Social Icons

Pages

Monday, January 30, 2012

Me time...

                                                     



Hello,
Nisameheni sanaaa sanaaa kwa ukimya wa takriban 2 weeks.. I got some time off kazini.. Nikaona nipumzike kamili kamili, manake nilikua hoi! Waking up at 4.30am kila Monday to Friday si mchezo.. I know I should have said bye, but mambo yalikua mengi nikaona siku zinazidi kuisha, nikaamua kusafiri na kwenda mbali kidogo kupumzisha akili.
Hakuna kitu kizuri kama kujiwekea time ya kwako mwenyewe. Me time!!! Time ya kutafakari kila kitu kuhusu wewe. Career, family, friends, love etc...
Kwa wenzetu vacation aka mapumziko ni muhimu sanaaaa..Kuna wengine wanakwenda wenyewe, wengine family nzima. Na pia kwa wenzetu hua wanafungua kabisa bank account na ku save every month - lengo likiwa ni kwenda vacation nzuri that they deserve...
Je, Umeshawahi kuchukua mapumziko? Ulipimzikia home, mkoani au ulisafiri ukaenda a place where no one knows you?
I know utasema ooohh majukumu ni mengi - ada ya watoto, house rent ya mwaka mzima, vyakula vimepanda bei nk... But kwani hao wanaokwenda vacation hawana majukumu kama yako? Ni maamuzi tu.
For example - last year April nilikwenda Ngorongoro nikakaa Serena Hotel for 3 days na nikakaa Manyara Serena for 2 days na family yangu. It was very nice. Watoto walifurahi sanaaa na wadogo zangu and tukarudi na experience, furaha na tukiwa tume relax vya kutosha...







Tukatumbuizwa na Wambulu aka waIraq..... Beautiful.....


Hapa kwenye pool ndo nilispend more time.. the view... mmmmhhh...

Anyway, wiki hizi 2 nilikwenda Mombasa... nikakaa hotel inaitwa Reef Hotel...
Nilikwenda mwenyewe coz nilihitaji kupumzika kabisaaaa.. I was sooo tired...

It is breathtaking... Upepo mwananaaa, swimming pool, bahari ipo karibu, mawimbi yalikua yananibembelezaaaaa, nice food, tasty cocktails, watu wazuriiii wa kumingle nao, nikala ubuyu, achari, vitoria, zambarau na tende za kumwaga...Plus bei zao ni very affordable...  I had sooo much fun..
Anyway, jaribu na wewe ukapumzike japo weekend moja.. Na sio lazima uende mbali. Hata hapo Bagamoyo tu. Chukua room yako - kama ni mwenyewe, au na mwenza au na family mulale friday na saturday mugeuze sunday - you will be shocked na jinsi utakavyo feel baada ya mapumziko hayo..

Niliwamiss sanaaaa.. Im back now .. Wanawake ni sisi - inaendeleaaa...

Much love,
xoxo


                          
                                             

                                             

Tuesday, January 10, 2012

Family Vs Kazi....

                                                     


Hellow,
Ningependa kukufahamisha kuwa tutakua tunajaribu kutatua na to give advice kwa watu tofauti watakaokuwa wanatuma emails za whatever they are going through every alhamisi. Nimeipa jina la - Tatua Thursday.. Kwa hiyo feel free kutuambia tatizo lako na nitaipost hapa na kuomba ushauri kwenye email ya - barbshassan@gmail.com
Jana niliangalia movie inaitwa Chrismas Cupid starring Christina Millian na wengineo. Hii movie ilinikumbusha how tunakua sooo engaged na pilika pilika hadi tunasahau vitu very important maishani mwetu. Mf You get sooo into your job - kwa sababu labda unafukuzia promotion au kuongezewa mshahara hadi unakua hupati muda wa ku spend na familia yako na close friends..
If I ask you - Chrismas na Mwaka Mpya ulispend vipi na wapi utanijibu nini? Je
- Ulikuwa kazini?
- Ulisafiri kikazi?
- Ulikaa na marafiki?
We usually take things/ people for granted. Tena tunawaonea zaidi family and friends. Umewahi kujiuliza labda if anything happens to you - kama ajali au hata kifo (Mungu atuepushie) nani ataumia zaidi? Nani atakumiss zaidi? Nani atakuwepo there for you? Kikazi watatafuta mtu wa kuku replace.. But your kids hawawawezi kupata replacement ya mama au baba... your friends hawawezi kupata replacement yako...
Ninachojaribu kusema ni kuwa pamoja na kuwa unawatengenezea watoto na familia yako kwa ujumla a better tomorrow kumbuka kutenga muda kwa ajili yao. Spend time with them as much as you can.
Cook for them, nenda nao swimming, play with them, hang out nao, wapeleke shule when you can.. It's the small things that matter.. Work will always be there, but work haitokupa the love that your family na close friends watakupa...


                                              
Be blessed,
xoxo

Wednesday, January 4, 2012

Salute!!! All Women!!!!

Nimetumiwa hii nikaipenda sana... I decided to share..

                                         


Kuna tukio nililiona MAISHANI:
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake wooote:
Imagine:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa, anakusamehe - halafu anasahau.
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuchia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeenggggiiiiii sana wanafanyiwa hawa watu lakini
WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

I SALUTE AND LOVE WOMEN!!!

Why Did I Sleep With Him... Part 2

Hellow...
Nimepata hii email nikaona sio vibaya ku share na kujaribu kumshauri mwenzetu...

