Thursday, March 22, 2012
Tatua Thursday....
Mambo Barbara,
Mimi ni mdada wa miaka 32, mchagga wa Kibosho, sina mtoto, nina kazi nzuri tu katika Advertising Agency, naishi mwenyewe katika nyumba ya kupanga na namiliki kiwanja (nitaanza kujenga mwaka huu) na gari nzuri. Nimeshawahi kuwa na mahusiano ya mufa mrefu tu lakini tulikuja kuachana baada ya boyfriend wangu ku cheat. Nina mwaka wa 4 sasa hivi nipo mwenyewe. Nimejaribu kweli kutafuta boy friend mpya lakini inaniwia ngumu. Manake ninaokutana nao hawajanifurahisha hadi mie kukubali kuwa nao katika serious relationship. Wakati mwingine kikwazo kinakuwa dini, mara nyingine kipato au kazi yake, wengine walikua na mahusiano tayari ( staki kuwa chaguo la pili), wengine wameoa, wengine hawakuniridhisha kwenye sex. Nimejaribu sanaaa kujichanganya na watu wapya tofauti tofauti. Mara nyingine my girl friends wameni introduce kwa wakaka, hadi nilishajaribu internet dating na blind dates ila bado mwaka hadi mwaka najikuta nipo mwenyewe.
Sijui kama tatizo ni mimi kwa sababu nachagua sana - ila sitaki tena kuumizwa na kuchezewa. Ndo maana nakua very specific na ntakaye kuwa naye next kwa sababu nataka awe wangu wa milele. Naomba musaidie kunishauri
- labda niende maeneo gani kukutana na watu potential.
- niongee nao vipi mara ya kwanza ninapokutana nao.
- nivae vipi labda
- how should I carry myself wajue nataka serious relationship?
Naomba munisaidie... pleeaaassseeee...
Asanteni in advance..
Haya kazi kwako mdau wa blog hii.. Tumsaidie mwenzetu..
xoxo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni kweli unaonekana unachagua sana, sisi binadamu hakuna aliyekamilika, nakushauri kama umemuona anafaa na akawa ana kasoro moja labda ya dini au kipato hizo zinarekebishika, maana unaweza kumpata mwenye kipato leo kesho akawa hana, cha msingi ni upendo wa kweli, usizani ndoa zote walipata chaguo lao mwengine walipata dini tofauti na wameoana wanaendeleza maisha mwingine alipata mvulana mchafu leo hii kamrekebisha na kawa smart. pls base kwa mtu mwenye mapenzi ya dhati.
ReplyDeletedon't be so desperate, be calm when time comes you will find ur perfect partner!
ReplyDeleteni muhimu kumpata unayekufaa lkn kwa dunia hii ya leo ngumu kumpata cha msingi ni kupenda mengine yatarekebika taratibu.
ReplyDeletewe Anonymous Mar 22, 2012 03:36 AM mwenzangu umri unaenda dini ki2 gani wangapi wamefunga dini tofauti.
ReplyDeleteMpendwa unachagua sana na ukumbuke wewe pia una kasoro zako na hutapata aliekamilika binadamu tuna mapungufu mengi. Jitahidi kuchagua mwenye mapenzi ya dhati anaekupenda sana wewe ukipata unaempenda sana wewe anaweza kuja kukusumbua baadae. Ubavu wako upo, wakristo tunaamini kuwa mwanamke alitoka kwenye ubavu wa mwanaume. Siku ya tabasamu kwako inakuja. Omba Mungu akuchagulie.
ReplyDeleteMama Alice.
Pole, kwa uchaguzi wako, ww lengo lako ni kuolew au kujirusha tu, kama ni kuolewa nakushauri piga goti omba sana, mungu atakupa mwanaume mwenye sifa unazo zitakaa.
ReplyDeleteomba kwa kumaanisha utampata mwenye sifa unazozitaka.
MH POLE SANA HUWEZI KUPATA ALIYE KAMILI CHA MSINGI HAPO ANAYEKUPENDA RAHA NA SHIDA HAYO MENGINE NI YAZIADA NA TABIA YK YA KUONA KASORO ZA MWENZAKO ACHA JE WEWE UPO KAMILI NO BODY PERFECT ILA UNAMZOEA MWENZAKO THE WAY ALIVYO.
ReplyDeleteMama Brice
Nakushauri usome kitabu 'sayansi ya mapenzi' na 'ufundi ktk kupenda' vya dr. Paul nelson(wa kliniki ya afya ya mapenzi-iko mwanza) vina majibu ya maswali yako kwa kina,Usipopata ufumbuzi wa tatizo lako n'tafute nikurudishie pesa uliyonunulia vitabu(singidani028@gmail.com)
ReplyDeleteDifferеnt pаrtners have unlіke pгefеrenceѕ
ReplyDeletewhen it сοmes to manual and the touchеs ԁuring thе
Tantгic Massageѕ are dіffusеd аnd
On that point aгe no "blockaded" areas.
Here is my web-site ... erotic massage London