Social Icons

Pages

Friday, May 25, 2012

Nifanyeje???


                                           

Shikamoo Dada Barbara,
Naitwa Lucy ni msichana wa miaka 23 na nipo chuo mwaka wa pili. Natokea katika family ya middle class na mama yangu ni single parent. Sijawahi kumfahamu wala kukutana na baba yangu. Nina boy friend ninayempenda sana na tumekuwepo kwenye mahusiano kwa miaka 2 sasa. Nilikutana naye chuoni. Na ndio nashiriki naye kimapenzi.
Mwezi jana mama yangu aliniita nikakaa kitako akidai ana mambo anata ku discuss nami. Ila alichoniambia kwa kweli kimeni frustrate sana na nipo njia panda sasa hivi. Mama alinambia kwa sauti ya upole na iliyojaa majonzi kuwa " Yeye ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na alibeba mimba yangu wakati ameshaathirika bila kujijua." Kwa hiyo ina maana mimi ni carrier wa HIV. Aliniomba nimsamehe kwani anahisi ameniharibia maisha yangu. Sikua na cha kumjibu na sijapata hadi sasa hivi. Nilienda kupima ili kuthibitisha na kweli nikakuta mimi ni muathirika. Sijui cha kufanya na mawazo yamenijaa tele. Na huyu kaka wa watu - my boy friend nimeshafanya naye mapenzi mara nyingi tu bila kutumia kinga. Naanzia wapi kumwambia hali yangu? Nahisi ataona mimi nilikua naifahamu hali yangu all through and chose not to tell him. Si ataona nilikusudia kumuua?
Katika chuo ninachosoma kuna a counselling center nimekua nikishinda humo kwani nimechanganyikiwa kabisa!
Naomba msaada wako wa kimawazo - na pia kutoka kwa wasomaji/ wadau wa blog hii..

Mubarikiwe
Lucy...

                                 
PS. Kwa leo sina comment. Nakuomba wewe mdau wa blog yangu tumsaidie Lucy...


Tuesday, May 22, 2012

Hereni....

                           

                                      Mambooooo.. Kwema?
Nina swali.. Je before ununue earings hua unangalia nini?
Urembo, kama ni Unique, bei au uzito??? Mimi binafsi cha kwanza kabisa naangalia urembo - kama they are attractive na cha pili ni uzito. Umeshawahi kununua hereni and then later on unashindwa kuvivaa because ni vizito kupitiliza? Hereni nyingine zinakua nzito kiasi cha kuwa inatanua kale katundu ka skio. Ishawahi kukutokea? So umeamuaje? Urembo kwanza au uzito kwanza? Hehheheheh. Urembo taabu jamani..

Hebu angalia jinsi skio linavyovutika...... Pindi unapovaa heavy or wide earings...

 Aisee hata kama ni fashion - acha niiitwe mshamba....


 mmmhh... Hapanaaaaaaa.....                             
Nisijeishia kua na maskio ya hivi..


Things to consider wakati wa kununua hereni.

- Material - zimetengenezwa kutumia material ipi? (plastic, silver, chuma) Ukizingatia what are you are allergic to...
- Uzito - Zitavuta maskio yako?
- Upana - Zitatanua kitundu cha skio?
- Unique - unique badala ya fashion (this is my motto) Although wengine wanaangalia how sexy they are au kama zipo in fashion.

Karibu kuongeza maoni yako...

Contact me:
Email - barbshassan@gmail.com
SMS - +255 759 008500

Thursday, May 17, 2012

Tatua Thursday....


                                                                       

Mambo Barbara,
Najua fika kua hua unapokea na ku post zaidi matatizo ya wanawake, ila hata sie wanaume tuna matatizo yetu... Na ndicho kilichopelekea mimi kukuandikia leo hii. Naitwa James, na nipo katika mahusiano na a beautiful lady ninayempenda sana na nia yangu ni kufunga naye pingu za maisha one day.
Tatizo linakuja kua mimi napenda sana sana kukiss. Nilijifunza kukiss baada ya kuona kwenye vipindi kwenye tv na kwenye movies. Nikaanza kujifunza  kujikiss mwenyewe kwenye kioo, mara nyanya au chungwa. Hadi nilipojiamini kua sasa najua ndo nikaanza kukiss ladies. Wazungu wanasema practice makes perfect - najiamini sasa hivi mimi ni bingwa wa mabusu. Tatizo langu ni kua my girl friend hajui kabisaaaa kukiss, na wala hana interest ya kutaka kujifunza. Mimi inaniwia ngumu sana sana. Manake ni kitu ninachopenda zaidi kufanya, in fact napenda zaidi kukiss kuliko sex. Ila mwenzangu na mie yaani wala, nikifuata midomo yake ya juu yeye ananitolea ulimi na akiwa amejaza mate kibaooo. Sina kinyaa ila inaboa.
Munanishaurije?
Je - nimuache na kutafuta a lady anayejua kukiss?
Je - nimvulie tu - ila itaniuma sana
Au ning'ang'ane kumfundisha tu - although hana hata mpango wa kutaka kujua kukiss.
Naomba msaada please.

