Social Icons

Pages

Friday, December 30, 2011

New Year....

                                                 

Hello...
Ni mwisho wa Mwaka mwingine tena na ni muda wa kutathmini what you have done, what you have achieved kwa mwaka huu..  Na piiiiaaa kujipangia malengo mapya kwa mwaka unaokuja. One thing's for sure - kama unajiamini sanaaaa basi ni muhimu uji push na kujiweka malengo makubwa zaidi na kama sivyo jiwekee malengo "achievable"....
Usiweke malengo sawa na mwingine - hujui why huyo mwingine amejiwekea vile... Kwa mfano labda mwili wako metabolism rate yake iko slow sanaaa huwezi kujiwekea the same malengo ya kupungua mwili sawa na aliye na metabolism rate iliyo fasta..
Panga kila kitu kulingana na uwezo wako.. Then try as much as you can ku achieve yale yote unayoyapanga kabla ya mwaka kuisha... Inahitaji a lot of discipline.. but ukiamini utaweza...

Something  else ... Kuna mambo ambayo in one way or another yamekurudisha nyuma kwa mwaka huu.. Wakati tunaingia kwenye mwaka mpya - LET GO of vitu vyote hivi.. Inaweza ikawa marafiki, wapenzi, biashara, kazi nk... Try something else.. kwa mfano - umejaribu business imeshindikana na ukapata hasara in the process... Achana NAYO!!! Move on... Jaribu something else au weka hiyo hela ya capital katika bank - kwa kufungua Fixed deposit account.. Utapata faida.. Sio wote tumeumbwa na mkono mzuri wa biashara...

All in all nawashukuru woooooooteee na nawapenda sana and nawatakia heri na fanaka katika mwaka 2012..
God bless..
xoxo


                                                               

Wednesday, December 28, 2011

Ingekua ni wewe - Ungefanyaje?.....

Hi kwema?
Krismass ilikuwaje? Did u get time ku spend na family, marafiki nk? Au ulikua mwenyewe kwa sababu zisizoepukika? Whichever way - I hope you enjoyed one way or another...
Kuna jambo limemtokea a friend of mine and kwa ridhaa yake kaniambia niombe ushauri from you...

                                        

Huyu dada ntamuita Eugenia * Sio jina lake*

Eugenia ni mdada mwenye miaka 31 anatokea kwenye familia Middle Class. Ana Degree yake in Psychology and anafanya kazi nzuri tu. Anajua kujipenda na kujiweka poa. Ana heshima, ni mcheshi, very smart, intelligent, hard working, focused, God fearing nk... Amekua in a relationship na this guy kwa muda wa miaka 5. Kama kawaida wanagombana na kupatana kama any other couple... Jamaa hajawahi kumvalisha Eugenia pete ya uchumba but wazazi na ndugu wa both sides wanajua kuwa watoto wao are a couple. Juzi hapa wakawa na a very big fight - wakagombana hasa - after Eugenia kufuma some sms zilitoka kwa demu kwenye phone ya boy friend wake. But si ni kawaida kugombana na kupatana? Heee the guy ndani ya 2 weeks akaanza kutoka na demu mwingine after mwezi na nusu kamuoa!!! Eugenia amepitia a lot na huyu jamaaa.. Wakati hana kazi - she was there, matatizo ya kifamilia - she was there, Leo hii jamaa kaamua kuoa demu mwingine...

Eugenia is in shock hadi sasa hivi... Kazini hawezi kwenda, sehemu tofauti hataki kwenda.. Anakaa akilia tu.. Atakua anajiulia a lot of questions right now..
1. Where did she go wrong?
2. Mbona the guy hakutaka wakae na kutatua their problems?
3. Was this a rebound relationship (hiyo ndoa)?
4. Au jamaa alikua na nyumba ndogo long time?
5. Why jamaa amempotezea 5 years in a relationship?
Tumsaidie anahitaji ushauri wetu..

Hivi vitu hutokea if not to you directly labda kwa mtu unayemfahamu....

have a blessed day..
xoxo

email me - barbshassan@gmail.com
sms me - +255 759 008 500

Friday, December 23, 2011

Season Greetings...

Hellow wapendwa,
Nina uhakika utakua unajua fika kuhusu kinachoendelea Dsm... Hali ni tete but Mungu anasaidia. Sina mengi ya kusema ila - Tushukuru kwa Yote na tusikate tamaa plus tuendelee kuombeana...
Wakati wa msimu wa Krismasi ni wakati wa kutoa zaidi ya kupokea - kutokana na hali inayoendelea dar - wanawake na watoto wengi wakikosa malazi, chakula na hata nguo - ni muhimu kujitolea. Wakati wa kipindi hiki cha krismasi gawa ulicho nacho na wahitaji....
Tuendelee kuwaombea waliofikwa na janga hili la Mafuriko na kuwasaidia kadri tuwezavyo. Kumbuka leo kwako - kesho kwangu na Kutoa ni moyo....
Mimi nitatoa - wewe je?

Ps - Roho za marehemu wote waliopoteza maisha wakati huu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa Amani. Amina.

Nawatakia heri na nafaka katika msimu huu wa Chrismas and a Happy New Year 2012.Monday, December 19, 2011

Shukrani....

       

                                                      


Hello...
As a normal African woman - nimekuwa na malengo yangu that I wanted to achieve at a certain point katika maisha yangu. Mengine niliyapa kipaumbele, mengine nikasema ya go with the flow. I have been able to achieve mengi tu kati ya niliyojipangia.. Mengine ni more personal, mengine ni professional na mengine ni social.. Katika Social ndo kwanza nimeweza ku achieve hili la blog.

Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru wewe mdau wa blog hii kunipa support wakati naanza - a few months back - hadi sasa hivi. Tukienda pole pole kwa kufundishana na kukosoana all through. Asante kwa kuwa na uvumilivu with me - helping me learn more siku hadi siku... You made this possible.. Asante na Mungu aendelee kuwalinda na kuwaongoza...
Leo ni Birthday yangu... I thank God kwa kuwa nami all through - it was a loong rough road - but nikaamini kuwa there's a light at the end of the tunnel.. Mwanga nishauona na nashukuru sanaaa kwa yote... Asante Yesu, asante Mama Maria, Thank you God....

Asante wewe na wewe kwa kua nami kupitia this blog...
Ubarikiwe kwa sanaaaaa...
xoxo

Monday, December 12, 2011

Book 17th Dec Mapemaaaaa...


ICE - Jewels/Accessories + BLACK - Dress = MAGIC ( Ice Black Magic )
Saturday: 17th Dec 2011
From: 9pm Till DawniBM - Much MORE Billicanas Complex DAR   
Dress in BLACK - Pay 20,000...... Otherwise - Pay 30,000  

Book A Table Now...   
Contact Frank Gonga & Martin Jay P

on  www.gongamx.com  or Frank Gonga on Facebook...

