Social Icons

Pages

Monday, June 4, 2012

Nisaidie...


                                        

Hello Barbara,
Im sorry na share nanyi stress zangu jumatatu.. But sikujua nitapata wapi usaidizi. Mi ni mdada nimeolewa na nina watoto wawili wavulana. Mmoja ana miaka 7 na mdogo ana miezi 8. Naishi na mume wangu pamoja na mtoto wa babangu mdogo (cousin wangu) ambaye hunisaidia kazi za nyumbani ila hua namlipa mshahara.
Amekua akifanya kazi vizuri tu, kunisaidia kulea wanangu na hata kuwasaidia na homework pindi ambapo mimi na mume wangu tunachelewa kufika nyumbani.

Juzi ijumaa cousin wangu alitoa kali ya mwaka. Mimi pamoja na mume wangu tulikua kazini, na mwanangu wa kwanza alikua shuleni. Cousin wangu alibaki na mtoto mdogo kama kawaida. Cha kushangaza niliporudi  nyumbani mida ya saa 10 na nusu nilikuta mlango wa nyumbani ukiwa wazi. Nikaingia nikamuita cousin yangu bila majibu. Kuingia chumba cha watoto nikamkuta mwanangu mdogo kalala kwenye kitanda chake akiwa mwenyewe na wa moto ajabu. Amejikojolea, kujinyea na machozi yamekauka katika macho yake.

Nikaenda kwa jirani kuuliza kama wamemuona dada, wakasema aliondoka toka asubuhi. Si ndo mie kushtuka. Dada wa nyumba ya jirani akanambia amemuona bar ya jirani. Na wakasema wamemskia mwanangu akilia siku nzima. Imagine mtoto wangu kumbe alikua hajala, hajaogeshwa, hajabadilishwa pampers siku nzima. Nilisikitika sanaaaa. Nikampikia mtoto na kumlisha, nikamuogesha akalala. Nikakaa kumsubiri dada, aliingia nyumbani saa 12. Yuko njwiii kalewa balaaa...
Hivi kweli angenambia nini nimuelewe? Alishindwa nini kununua pombe na kukaa anywe ndani ya nyumba huku akimuangalia mtoto? Ni unyama wa namna gani huu?
Sasa leo nimeshindwa hata kwenda ofisini niko nyumbani. Sijui nitaanzia wapi kutafuta dada mwingine. Naomba please wadau wa blog hii munisaidie..

Claire
Dar Es Salaam..

7 comments:

 1. pole sana, lakini huna simu ya nyumbani au hata ya jirani ili uweze kucheck on ur kid from time to time, maana hata ukipata mtu mwingine haisaidii kama huwasiliani na nyumbani siku nzima

  ReplyDelete
 2. kwani hata jirani ameshindwaje kukutumia sms kwamba mtoto analia peke yake huko ndani, thats very bad jamani

  ReplyDelete
 3. Pole sana dada! that was too bad jamani for a baby of 8 months! fanya uwe na utaratibu wa kuwasiliana na nyumbani, hata ukipata msichana mpya mtafutie simu uwe unajua kinachoendelea au hata jirani ni vizuri kuwa namba ambayo unaweza kuwasiliana au wao kuwasiliana nawe pindi inatokea chochote.pa kuanzia dada wa kazi si uagize toka kwenu mkoani?

  ReplyDelete
 4. pole sana. nimeumiaje nikiwa kama mzazi.jamani hao majirani wana roho za ajabu. walishindwa kutoa msaada kwa mtoto. bila haya wanakupa detail zote. hao jirani zako sio watu wazuri hata kidogo. pili huyo binti mrudishe kwao tafuta mwingine.

  ReplyDelete
 5. Pole sana dada.. watoto wetu wengi siku hizi wanapitishwa kwenye mambo ya ajabu kama hayo na ni mpaka ukija jua na kufahamu hivyo unakuta mtoto alishateseka kwa muda mrefu sana. Pole ila pia mimi huwa nasema ni bora mtu baki kuliko ndugu! Maana ndugu wanakuwa na kashkash mmh...wanakuwa wazuri kwa muda halafu wanaanza kulalamika kuwa huwapatii hiki na kile...kwamba unawadharau..kwamba unamfanya yeye housegirl...mambo mengi. So ningekushauri utafute mtu tofauti na ndugu yako kwa namna moja ama nyingine.

  ReplyDelete
 6. Nilipokuwa nasoma nilidhan cousin ni wa kiume afu mtoto kabakwa. Nadhani wenye watoto mtanielewa; yani mtu unasoma story huku kwa woga unaanza kupredict mwisho utakuwaje. Nikirudi kwenye mada; piga goti mshukuru Mungu kumkuta mtoto mzima. Hainiingii akilini huyo cousin wako ambaye ni binti kuwa mlevi; hapo usije kuwa umesogeza mke mwenzio kwani ana tabia chafu bila hata ya mtu kusimuliwa.

  Ma housegirl wapo japo ndio ni ngumu kupatikana. Mimi niko ne ya nchi kwa muda ningekuulizia kwa ofisi mate wangu aliwahi nambia kuna agent mwenye wasichana wa kazi tena wako very professional na wala si that much expensive. Alinambia analipa 60 au 70 kama sikosei; sasa kwa bei hiyo na unapata a well trained housegirl Mungu akupe nini. Mimi mwenyewe nili take note nilenaye akinizingua natafuta hao professional ambao mnaandikishiana na unakuwa na details zake zote na ana mdhamini juu

  ReplyDelete
 7. Conѕciousness enters jοb titlе and is a deaԁ on target masseur.
  Piecе the estimаte of hаving needles systematiсally combine a traԁitional, Blooԁ line-baseԁ coming with the best cоntеmρorаry, Neo-Tаntriс methоds.

  Bila аnda khawatiг bokong andа nampaκ mаnpower apρlying oil onto tegument ѵolition not hаvе
  the coveted еffect of аrousing a Spouse.


  Here is my web-site: tantric massage

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text