Regards,
James

Kwa kweli wengi tunachukulia kissing poa - ila I'm one of those people ambaye napenda sana sana kukiss..  My first experience ya kukiss huyo jamaa alikua kala vitunguu! Aiseee nilichukia kissing kwa muda mrefu sana. Hadi nilipopata mtu ambaye alinifanya nipende kissing. Right now hunambii kitu!! Hahahhah. Experience yako ya kissing ikoje? Unapenda why? Na kama hupendi why? Na kama hujui - je unafanya nini ili kujifunza?  Manake wenzetu wanasema - Kissing is opening the window to someone's soul.
Funguka na pia tumsaidia James... Maoni yako ni muhimu sana...


                                         
mwaah!!!
have a great day

Thursday, May 10, 2012

Mothers Day.....


                               Hello...
Siku tunayo feel special, ku feel tunapendwa na kua appreciated kama kina mama inawadia.. Ni 13th May - Mothers Day...
Aunty Sadaka ameandaa event itayotufanya tuji feel more special sisi kama kina mama na familia zetu..

" To celebrate mothers day, Aunty Sadaka ame organise a special event kusherehekea motherhood. All mothers na kina baba wanakaribishwa. Mlete mama yako, aunty, sister na any significant woman katika maisha yako at JB Belmont this saturday 12th May for dinner, dance na special activities. Show your appreciation to this special woman in your life kwa Tsh 50,000 kwa kila mmoja.

A CHILD"S BEST FRIEND IS THEIR MOTHER....

USKOSE....

Pata ticket yako mapema at - Shear Illusion - Mlimani City au Nyumbani Lounge au piga namba - +255 655 717575 au +255 787882


hugs
xoxo

Tuesday, May 8, 2012

Saidia Kutatua Tungo Hii......