                                

The Other Woman a.k.a Nyumba Ndogo a.k.a Mpango Wa Kando

Hellllooooooowwww,
Forgive me kwa nitachosema leo... But heeey ni kitu tunaona everyday na most likely hata sisi wenyewe humu ndani tushawahi kuwa na mahusiano, kutamani au kutembea na mume wa mtu - wakati tunajua kabisaaa he's already taken.
Kuna raha gani kuwa na someone who you know sio entirely yours., someone ambaye you can't be with muda na wakati unapomuhitaji, someone ambaye huwezi kujiachia naye kwa kwenda for movies, events nk.
 Let's start hiviii, Are you the other woman in someone's married life? Kwa nini uamue kua na affair na a married man in the first place? Utakua labda unawaza/kufikiria kua uko very much in love with him. Au utakua hujali kua he's already taken.

Why umekubali kua naye knowing darn well yuko married? Umeshawahi kuwaza kua wewe ndio muharibifu wa ndoa hiyo?

Atakua labda kakuambia kua wamekua na matatizo katika ndoa yao for years kabla hajakutana na wewe. So maybe nawee ndo unatumia hiyo kumvuta closer to you. Unaamini it's not your fault kua yupo in a relationship with you. Unawaza kua mke wake ndo mwenye tatizo as she doesnt know jinsi ya kumpenda and to cherish him. Labda kakwambia mke wake hana time naye coz she's too busy na kazi au watoto na hawako in love kama zamani.. Right? Labda hata ameshawahi kua soo emotional na wewe na kukulilia akikwambia shida za ndoa yake.

Labda kakupa a very long list ya matatizo yao and you believed him. Si ndio? Unajiuliza so what kama u are loving a married man? Inawahusu ni walimwengu eti eeeh?


Umewahi kuwafikiria watoto wake? Umewaza how many hearts you have broken?
 Umekubali kuwa mpango wa kando kwa muda gani? Na je yuko tayari kumuacha mke wake and marry you? Aki commit kwako - kwa mfano - una uhakika gani kua he wont cheat on you?
Huishiwi nguvu emotionally when you have to compete for attention and ku share a man? Hupati wivu wakati mwingine? Kua mkweli...
Haya ni baadhi ya maswali unayotakiwa kujiuliza right now kama wewe ni mpango wa kando wa a married man. Au if you are THINKING kua in a relationship na a married man...


ADVICE KWA MPANGO WA KANDO
Kama already umeingilia ndoa ya watu, hujachelewa, you can leave now. Ni maamuzi tu. Usmitishie nyau wala kutikisa kibiriti kwa kutoa ultimatum, ondoka tu! Sawa itakuuma kwa muda lakini you will heal. Tafuta vitu vya kufanya - jifunze new things ili kujiweka busy usimuwaze... Kuna thamani gani kua kwenye relationship with a guy who is cheating on his wife? Put yourself kwenye the wife's shoes, how does it feel?

Kama ndo kwanza kua na feelings na a married man, kimbiiiiaaaaaaa.. It's a bad idea!!! Ukikubali kuingia kwenye hiyo relationship na ukaacha iendelee it means feelings zitakua deeper and itakua ngumu wewe kuachana naye... And kama na yeye akikupenda, UNALO!!!
Kuna wanaume kibaaaoooooo!!!! Eg - Bachelors, divorced, and widowed. Watafute taratibuuuu and sehemu tofauti. Avoid being the other woman! Itaku cost...


                      


Song Of The day - Changing Faces - That Other Woman..

I can't be that other woman
I can't be that other woman

You only see me every Friday night at nine
Can't imagine what you told her this time
You never take me to a public place
Worried that somebody might notice your face
Rush to the liquor store and then a motel
Call up your friends to just cover you're trail
Not a word until the week goes by
You call me when you want some pie
Why am I crying every night over you
You're never gonna leave her
Finally I woke up and smell the coffee
I understand
Why two women can't share one man

I can't be that other woman
I can't love you down
Can't keep creepin' around
Can't be that other woman
Yes I want you bad
But she needs you much more

I can't be that other woman
I can't love you down
Can't keep creepin' around
Can't be that other woman
Yes I want you bad
But she needs you much more


You never see me on the holidays
You disappear and won't return my page
You take my body in the middle of night
I ain't gon lie cause boy you do it so right
And then you melt with them same three words
Sweetest seduction that I've ever heard
And in the morning with the sun rise
You run to her I realize
Why am I crying every night over you
You're never gonna leave her
Finally I woke up and smell the coffee
I understand
Why two women can't share one man

I can't be that other woman
I can't love you down
Can't keep creepin' around
Can't be that other woman
Yes I want you bad
But she needs you much more
I can't be that other woman (See)
I can't love you down (What goes around comes around)
Can't keep creepin' around
Can't be that other woman
Yes I want you bad (I want you oh so bad)
But she needs you much more (yeah, yeah, yeah, yeah, yeah)

Can I get a witness
(Yes you can)
Can I get a witness
(oh yeah, yeah, yeah, yeah)
Can I get a witness
(You know you can)
Have you ever been in love with another girl's man
Can I get a witness
(Yes you can)
Can I get a witness
(oh yeah, yeah, yeah, yeah)
You said you're leaving a thousand times
But I won't believe til the papers are signed

Can't be that other woman
I won't believe it no
I gotta be the only one
Yes I want you bad
But she needs you much more
I can't be that other woman
I can't love you down
Can't keep creepin' around (No more late night booty calls)
Can't be that other woman
Yes I want you bad
But she needs you much more
In the morning with sunrise
You will run to her
You are never gonna leave her
So I'm saying good bye...
(Fade in chorus)
Unaweza ichek kwa youtube pia...


Good day my people,
xoxo

Monday, December 5, 2011

What do Men Want? Part 2...

Mambo..
Wikend ilikuwaje? kwema? Fresh basi...
Nipo kwenye a new relationship - ndo inaanza anza - so nisaidieni kuomba so that all can go well.. Tehetehetehe...
Anyway - nataka ni share with you vitu ambavyo attract men mara wanapokuona the 1st time..
Hii ni according to Dr. Paul Dobransky amabye ni psychologist na relationship expert pia aliyeandika kitabu kinachoitwa - The Secret Psychology of How We Fall in Love, “Katika dakika 5 za kwanza za kukutana na mtu. kinacho attract wanaume zaidi ni physical beauty. Kwa men hii ndo step ya kwanza ya courtship kwao."
Anaelezea zaidi kuwa , haimaanishi kuwa wanaume wooote wanataka vimodo virembo. Instead, anaelezea jinsi gani kila mwanamume ana taste yake kwa wanawake, physically. Mwisho wa siku ni kuwa - zile dakika za kwanza ni crucial sana.  “It’s not about personality, intellect, career or any other crucial things that make up a relationship."

