Social Icons

Pages

Tuesday, February 28, 2012

Stori....

                                                   

Hi, kwema?
Weekend nilikua na washkaji zangu. Tumekaa na kupiga sana story. Sikumbuki how but tukaanza kuongea kuhusu madada wa nyumbani. One of my friends akaanza kutusimulia story ya dada wa rafiki yake....
Kuna mdada kaolewa na anaishi na her husband na watoto. Yeye na mumewe wanafanya kazi, watoto wanaenda school, so wakahitaji usaidizi wa dada atakayekua anawasaidia kazi za nyumbani - kupika, kufua, kufagia na kupiga deki nk... Sasa basi familia hii wakawa kila siku asuhubi wanaamka wamechoookaaaaa.... Watoto wanasinzia shuleni na wakubwa kazini. They always wondered how and why.
Yule mama wa familia akaenda kumueleza a friend of hers - rafiki akamwambia you never know labda munalimishwa usiku. Anyway twende nikupeleke kwa mganga akucheki. Wakaenda. Kufika mganga akamwambia "dada wenu wa kazi amekua akiwaamsha usiku na kuwafanyisha kazi zoooote. Mnachota maji, mnafua, mnafagia nyumba nzima nk. Yule mama ndo akafunguka macho hapoooo.Na kuanza kukumbuka kuwa wamekua wakishangaa how they wake up saa 11 alfajiri na kumkuta dada keshamaliza kazi zooote. Daaah.. Hii siyo ya kucheka kabisa.
Sasa huyu mama kwa kua alikua keshafunguliwa macho, usiku wa manane wakaamshwa na yule dada yao. Yule hapo ana ufahamu mzuri tu na anaona na anajua kinachotokea. But akajifanya mjinga. Dada akakaa kwenye kochi na kunyoosha miguu huku akiwa command. Wewe kachote maji, wewe kafue, wewe kaoshe bafu, wewe kapige deki. Yule mama akashindwa kuvumulia na kuanza kupiga kelele. Familia nzima ikazuinduka na majirani kufurika. Ndipo akawasimulia wakampa dada mkong'oto na kumpeleka polisi. I dont know hatma yake iliishia wapi.
Jiangalie na wewe. Usije kuta na wewe unafanyishwa kazi usiku kucha na your dada. Tafakari chukua hatua and pray a lot.

                             
                                              
PS. From now kila jumatano tutakua na "Wimbo Wa Wednesday" Ntakua nakuchagulia wimbo mmoja (haujalishi kama ni mpya au wa zamani na from anywhere in the world) upate kuuskiliza kwa siku hiyo...

Kwa maoni na maswali au kama unataka kutokeza kwenye Tatua Thursday feel free to:
send an email - barbshassan@gmail.com
au sms - +255 759 008500

have a lovely day..
xoxo

1 comment:

  1. Wamama tukeshe na kuombea familia zetu. Na hao madada zetu wa nyumbani tuwaweke kwenye maombi pia tusijiombee wenyewe na watoto wetu. Kama ni muislam na aende msikitini, mkristo halikadhalika aende kanisani, tumjue Mungu kwake yote yanawezekana.


    Mama Alice wa ukweli!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text