                                                             
BABRA MIMI NI MWANAMKE WA KITANZANIA IMEOLEWA NA NINA MTOTO MMOJA  WA KIUME NA MUME WANGU JAPOKUA AMENIKUTA NA MTOTO MMOJA WA KIKE. TULIKUBALIANA NA HANA TATIZO LA KUMLEA BINTI YANGU.
MAHUSIANO YETU YALIANZA KAMA UTANI, MUME WANGU NILISOMA NAYE SHULE YA MSINGI! LAKINI TUKAJA KUPOTEZANA KWA MIAKA MINGI, LAKINI NIKIWA WAKATI WA MCHANA NA RAFIKI YANGU  KWA AJILI YA CHAKULA CHA MCHANA AKAPITA. NIKAMWAMBIA RAFIKI YANGU! "MH HUYU KIJANA NAHISI NAMFAHAMU"  AKATUPITA BILA KUJUA. ALIPOFIKA MBELE KIDOGO, NIKAMWITA NA KUMKUMBUSHA, AKAFURAHI KWELI. NILIPOTAKA KUJUA ANAKOELEKEA, AKANITAJIA JINA LA OFISI YETU, NIKAMUULIZA KULIKONI? AKAJIBU AMEAJIRIWA HUKO.
BASI MAISHA YAKAENDELEA KAMA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI MOJA, WAKATI HUO NILISHAACHANA NA BABA WA MTOTO WANGU WA KWANZA.BASI BINADAMU AMEUMBWA NA HISIA! TUKAANZISHA MAHUSIANO YA KIMAPENZI. LAKINI KATIKA KAMPUNI HIYO HIYO KUNA MWANAMKE ALIKUA ANATAFUTA MTOTO, BILA KUTEGEMEA KWA SIRI WAKAANZISHA UHUSIANO! LAKINI MTU HAKUNYIMI NENO, NIKATONYWA, WALAKINI SIKUTILIA MAANANI NA WAKATI HUO MIPANGO YA NDOA ILIKUA INAENDELEA, SO NILIJUA NI NJAMA NA HILA ZA WALIOKUWA HAWANITAKII MEMA, KUMBE KWELI.
BASI, WAKATI NDOA INANUKIA NAMI NLIKUA NI MJAMZITO, NIKASIKIA YULE DADA NAYE MJA MZITO, SI NIKAULIZA KWA MUME? AKAKATAA KATA KATA, NIKAMWAMBIA NI BORA UWEKE MAMBO SAWA SASA HIVI, AKAENDELEA KUSHIKILIA MSIMAMO WAKE. NIKAACHANA NALO. KUMBE WENZANGU WANAENDELEA KWA SIRI NA MTOTO AKAZALIWA WA KIUME KAMA WANGU NA ANAFANANA NA BABA YAKE NA NIKASIKIA TENA HUWA ANA KWENDA KULE NA HULALA PIA!
DUH! BASI SIKUAMINI! MARA ZIKAANZA SAFARI ZA KWENDA MARA HUKU AU KULE! AMA ANASINDIKIZA MSIBA, MARA OH NILIKAMATWA NA POLISI ANARUDI ALFAJIRI, MARA ANIRUDIE NA T-SHIRT TOFAUTI UKIULIZA OHH NLOVAA ILIMWAGIKIWA NA KITU NIKANUNUA NYINGINE YA MTUMBA. SAWA SASA HIYO CHAFU IKO WAPI TUFUE, OH NILIITUPA! UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBU, SIKU INGINE ALIPOKWENDA KULE AKAACHA ALICHOVAA AKARUDI NA ILE TSHIRT ALO DAI KAITUPA! NIKAMUULIZA! NIKAZUNGUUSHWA! NIKASHIT
MBAYA ZAIDI MAMA MKWE ANA MSHADIDIA YULE WA NYUMBA NDOGO! NIKAWA NAZIDIWA NA TAARIFA ZA MUME WANGU KUA ANAZIDI KWENDA KWA HUYO DADA MPAKA WALIOKUA WANAMUONA WANANIONEA HURUMA! NIKAITWA TENA NA TENA NIKAAMUA KWENDA. NIKIWA NJE NASUBIRI ATOKE NIMDHIHIRISHIE KUWA ULICHOKUA UNAKATAA MI NAJUA UKWELI WOTE, KULE NDANI NIKAWA  NAPEWA TAARIFA ZOTE ZA KINACHOENDELEA, SASA WAPO SITTING ROOM,SASA WAMEINGIA CHUMBANI, SASA WAKO BAFUNI, SASA WAMETOKA SEBULENI,MARA NIKAELEZWA NDO WANATOKA HIVYO NIWE TAYARI. BASI NIKASOGEA KARIBU NA MLANGO NIKASIKIA WANAVYO AGANA,KWA MABUSU TELE TELE, MTOTO NAYE AKAWA ANAELEKEZWA KUMBUSU BABA YAKE ANAONDOKA! YOTE NAONA NA KUSIKIA JAPOKUA WAO WALIKUA HAWANIONI.
NIKAONA INATOSHA NATAKA WOTE WAJUE NINAJUA KILA KITU, WALISHTUKA NUSU WAANGUKE! MTOTO AKAKIMBIZWA NDANI, MUME ALIKUA HAAMINI MACHO YAKE, NIKAMWAMBIA MUME  WANGU HAPA NDIPO ULIPO AGA KUA UNAKWENDA? MAJIBU YALIKUA MAGUMU.
NIKAAMUA KUWAACHA NIKAONDOKA ZANGU, KIUKWELI HAIKUA RAHISI NILIKUA NALIA KILA SIKU NA  KULA CHAKULA HAKIPITI. PRESSURE NA KILA KITU KIBAYA KILINIELEKEA MIMI. ILA NILIYASHINDA YOTE. KWA SASA NA JIONEA KAWAIDA TU AENDE AMA ASIENDE POA TU, NA TAARIFA ZAKE NAPATA ZOTE NAPATA.
LUCY
PS - Rukhsa kumshauri Lucy. Ingekuwa wewe Ungefanyaje????

Ukiwa na story yako nitumie - email - barbshassan@gmail.com
au SMS - +255 759 008500

Wednesday, May 2, 2012

Ulikutana na Mume au Boyfriend wako wapi?

Mambo,
Pole sana kwa kuwa kimya for a while.. It's a long story.... Ila naomba radhi kwa hilo... I was thinking, unajua jinsi mashangazi na wazazi wetu wanavyotulazimisha kwenda maharusini? Especially kwa sie ambao hatujaolewa. Wakiamini kuwa huko ndio tutakutana na "potential husbands" Sijui kama kuna ukweli wowote ndani ya hili. Anyway nikaona si vibaya tupeane advice kuhusu wapi tunaweza kukutana na hao "potential husbands". Na tunaweza kufanya hivyo kwa wewe ku share ni wapi ulikutana na aliye mume wako au boyfriend wako kwa sasa... I believe itasaidia sana.. Hehehehhehe
Je mulikutana club au bar? Ila hua wanasema eti ma boyfriend utakaoanzana nao club hawadumu


Au harusini?

Courtesy of www.8020fashions.blogspot.com

au kwenye funeral?

         
Airport?Ndani ya bus au train?

                             
Au ofisini?

                                           

Fungukaaaaa.. Hehehehehe..

For a private neno niandikie - barbshassan@gmail.com
or SMS - +255 759 008500

much love
xoxo
 

Sample text

Sample Text

Sample Text