Hizi hapa traits 8 ambazo men wamekubali kuwa ndo wanachoona kwanza and vina maana gani kwao:

                            

1. Kwanza kabisa, Men Admire
Wajuzi wa mambo wanasemaaaa -  Behind every great woman, is a man checking out her ass.. Ni tofauti na popular belief kuwa wanawake ndo wanaangalia zaidi ya men. Wanaume wanaangalia without ku stare au kuonekana wazi anamuangalia mwanamke. Med admire : wanawake inspect.. Mwanamke anaweza kuamua anamtaka a mana kabla ya the man kumuona yeye au kabla ya kupata attention yake. Wanaume wana notice curves na contours wakati wanawake wananotice form na structure. So even though both wanawake na wanaume wanaangalia the opposite sex, wanaume wanafanya hivi kimya kimya.  


                                                  

2. Confidence
Eye contact - Kumuangalia mtu machoni inaonyesha confidence ya hali ya juu kwa mwanamke. The way unavyojibeba na pozi zako can also tell a guy kuwa - "Here Iam and I feel great"  au pozi lako linaweza sema " Oohh please usiniangalie.. Ngoja nijifiche." 
A woman akiingia sehemu, with her head held high na bonge la smile usoni, wanaume watakua attracted kwake. Usiangalie chini na kuogopa kumuangalia mwanaume in his eyes. Kumbuka ukimuangalia mtu staright in his eyes, wanaume wengi will wake make a move na kukufuata coz anaona kabisa kuna hope ya kuwa na connection na wewe. 

                   

              

3. Your Smile
A smile inaeleza mambo kuhusu a woman. Personally my man is crazy about my smile! (hahahhahahah)  But je smile yako ikoje? Ni sweet na ya ukweli au inaonekana kama umefosiwa kusmile? Pia wanaume wengine wanapenda smile flani na facial expressions. Kwa mfano - Mwanamke akiwa anacheka sanaaa na anaonekana yeye ndo mchekeshaji katika group ya marafiki alokaa nao, kuna wanaume ambao watakuwa attracted kwake. Ila kuna other men ambao wanapenda the sweet and innocent smile

                        

4. Washkaji
Believe it or not, men wanahofia sana ukiwa na bongee la group la washkaji. Ukiongea na marafiki kama 20 hivi, most men hawatothubutu to come up to you kujaribu kukutongoza. Kila mmoja anaogopa kukataliwa ujue... Tembea na washlaji wawili tu wanatosha! So munakua watatu. Washikaji zako wawili watapiga story wakati wee unakwenda kupiga story with the new guy....                                 

5. Your Hair
Wanaume hawajui spilt ends, growth wala treatment.. But hua wanaangalia kama your hair zinaonekana soft na kama zinanukia vizuri. Hair style nzuri inaonyesha kuwa the woman ni msafi, responsible na anachukua muda to take care of herself. Fact - 44% ya wanaume - baada ya research - walisema cha kwanza wanacho notice kwa mwanamke ni nywele, 26% more than her clothes, 25% miguu, 4% - make up. And wanaume wengi wakasema kuwa they would rather approach a woman aliye na nywele nzuriiii badala ya mwanamke aliyevaa low cut shirt... Umeona eeehhh???


                    

6. Your Makeup
Unajua Clown? Yule anayefurahisha watoto? Lakini hua anajipakapaka vitu kibao huko usoni.. Yaah.. Usifanye hivyooo.. Usipake make up hivyo.. Hata kama unataka ku attract m tu.. duuuu!! Not that much... Ushawahi kum hug a man kisha unapomuachia unaona aibu? Coz umeacha - eye shadow, mascara, lipstic na foundation kwenye shirt lake? Most men prefer wanawake wanaopaka make up kiduchu tu. Jaribu to keep uso wako as natural as possible, ukiongezea kidogo kwenye favourite features zako ( km - macho au lips), na uonyeshe dunia kuwa you are proud of who you are na mwili ulopewa.

                                  

7. Your Cleavage and Madusko (aka makalio)
Newsflash, cleavage and madusko ndo vitu vya kwanza ambavyo men wana notice kwa mwanamke. sasa hii haimanishi kuwa uache shati loteee wazi hadi kwenye kitovu ( hahahah) Noooo!! Cha muhimu na kuzingatia hapa ni kuwa - Usionyeshe kila kitu kwa sanaaaa na pia usivizibe kwa sanaaaaa... A man like mwanamke wake awe alluring na sezy bila kuoneka cheap na vulgar! Na kumbuka men wanaopenda wanawake ambao wanavaa na kuonekana vulgar na flashy hua sio wa kua kwenye a relationship.
 
                                    

8. Your Bag
No, wanaume hawajali kama umebeba Gucci bag original au fake, ila watakuangalia unavyolibeba!!!! Wanawake wanaobeba mapochi yao kwa majivuno wanaonekana kama wako materialistic. Wanaume wengi hawataki mwanamke High- maintenance so wataangalia size ya pochi  yako kama ni kubwa zaidi ya gym bag yake na wanachukulia hilo kama sign ya value of material things. Sio all men wata notice your pochi, ila kwa wale watao notice watakusaidia kutathimini kama a guy anayejali pochi yako is really the one for you. 

Una cha kuongezea? Please feel free to do so...
sms - +255 759 008500

Monday, November 28, 2011

Why did I Sleep With Him.....

           
               

                              

Hellow,
Hivi ishawahi kutokea - due to different reasons - Ukajikuta you have slept with someone na asubuhi yake uka regret au ukaendelea ku regret for the rest of your life? Labda una regret coz you just met him and you thought kama hungeanza by having sex labda angekuheshimu na mungekua na the perfect relationship, au labda ni colleague wako kazini - unajiuliza how will you face him nk, Maybe hukutumia condiom, labda ni mtu unayemfahamu kwa muda but nyie ni friends tu and you wanted to keep it that way, Labda kakuambukiza an STD nk...
Ni matukio gani labda yalipelekea wewe to sleep na huyo mtu and maybe kwa nini uka regret? kama kawaida yangu nimefanya kaji research kadogooo kuhusiana na hili.. Nilipata the following majibu...

Ulevi - Kuna msemo "Beauty is in the eye of the Beer holder" Ukishalewa unaona jamaa yupo more handsome au ana vitu/ qualities unazopenda. Aaahh mbona anakubeba tu hivi hivi...  Morning after sasa.. You kick yourself kisawasawa anakua vile vyote ulivyoona havipo!
Revenge – Wanawake na wanaume wengi wakifumania au kujua kuwa theri loved ones wame cheat on them wanalipa kisasi. How? Wata have sex na the next person atayewatongoza. Unabisha?