Hi barbara,,
Mm ni binti wa miaka 26 bt nimeshapitia machungu mengi kny relationship!
Nimekosa usingizi nikasema ngoja nipitie kny blog yako coz huwa unanifurahisha na topics zako na maneno unavyochombeza..kiukweli huwa nafurah sana!
Comin back to the topic...kama mwezi mmoja umepita nlikutana na mfanyakazi mwenzangu makao makuu ya ofisi yetu,kiukweli kaka ana muonekano mzuri bt sikuwah kuhisi kama ninampenda mpaka alipoanza kutafuta pin yangu na no ya simu na kuanza kumsumbua mfanyakazi mwenzangu akisema ananipenda n anataka awe shemeji yake so anipe ili tuwasiliane!
Nilihofia kumpa coz najua baadhi ya vijana wa ofsn kwetu ni vimeo balaaa ila aliendelea kumsumbua so ikabidi nimpe nimsikilize anataka nn!
Alianza kwa kunisifia yo so beautiful bla bla kibao na akawa anataka tuonane!Nilimkwepa bt kasi aliyokuja nayo mpaka nilikubali mwenyewe kumuona!
That day ndo nlihisi naanza kumpenda n ana mvuto kiukweli n naye hajafika 30's bt yuko mbali kimaisha!Nilikuwa nina muda mrefu nikiwa single n nlitaman niwe na mtu kiukweli tena age mate wangu weee...nlichanganyikiwa kiukweli na huyu kaka!
Ngoja nirudi na flashback....baada ya kupata pin yangu,tulikuwa tunachat mpaka midnight n akaniambia hana galfriend kwa sasa,,guess nilifurahijeeee?
But kwa upande mwingine ckutaka kuanzisha mahusiano na colleague coz mkibwagana mnaweza mkachukiana na mkashindwa kufanya kazi!
Aliniomba tutoke n ckumkatalia coz nlijikuta naanza kummiss from nowhere!
Siku tumetoka nilishindwa kuresist na nikajikuta nimekubali kufanya nae mapenzi n I enjoyed it coz ni mtu ambaye nilimpenda kutoka moyoni!
Baada ya siku mbili si ndio ananiambia ana galfriend n wamekaa almost six years n kaona aniambie mapema coz it will be unfair n bla bla kibao!niliumia sana na bado inaniumiza sana bt nlimjibu tu NO PROBLEM bt kiukweli mpaka naandika hii mail ni sa 7 usiku siwezi hata kulala namfikiria yy n y aliamua kunifanyia ivo!
Kupunguza machungu nliamua kwenda runway nikidhani nitapunguza machungu bt nliona makelele ndo yananichanganya so nikaamua kutoka zangu nje na kufikiria bila kupata majibu!nilirudi home nikafikia kny kioo nikajiangalia nikasema nina mapungufu gani kama mwanamke,,,cna akili?No o kaniona npo easy sana?bt wanaume hata umbanie mwaka mzima ukimpa tu anaweza kukubwaga!!
Tumedeletiana BBM n hadi phone no bt mbaya zaidi tupo ofisi moja n I regret why did I sleep wit him?wakati niliweza kukaa muda mrefu bila kuwa na mtu,,Y yy nlimvulia nguo??najuta sina maneno ya kuelezea maumivu ninayopata kwa sasa
Ninamchukia n wil hate him for the rest of my life n cjui nitafanya nn nikimuona!
It is between me and u kama utaipost plse jina langu lisiwepo!
Kama utahitaji any clarification mi nipo ila sina hamu tena ya kupenda na nikiona gari la Gx 110 ndo nasikia hasira coz ndo gari anayotumia!!
Thanxxx barbara

xoxo
email me - barbshassan@gmail.com
sms - +255 759 008500

Tuesday, January 3, 2012

Does it REALLY Matter???

                                       



Hellow people...
Kwema? Tumeuonaaaaa..... (cheering)
Mi najiona very lucky as huwa na meet a lot of people - wa kila namna - ni kwa ajili ya kazi ninayoifanya.. Huwa napata story kibao in the process.. Za kuhuzunisha na nyingine za kufurahisha.
My point ni kuhusiana na wanawake ninaokutana nao ambao ni wazazi - and maybe hata wewe ushawahi kukutana na hili....
Wanawake wanakuaga soooo conscious kuhusu mtoto anafanana na nani kati yake yeye na baba mtoto! Mara nyingi - And I dont know why - wanawake tunapenda sanaaaa kusema (hata kama sivyo) kua mtoto kafanana na babake.... Tunaweza hata kuanzisha ugomvi pindi mtu akiuliza why mtoto hafanani na babake...
Kwa Biology finyu ninaayokumbuka ni kuwa - mtoto anaweza kufanana na mtu yeyote kutoka kwa familia ya mama au ya baba mtoto..
Anyway - Kwani mtoto asipofanana na babake ina maana kuwa huyo sie baba mtoto? Na kwani inaleta tofauti gani kama mtoto hafanani na babake? Unajaribu kuthibitisha nini? Na utakuta kama mtoto hafanani na babake - unajaribu kutafuta features au vijitabia ambavyo unalazimishia kuwa mtoto karithi from the dad...
Au ndo yale yale "Ukweli wote anaujua mama" na "Kitanda hakizai haramu" So unajaribu kulazimisha kuwa mtoto anafanana na babake even if kama sivyo?
Msiniseme jamani - ni mtazamo tu....

             

Email - barbshassan@gmail.com
sms - +255 759 008500

Ubarikiwe..
xoxo                        
 

Sample text

Sample Text

Sample Text