Social Icons

Pages

Wednesday, January 4, 2012

Salute!!! All Women!!!!

Nimetumiwa hii nikaipenda sana... I decided to share..

                                         


Kuna tukio nililiona MAISHANI:
Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake wooote:
Imagine:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa, anakusamehe - halafu anasahau.
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuchia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeenggggiiiiii sana wanafanyiwa hawa watu lakini
WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

I SALUTE AND LOVE WOMEN!!!

2 comments:

  1. thats so sweet! i women so love my mama and all other so much..

    ReplyDelete
  2. i lav my mama sanaaaaaa

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text