Huzuni –  Kuna watu hawajui jinsi ya ku take care of traumatic experiences eg -  kaachwa mataani siku ya wedding yake, kafiwa na someone very close etc anakua soo vulnerable na hii inapelekea mtu huyu to sleep with anyone atakayemtongoza.

Isolation – Unapokua kwenye maeneo mapya ambapo you dont know anyone au unajua very few people unakwenda tafuta comfort in the arms of a stranger. Actually yeyote who will smile at you!

Lovelessness – Amini usiamini, wanawake na wanaume ambao wanahisi hawapendwi tena na labda walikua either wako in a long term relationship au wanaishi na wapendwa wao wakliachika wanataka kua appreciated again. Wata have sex na anyone - tena easily...

Boring sex – Eeeehhhh.... Ukiambiwa ujitume unaona tunakutania... Hehehhehe..  Studies reveal kuwa wanaume na wanawake ambao wananyimwa sex au the sex is boring katika relationship yao wata have sex na anything - sio anyone tu!!

Blackmail – Kuna ma Conmen na perverts wa hatari around. Hawa watafanya kila njia na namna to have sex with you. Labda ni ex wako and ana picha yako ya utupu mliopiga when mlikua pamoja and maybe umesha move on na una mtu mwingine - akaja kutana na wewe u look more beautiful and sexy - weee ataku threaten hadi ukome.. Baby come back kwanza, ikishindikana anaku black mail kua atatupia hizo pics zako ndani ya faebook kisha aku tag. Utafanyaje?

Frustration –  Kuna watu wana frustrations za ajabu katika relationships zao.. Yaani inakuwa mateso kweli so mtu anaamua liwalo na liwe.. Kuonyesha kuwa She/He is done with you - anaweza kumchukua mtu yeyote and sleep with them and ata make sure you will find out...

Peer pressure – Unapojikuta kuwa everyone is doing it, so unajiuliza kwa nini na wewe usijaribu?

Kama ulishawahi regretting to have sex na someone share nasi story yako...


            
PS. Unaweza nitumia email - babo25@gmail.com au sms - +255 759 008 500 

Have a good one.
xoxo                

Shukrani...

Hellooo,
Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru wewe na yule muliotenga muda wenu na kuja Nyumbani Lounge this saturday na kushiriki kikamilifu kwenye Grooveback Divas Night. Thank u thank u thank u.... Nimeshuhudia upendo mkubwa kutoka kwenu. Kwa wewe ulioshindwa kuja usjali - Hii itakua every jumamosi ya end month pale pale Nyumbani Lounge.. Karibu

Shukrani za dhati kwa waliowezesha Diva's NIght ifane zaidi - Our Sponsors -  Baileys, Micro Max Mobile, Navo's Choice, Oriflame, http://www.gongamx.com/ , http://www.8020fashions.blogspot.com/ , Nyumbani Lounge pamoja na Grooveback.

Bila kusahau - namshukuru sana Mwenyezi Mungu..

Asanteni sana na Mungu awabariki.. Picha zitafuata...

bless,
xoxo

Friday, November 25, 2011

Are You Ready For Diva's Night?

                        

D.I.V.A - Demu Intelligent very Ambitious

This saturday mambo yamekuwa mambo. If you think you can dance yaani Best Dancing Diva - Unaweza jishindia *  GrooveBack Night membership card + Micromax Phone + A Bottle of Baileys + Products from Oriflame

Kwa atayependeza kushinda woooote yaani -    *Best Dressed Diva -atashinda - Shopping Voucher from Navo’s Choice + MicroMax Phone + A Bottle of Baileys + Products from Oriflame

Kuna zawadi nyingine kibao - How utazishinda? Fika Nyumbani Lounge from saa 3 usiku hadi saa 6 usiku na utaingizwa kwenye Droo. And unaweza shinda the following:

-  Massage and pedicure/manicure voucher – Teddzzz Salon

- Gift Hamper – Jackz Cosmetics

- Baileys Bottles

- Round of Drinks from Nyumbani Lounge
- Products from Oriflame
- Shopping Voucher from Chocolate Princess
Dress to impress - si unajua tunavyosemaga... If You Got It Flaunt It!!! Manake kutakua na Red Carpet. Pamoja na yooooote kutakua na a Beautician kutoka Oriflame atatufanyia skin test na make up for free kwa watakaopenda....
Show off the DIVA in you this saturday...

PS. Dont Forget your Business Card....                          
A peek at Micro Max phones...


Remember - Kiingilio ni Shiling elf 10 tu....
C you at Grooveback Diva's Night..

Diva kisses your way...
xxxx

Thursday, November 24, 2011

Diva's Night....

  Heeeeyyy,
Kwema, Mzima?

Soooooo u think u can dance? Na je wewe unadhani unaweza kua best dressed Diva? Karibu Grooveback Diva's Night j'mosi hii @ Nyumbani Lounge. Unaweza shopping voucher ya Navo's Choice, Vipodozi from Jackz Cosmetics, Products from Oriflame, Shopping voucher kutoka Chocolate Princess na Phones from Micro Max!!! Flaunt your Divaness! C yah!!! :)          


                                                              
                                Shukrani kwa Sponsors wetu

- Grooveback
- Navo's Choice
- Gongamx.com
- Nyumbani Lounge
- Chocolate Princess
- Oriflame
- Jackz Cosmetics
- 8020 Fashions
- http://www.wanawakenisisi.blogspot.com/

Ukiona tangazo hili mfahamishe na mwenzio.. Tukutane Jumamosi hii...
xoxo

Wednesday, November 23, 2011

It's a Celebration of Women and Music!!!

                                   

Ladiiiiieeeesss ni muda wa kuringa na kujidai na kufurahia kuwa mwanamke! This saturday kutakua na Grooveback Diva's Night pale Nyumbani Lounge! Let your hair down na dress to impress. Kutakua na Red Carpet, Music kutoka kwa Divas kama Lady JD, Mariah Carey, Shola Ama, Mary J Blige, Chaka Khan, Unique Sisters.. nk Kwa kiingilio cha Shilingi Elf 10 tu za Kitanzania. Na piiiiaaa  kutakua na zawadi kibao - Shopping Voucher kutoka duka la Navo's Choice, Shopping Voucher kutoka Jackz Cosmetics, Simu aina ya Micromax na mengine mengiiii... Usiachwe nyuma. Karibu so we can celebrate being Ladies...
Kumbuka D.I.V.A ni - Demu Intelligent Very Ambitious!!! Karibuuuu..

Kwa maelezo zaidi sms me - 0759 008500 au email barbshassan@gmail.com

Grooveback Diva's Night is sponsored by Grooveback Night, Navo's Choice, Jackz Cosmetics, Nyumbani Lounge pamoja na http://www.wanawakenisisi.blogspot.com/ 

Have a good day....
xoxo

Tuesday, November 22, 2011

The Uninvited Guest....

