Mambo Irene na wengine woooteeeee...
Niliahidi kuwa na "Tatua Thursday" kwenye blog yetu. Leo tutamsaidia Irene na wengine wenye the same problem. Siku zinazidi kukatika while we are heading to Valentine's day.
- Wanaume are boys in their hearts. Wanapenda sana Toys - sio toys za kitoto.. namaanisha hizi gadgets!!!! So you can buy for your Man/boy friend, fiancee, hubby - Ipad 2, Wii, Digital camera, cuff links, a watch, A simple nice gold/silver chain au bracelet, Kama ni mpenzi wa michezo - mchukulie hata jezi ya timu anayoipenda uandike jina lake at the back, kama ni mpenzi wa golf - buy for him set nzima ya kucheza golf - this is a bit on the high end, Nguo - in his favourite colour, Perfume, Shoes, A phone - ambayo amekuwa akiitaka kwa muda, aquarium, Leather bag la ofisini, Business card holder, nk..


                                                       
But even if unaweza kumnunulia vyote hivi au kati ya hivi ma lovey dovey tusisahau!!! Siku ya Valentine's unaweza kumpikia his favourite food, chill some wine, vaa some sexy new lingerie ambayo hawajahi kuiona, do your hair, kucha, make up kiduchu...

Motto ya ladies wa Wanawake ni sisi for this Valentine's is - "Look Good Enough To Eat This Valentines"

*Kisha muntumie picha eeeeh nione how good you like plus picha za zawadiiii... tu share jamaniii...*


                                                        
All the best
and mapenzi tele...

Monday, February 6, 2012

Valentines Day!!!!!!!

                                


Hellllooooowwww....
Msini shoot bure.. Nilikua naumwa malaria jamaniii...   Nisameheni buree..
Anyway 7 days to Valentines.. Umejiandaaa andaaje kwa ajili ya siku ya wapendao? Ushamnunulia mpenzi wako zawadi? Au you are still thinking of what utamnunulia?
Juzi nilitumiwa hii message - Wanaume wananalamika kuwa - Wanawake wanataka wanunuliwe expensive gifts wakati wao wananunulia wanaume cheap stuff!!! Is this true? What is the most expensive lakini romantic gift you ever bought for your mume/boy friend/lover???
Message yenyewe hii hapa - Valentine's day is a problem day!!! Because sielewi how a set of people (mnajijua) would want to exchange boxers and singlets for perfumes, watches, jewellery, phones pamoja na hair (the topic of giving hair as a gift is for another day kwa sababu hukuzaliwa na upara! Scientifically a woman cant be bald, so why buy hair?) It is completely overwhelming!!!! Don't you know what equitable exchange is? Ni sawa kubadilishana boxers na a Galaxy Tab on Valentine's Day? Or exchange a singlet for a Bold 5? How can you give a belt and be expecting an iPad2? Ladies enough is enough!!! The boys are not smiling. Try and impress your men this year...
If you know you are buying singlets, boxers etc.. please expect a similar responce, that's fair enough; Let's raise the bar mwaka huu, and accept these words of truth and advice in the spirit of LOVE.
From the Comittee of Concerned Men (CCM)
Haya changamkeni wenye wapenzi!! Kimesanuka kwa wanaume!! Wamechoka kunyanyaswa!! Wao ndo watoe vitu vya bei ghali tu.. Hahhahahhaa...

                                                                                     
Hugs...
 

Sample text

Sample Text

Sample Text