Hey,
Nisameheni kwa kua kimya sanaaaa.... There's something tunaandaa kwa ajili  ya ladies - Diva's Night na Grooveback - Itakua this saturday pale Nyumbani Lounge. Ntawajuza zaidi as days go by - make a date basi tujumuike pamoja.

                                                   

That said - kuna haka katabia ambacho nimegundua wanawake ndo tulikua nacho zaidi before but siku hizi it's being done by both men and ladies. Utakuta mtu kaalikwa sehemu maybe for dinner, lunch, party au hata wedding. It could be something big or not. Lakini unakuta wewe uliyealikwa unabeba mtu mmoja au zaidi ya wawili kwenda nao ulikoalikwa and without notifying yule aliyekualika! Maybe huyo aliyekualika alikua kajiandaa kulipia drinks na chakula kwa a specific amount of people. Wee umejibebesha huko washkaji zako ukaenda nao! Yule aliyekualika hatoweza kukwambia chochote because of ukarimu wetu watanzania. But hebu fikiria damage utayosababisha kwenye mfuko wa huyo mtu. Hata kama that person ni tajiri lakini ana budget yake! Hivi unahisi utaalikwa tena na the same person siku nyingine kweli? Na hiki kitabia kimetokea wapi? Wee una tabia hii? Ukifanyiwa wewe how will you feel?
For example wengine wanapewa na invitation card kabisa na imeandikwa jina lako tu - unambeba mkeo au mumeo/ boyfriend au girlfriend au sometimes some friends tu wa kawaida? Huoni aibu?
Tujifunze bwanaa... Kama umealikwa mwenyewe nenda mwenyewe, kama unataka kumbeba mtu basi uliza kwanza, sio kukurupuka tu.. Na wewe mtu akitaka kukubeba juu juu eti kaalikwa sehemu kataaaa!!! Hakikisha you have been invited too...
Anyway - I hope nimeeleweka....

P.S -  It is against the rules of etiquette for a guest to show up at either an invitation-only event or your home uninvited. It is also against the rules of etiquette for you to show up at someone else's home or an invitation-only event uninvited or with an uninvited guest.
 
 
 hugs n kisses...                                      

Wednesday, November 16, 2011

Limbwata....

                 
                                    
                           Huyu ndo Shanita mwenyewe akiwa na moja kati ya magari yake ya kifahari..

Hi,
Katika gazeti la leo la Uhuru ukurusa wa 2 kuna habari kuhusu msichana wa miaka 25 Shanita Nalukenge (Mganda) na a married businessman David Greenhalgh (England) ambapo inasemekana kuwa David amemfikisha Shanita mahakamani after Shanita kumtapeli David 7.8 Billion Tsh. Na wanasema jamaa alipewa limbwata na the lady ndo maana akawa hafurukuti na kummwagia Shanita mihela kisawasawa zikiwemo Pound 400,000 aliyompa siku ya birthday yake! David kamind sanaaaaa ila anasema hamind kuwa Shanita aliiba hela yake na kuitumia vibaya bali kuwa she was spending his money na vijana wadogo ambayo walikua wanamtukana! Mbona kama jamaaa ana wivu tuu.. Hehehhehe! Anyway for more of that story cheki humu
http://allafrica.com/stories/201111090765.html  

                                                      David huyu hapa...

Baada ya kusoma this story nikawa najiuliza Kuna ukweli gani kuhusu limbwata? Kuna mtu akanambia " weee unaona jinsi wanaume wa Kihaya walivyo wakorofi na wagumu lakini kwa wake zao kimya! Unajua sababu?" Mie kimya!!! Eti ni kweli?
Naambiwa kuna aina nyingi za limbwata - kuna Kaligoligo ambayo eti hii inavuka hadi bahari!! Hahhaahha! Mutaniua kwa kucheka!
Tuanze kwa kujiuliza - Limbwata ni nini? Limbwata ni dawa ya kumfanya mtu akupende zaidi - unakuwa husikii wala huelewi... 

Kati ya Limbwata zilizopo, I heard kali zinatokea Bukoba. Eti kuna - Shuntama (Maana kwa Kiswahili - Inama) Kila utakachoambiwa utafanya! Eg -  Mwanamke: Nifulie chupi zangu - Mume: Haya mpenzi. Mwanamke: Nipikie chapati - Mume: Haya La azizi ( Mume anapinda mugongo!! Hahahahahahahah!!! I'm sorry but this is too funny!! Khaa!! Hivi ya kweli haya? Haya naambiwa pia kuna  -  Genda Ogaruke (Yaani Nenda Urudi) - yaani utakwenda kisha ukifika huko utamkumbuka demu na utarudia.
Jinsi ya kutengeneza Genda Ogaruke siijui - Labda utufahimishe if you know.. But nimegusiwa jinsi ya kutengeneza Shuntama - Eti unachukua a piece of meat kisha unaweka in your private parts for 3 days - unaitoa wakati kwa kuoga au kujisaida kisha unairudishia. After 3 days unaitoa unaichanganya na nyama fresh na kuikaanga - kisha unampa bwana anakula. Baada ya hapo!!! Hahahahahahah!!!! Atafanya kila utakalona kukupa kila utakacho!!! Hahahahahahahaha! Jamani sorry nacheka sana leo... Nimefurahi tu...

Tanga - Limbwata - Unakwenda kwa mganga unamwambia shida yako... Anataengeneza some powder from Love herbs kisha unakuagiza upeleke some stuff zako au za huyo unayetaka akupende  eg - kucha za toes and fingers, pubic hair au nywele za kawaida. Kisha anazifanyia Love spell akitaja jina la huyo umtakaye akupende. Unamuekea kwenye chakula then anatakiwa akupende na kukujali kupitiliza after that..

Hivi kweli Limbwata exists au hao wanaotengeneza they play with our psychology?
Niliona this article from - http://www.http//worldhotstars.blogspot.com  nikaipenda sanaaaa...LIMBWATA FACTSA) If LIMBWATA is to allow your wife to be a partner and participant informulating the family budget, then I support it, becoz women are wiser spenders than men.

B) If LIMBWATA means that the family money is used by Mama Watoto topurchase stuff at Kariakoo rather than being drunk by the husband atRIVERSIDE or GAZA ONE then I support that men are affected by LIMBWATAz

C) If a LIMBWATAz husband is the one who won't spend ALL the monthly salary with NYUMBA NDOGO or at KITIMOTO Bar (while his KIDS starve) then HONGERA to all LIMBWATAz husbands.

E) If LIMBWATA means that a MUME spends quality time with his MKE and WATOTO, instead of engaging in dubious investments where he is CONNED then; "Watu Walishwe LIMBWATA forever".

F) If LIMBWATA means that when MKEO is SICK you help her with work,that when she is over burdened you extend a helping hand then LONG LIVE LIMBWATAz

G) If LIMBWATA means that you DON'T BEAT UP your wife, that you seekassistance from your wife for they are called helpers when you have tried all the altanertives in vain, then LIMBWATAz LIDUMU MAISHA .

H) If LIMBWATA means that you treat your wife as a human being, that you are polite, don't bark at her like a dog, DONT growl at her like a hyena, consider that after work she is as stressed as you are then VIVA LIMBWATAz.

I) If LIMBWATA means that you are at home after work, and that your wife and kids are your next of KIN then HONGERA WALE WOTE WALIOLISHWA LIMBWATA.Na ukae hivyo hivyo kaka! KAMA UMELISHWA LIMBWATA, WEWE NI BINGWA!!
Tell you WIFE to add More LIMBWATA
                      
                                        
                                         
                                                                                     

Hugs and kisses,
mwaaaah

Tuesday, November 15, 2011

Kiafrika Zaidi - Traditional Nguo Za Different African Countries.... Part 1

Hey,
There's nothing kizuri kama kuenzi Uafrika wetu. Na pamoja na kukuza na kuendeleza cultures na tabia zetu za Kiafrika, Kuna mambo ya msingi ambayo tunachukulia poa. Mavazi ya Kiafrika ni mojawapo. Acha pembeni food (another topic for another day). Coz kwa mavazi tu someone anaweza ku conclude what kind of person you are. Ukiwa umevaa nguo za Kiafrika kama mwafrika - immediately mtu anajua wewe uko very proud of being an African.
Nilichofanya nimetafuta National dresses za different African countries ili at least me na wewe tushoneshe na kuringa nazo. MAnake ubunifu wetu umeishia kuiga tu za Kinigeria zaidi wakati kuna Mataifa kibao Africa! Hehhehe...
Ps.. Ukizingatia kua kuna nchi kibao ndani ya bara la Africa - we can't finish all these countries kwa siku moja. So huu utakua mfululizo... Twende taratibuuuuu...

  1. Algeria

                                                     For Ladies.....

                                                     Kwa wakaka...

Pia nimeona wadada wanavaaa a loooooot of jewellery ......
2. Angola
Ladiiiiiiieeessss - nawatonya... Etiiiiii huko Angola population yao ni 56% wanaume na 44% wanawake.. Haya kama unatafuta mume wa peke yako nenda huko - just don't forget to  learn Portugues! Hahahahahah!
Nimepata this pic kutoka kwa Bella Naija ambapo Nelsa Alves Miss Angola 2009 alivaa katika mashindano ya Miss World kama National costume

                                                         
 

3. Benin
Benin ni nchi iliyoko West Africa. Ni nchi maskini, mara nyingi utakuta watu wa huko wakivaa rags. But wenyewe wanasema unaweza wewe kama mgeni kununua Beninese fabric ukapeleka kwa fundi ushonewe nguo zao - Bubus na Bombas. Hazina tofauti sanaaa na nguo za Nigeria... 

4. Botswana
Nikiskia Botswana nawakumbuka Makhirikhiri!!!!!

Tafuta ngozi.. Sjui ni ya ngombe au mbuzi au swala.. Humo humo tu.. Hehehhe Kwa kweli You will never find me wearing that, Hata nikipewa bure! Mweee!!!

5. Burkina Faso
One of nchi maskini zaidi Duniani...
                                         
Ilikua ngumu sana kutafuta Natioonal costume ya Burkina - Ila kwa vile ni West Africa - most countrieas za kule wanavaa nguo za kufanana kama Nigeria ( nimetaja Nigeria coz wengi wetu tunafahamu nguo zao and tunazimiliki) Anyway cha kusikitisha ni kua wanawake wa Burkina Faso wanapitia a lot of social, economic pamoja na political discrimination. Kwa mfano - Hawapati urithi sawa wala haki za Kisheria sawa na wanaume. Rates za wanawake wasojua kusoma na kuandika ni mara mbili zaidi ya men na a very large percentage ya wanawake wana maambukizi ya HIV/AIDS...

Tuwaombeee....
Be blessed.


Maoni yako... tuma kwa barbshassan@gmail.com
or sms - +255 795 008500                              
                                                                                                                 

Monday, November 14, 2011

Single Ladies...

Hi,
How was wikendi? Mi nilikua home tu manake mtoto aliumwa (Malaria) Anyway she's better now. Shukrani kwa wote muliompa pole my girl. Senkyuuuuu..
Basi katika ka weekend kangu nilipojifungia ndani tu - with mtoto kuumwa plus bonge la mvua in Dar, nikaletewa hii Series ya Single Ladies na Loveness Love (thank you mami) Mbona nimenogewaaaa..


                                                
Kwenye this series yupo  Stacey Dash ( alim divorce mumewe in real life juzi juzi - kumbe jamaa alikua anamdunda sana huyu demu) Ana act kama Valerie "Val" Stokes - Yeye ni an aspiring fashion mogul akanunua a fashion boutique ambapo pia ana design some clothes mwenyewe. Anajaribu sana kupata the right guy. Na urembo wote na success aliyo nayo inakua sooo hard kumpata anayemtaka yeye!Alikua in a long term relationship na akaamua kumpa the boy friend an alternative akwamwambia "Either put a ring on it au sepa" Jamaa akasepa!! Duuuuuuu!!!!

                                                         Huyu ana miaka 45!!! Udongo mzuri?


Pia yupo LisaRaye Mc Coy ana act kama Keisha Greene (I love her confidence na the way anavyochukulia maisha in general)  - Hapa ana act kama A former hip-hop music video model akaja kuwa a semi-professional poker player ambaye ana rely on her head badala ya moyo kwenye mambo ya relationships.

                                                            
 Huyu ana miaka 44! Daaa!! Mazoezi na diets za kutosha!


Kisha kuna Charity Shea ana act kama April Goldberg-Jenkins  - April hapa kaolewa na a black american kwa miaka saba. Yeye ni assitant kwenye a Record label. Alikua na a relationship ya nje na Mayor wa mji wao ( ambaye ni that rapper Common) kisha news ika leak! Mumewe akajua! Shughuli. Siku ya bday ya April mumewe akamletea divorce papers as a present! So much for a gift! Mi ningekufa!!!

                                                                  


Hii series evolves around hawa wadada watatu katika maisha yao - professionaly, kimapenzi na maisha kwa ujumla. Kulia wanapoumizwa kisha wanasimama na kuendelea na maisha. At the same time they are go-getters wanajituma kutafuta money. So wanaku inspire pia huku wakipitia the normal stresses za relationships - wakati wakiwa kwenye relationships.
Kuna one gay guy kwenye hii series yeye anauza duka la Val. Ananifurahisha sana yule kaka - he tries sana kuwapa advice za relationships hawa wadada. Kwa mfano kuna siku Keisha alikua approached na mbaba mmoja tajiriiii - he had it all. The looks, money and a gentleman - hadi alipojitolea kumpa Keisha dola elf 10 to sleep with her. Keisha akakataa. Alipoenda kuwapa story mashosti zake the gay guy akamuuliza Keisha why hakuchukua hiyo hela. Keisha akajibu - Khaa I'm not that cheap. Mi siwezi kununuliwa. The gay guy akasema - "Why is it kua if a man akikupa hela up front inakua prostitution but if he wines and dines you katika mitoko mitano tofauti na aka spend hela ile ile unamuita prince charming/sent from heaven!"
Think about hiyo statement... Kuna ukweli ndani yake? If there's umejifunza nini hapo? Umetafakari vya kutosha? Utajiweka wapi? We learn something new kila siku.. ..

Your comments ni muhimu sana...
Write to me barbshassan@gmail.com
or sms 0759 008500

Have a lovely day
xoxo

Thursday, November 10, 2011

Relationships (part 3)

Hello,
Nakua mkweli leo. I have never lived na mwanamume maishani mwangu, sipendi kitchen party at all! But all in all mamangu (Magdalena Mkunde) amenifundisha mengi kuhusu maisha na jinsi ya kujitegemea - whether naishi na mwanamume or not. Why nimeanza like this unajiuliza?
Well - Hua wanasema "The way to a man's heart is through his stomach" Hawakukosea. Kwani nani hapendi msosi? Na dont ask me kama - naishi nile au nakula ili  niishi (this is debatable)....
Imajin this - Mumeo/ stay in boyfriend wako kaenda ofisini siku nzima anarudi home humuangalii hata mara mbili - kisha to top it up unampikia wali na mchuzi wa mayai!! Mchuzi wa mayai unaujua? Im not talking about egg soup ile ya chinese! Nooo!! Mchuzi wa mayai!! Yaani unachemsha mayai pembeni. Kisha unakaanga mchuzi pembeni (ambao uko maji maji meupe kama mchuzi wa jela) kisha unamenya yale mayai ulochemsha unakata slices na kudumbukiza kwenye mchuzi!! Na hii unampikia 3 times a week!!! Hiviii huyu mwanamume akitafuta nyumba ndogo yenye kumliwaza na kumpikia mapochopocho utalalamika? Au ndo diet? Heheheheheh! Seriously!!!

                                    Bleeee (kama naniliu eeh)

Pamoja na hilo hujui kupika unaamua kupika ndizi matoke - unadumbukiza ndizi nzima nzima kwenye sufuria, unakatia onions na nyanya humo humo na nyama kidogo kisha unajaza maji hadi juu!! Vitunguu vyeupeee!! Huyo bwana si ataenda kula chips vumbi jamani!! Unamkosa hivi hivi ukiona na kumsogeza mbali nawe.
Plus unathubutu kumpa your house help vinasa (underwear) za mumeo afue yeye!! Hivi kweli??? Hivi ukiibiwa utamlaumu nani? Utaimba Mulika Mwizi hadi uchoke!!!
And these things sio lazima ukafundwe kuvijua ni logic tu!
Hebu imajin mume akirudi home unamhug and welcome him home, unamtayarishia maji ya kuoga (sio lazma umtilie asmini), muwekee his pajamas tayari. Then mkaribishe mezani ambapo unapika at least vitu vinne tofauti mf - wali, chapati, mchuzi wa kuku/samaki, na mboga za majani, salad and fresh juice. Kaa ule naye huku mkipiga story. Asking him siku yake ilikuwaje and stuff. Au nakosea? Mi ni hopeless romantic eeh? But ni vitu that I believe in jamaniii...

                                        
Anyway, kama hujui kupika basi jifunze at least vitu ambavyo your man likes. Na kupika sio rocket science anyone anaweza kujifunza.
Anyway ndo hivyo - I've thrown my 2 cents advice hapo ambayo hata mie mwenyewe ntajaribu kuifanya na kuikariri siku ya siku when I start living with a man.
Ila jamani if the man pia mara moja moja akikupikia - rahaaaaa eeh? Hehehehe...

Have a lovely day
xoxo

Tuesday, November 8, 2011

Eti Wanaume - You don't like Weaves??!!

Helloooowww,
Juzi I came across an article ilikua inaongelea why wanaume zetu hawapendi sie wanawake kushonelea Weave/weaving/hair extensions.. Whether umei bond au kushonea. Kumbe wana mind! Heheheh I didnt know that! Mara ooohh zinaonekana kabisa fake, Anyway labda men have a point. Let's see walitoa vigezo gani why they dont like them. You ready? Haya twende!!!!

1. Weaves zinaacha evidence
Hahahhah!!! (Sorry I just had kucheka) Hii of course itakuwa kwa wale ma players. Manake weave ukilichana linaachia - nywele kibao zinachomoka, zinabaki chumbani kwenye carpet na hata in the bathroom. And worse hua zinabaki on the bed!!! Kisha maybe wee ni mpango wa kando aka nyumba ndogo aka side chick, The guy anaogopa kukamatwa ndo maana wanachukua weaves!! Shame on you players!!!!
                                                
2. Weave zote zinafanana
Nani kasema!! If you guys were the ones munanunua ndo mungejua weave hazifanani! Kuna Indian, Brazilian, Italian and kuna pia Plastic - ambazo hizi hazifai kabisa coz you can't set it. We know better.. na kama you would have been the one buying pamoja na tofauti za bei then you would understand more. Ndo maana munakamatwa nyie guys when unaning'ang'ania kuwa its my hair wakati I know for sure it's not!!!
3. No touching my hair 
Utaziharibu bwana. I spent 30 minutes asubuhi nikizachana. Sasa unataka uzipapase ili iweje!!! Dont mess with my weave!! Hahahahah!!! 
4. Tukigusa vichwa vyenu kuna bumps
Guys this is only when ni weave za kushonea - but bonding inakua bumps hauzi feel sana.. Eeeh I'm clearly trying to justify myself - ila honestly hii ni ukweli!!
8: “Pull my hair.”
Neno tunajua linatumiika sana when having sex - in the heat of the moment tunajisahau tumeshonea weave kisha unamwambia - pull my hair - mara uuuwwiii unakumbuka it's a weave - unadakia - don't pull my hair.. Ni ukweli pia kuwa we can't go swimming kwa sababu (kama sio original weave) zinaharibika! OOhh weeelll kila kitu kina a price to pay - weave ni kwa wanawake to pay!

9. Zinanuka
This is only kwa wale wadada wanaokaa na weave zaidi ya mwezi mmoja kisha hawazioshi! Sasa what do you expect! Hii ni kweli! Kuna jasho, dandruff na mafuta - mchanganyiko wake harufu ya hatari!! Wash your weave girl usituaibishe!

10. Zinaoneka Fake
Do you really want to talk about fake? Mbona hulalamiki about fake nails, fake boobs, fake makalio (ya mchina) na mengineyo? Au unachagua what not to like tu ilimradi? Na sitokataa kuwa kweli kuna weaves nyingine unaona kabisa mshono umepitia hapa au nywele zimeishia hapa, but kuna nyingine zinashonewa vizuriii hadi you guy think it's real hair!!! Sema tatizo zile za ukweli sanaaa hatuwezi ku afford hiyo bei! Wanaoweza ni kina Ashanti, Beyonce na kadhalika.
 11. Hawezi ku run his fingers through nywele
Hii nakubali kiroho safi... Wakati wa ku cuddle na mwenzio kisha anataka akupapase nywele aingize vidole in between the hair, anakua anakutana na visivyoeleweka hapo kati!! Tehetehetehe... Ma lavy davy mengine yamepitiliza ujue!!!  But then again hata kama bila weave na nimetoka kutengeneza my hair salon kisha unapitisha midole - hahahahah no way!! Stay off my hair!!

12. Anajiweka High Class sanaaa..
Mwee! As if that's a bad thing!! Kweli??? Eti guys think kuwa ladies wenye natural hair ni down to earth and wachapa kazi but wenye kushonea weave wanapenda kujiweka high class and love to flirt!! Hii imetoka wapi?? Utakuta ni assumption ya mtu mmoja tu kisha akasambaza kama hizi msg za jokes!! It's a lie oooh (In Nigerian accent)


Ila yote tisa, kumi - It's my hair!! Si nimenunua with my money!!! Be it a weave au kama ni za kwangu original zote ni za kwangu!! Kwani hair inakuhusuje? Au ndo utasema - I love you wholly and completely kwa hiyo inabidi nipende kila kitu. I beg to differ. Nipende kote basi uniachie hiki kichwa! Hahahha! I joke.. Ukipenda boga penda na ua lake- ukinipenda penda na weave yangu!!!

                                                      


Mi mwenyewe I'm rocking a weave and proud of it!!!!

         xoxo
have a good day..                                             

Thursday, November 3, 2011

Sjui Nisemeje...

Hello...
Leo i came across a story iliyotokea Russia - ambapo kuna watoto wawili wa kike walizaliwa in the same hospital ila wakabadilishiwa vile vitag vya mkononi. They were switched (sjui kama ni by bad luck au ni kwa kukusudia). Anyway ilipelekea moja ya familia za these girls kwa their parents ku divorce as baba mmoja alimshutumu the wife kuwa she cheated on him coz mtoto alikua hafanani na huyo daddy kabisa!
12 years later imegundulika kuwa wale mabinti walikua switched after birth baada ya kufanya DNA.
Familia hizi mbili zimekua awarded dola laki 1 each kwa usumbufu uliojitokeza. But imajin kumlea a child for 12 years kisha mwishoni unaambiwa sio wa kwako. Imajin baada ya emotional attachment iliopo kati ya these girls and families zilizowalea kisha wanakuja kung'amua kua this is not my mommy or daddy. Imajin one of the families ni wakristu nyingine ni muslims wamelelewa katika dini na maadili tofauti. Hawa mabinti wamesema hawataki kurudishwa kwa their bilogical parents kuwa wako satisfied kuishi na wazazi waliowalea since birth.
Na hizi familia mbili zimeamua kwa kutumia the money waliyopewa watanunua nyumba moja kubwa na kuishi wote ili wawe karibu na their biological children au wanunue houses next to each other ili wawe neighbours.
But nimekaa hapa I'm thinking how many families wanaishi na watoto who are not theirs? How many women wanashutumiwa kuwa wame cheat na kujifungua watoto ambao sio wa baba huyo kumbe walibadilishiwa watoto. Tena at least huko nchi za nje kuna investigators unaweza kufuatilia vitu - hapa kwetu jee? Si ndo usahau? And kwa mfano ikitokea hapa kwetu - will you be awarded anything?
Which reminds me - eti wale wagonjwa ambao walikosewa kufanyiwa operation - wa mguu akapasuliwa kichwa na wa kichwa akapasuliwa mguu - were they or their families awarded with anything na serikali?

Contact me - babo25@gmail.com or sms 0759 008500

Love ya
xoxo

Tuesday, November 1, 2011

Desparation inaweza kukupush kwa kiasi gani?

Hellow beautiful people,
You good? Weekend nilipata kuangalia movie inaitwa 35 and Ticking...


This pushed me kuangalia maisha ya wanawake wenzangu tofauti. Ujue it's soo easy for us kupoint fingers na kusema - yule mbona hajaolewa hadi now, anasubiri nini? Anajali sana about career na kuweka mapenzi pembeni? Yule mbona hazai... nk..
Society kwa ujumla inatufanya sisi kama wanawake sometimes kujichukia na kupata depression ya hali ya juu because of what they expect us to do kwa muda flani. Kwani kuna sehemu tunaambiwa wanawake tuwe tumeolewa by miaka mingapi, au tuwe tumeshapata watoto kabla ya kufikia miaka flani? Aaah this thing hua inanichanganya sana.
My point is - pindi unapokua umechagua au kujiwekea your own goals in life - labda umejiwekea kuwa you wont get married hadi upate Masters ya whatever... Ila watu wa nje wanaanza kukusema - Ooh doesnt she hear the biological clock ticking. Jamaniii.. Watu wana malengoooo.. Hehhehe.. Ila kweli inaboa.
Basi na wewe mwanamke mwenzangu when you hear people talking about you unapanic! Unatafuta bwana kwa haraka au unaanza mambo ya online dating ( who said that works anyway) Unaishia kupata mtu ambaye haeleweki coz kwa ajili ya haraka unakua unamfahamu kijuu juu tu. Mukishaoana au after kufika mbali in the relationship anaanza kukuonyesha vimbwanga! Unajutaje! Tena hao wa kukutana through the internet unakuta kasema yeye ni mwembama (kumbe mnene), hana kazi (very successful) etc...                                                        
Hahhaha That's another topic for another day...
 Kwa hili la leo.. Nipe comment zako - Labda mi sjui kama kuna a certain age ambayo wanawake tunatakiwa tuwe tumeolewa au kuondoka home kwa wazazi au kupata watoto. Kama unafahamu please tuhabarishe.

Advice from me..
Live your life - in the process - achieve your goals. Ukisikiliza sana watu you wont get anywhere.Be you and do what YOU love. Don't let peer pressure choose your life path.   Love yourself.

xoxo
Have a lovely day

ps... Contact me - barbshassan@gmail.com
sms - 0759 008500                                         
 

Sample text

Sample Text

Sample Text