Social Icons

Pages

Thursday, February 16, 2012

Tatua Thursday....

                                    
Mambo vipi Barbara?
Naitwa Alice. I'm in a fix!!! Nilikua ndani ya relationship na kijana niliyempenda sana sana.. Tulianza toka tukiwa form 3 and tulikuwa wote for approximately miaka 8. Ila miaka miwili ya mwisho alikua Ulaya ambapo alienda kumaliza masomo yake. Nilivumilia kuwepo kwenye long distance relationship. Kumbe huku mi nikawa najibana and kujitahidi kuwa faithful mwenzangu huko alikua anajiachia na wanawake tofauti tofauti ambapo baadaye nilikuja kuona picha kibao katika facebook yake. Nikaona why niendelee kupoteza muda nikimsubiria mtu ambaye ni dhahiri kuwa amesha move on. Manake mawasiliano yalikua hamna tena - wakati alikua akinipigia baada ya kila siku mbili. Anyway, nilimpigia kumwambia kuwa tu end mahusiano yetu ila akawa hapokei simu wala kujibu e mail wala sms. Ilinibidi kufanya maamuzi mwenyewe. Nikaamua  mi na yeye basi! Nikaingia kwenye mahusiano na mtu mwingine anayenipenda kwa dhati na ananijali kupindukia. Ninawa na furaha tele moyoni. Baada ya mwaka akanichumbia na kuleta mahari kwa wazazi wangu. Sasa hivi tumeoana na tunaishi kwa furaha sana na tayari tuna mtoto mmoja mchanga.
Kivumbi kilitifuka siku yule boyfriend wa zamani aliporudi nchini. Alinitafuta ofisini kwangu na hadi nyumbani kwa fujo za kila namna, akisema nimlipe kwa kumpotezea muda na kumuumiza kisaikolojia. Analeta mambo ya huko Ulaya. Sasa kati yangu mimi na yeye nani anatakiwa kumdai mwenziwe. Anyway amekua akinipigia simu hadi saa 6 za usiku, sms zisizoisha, leo ananidai kesho ananiambia baby come back!
Tunakoelekea huyu bwana atanisababishia niachwe na mume wangu. Ni kama anafanya kusudi kuniharibia ili nirudi kwake. Na mie sitaki na nimeshamwambia mara kibao. Uzuri ni kuwa nilishwambia mume wangu story zake kabla hata yeye kurudi. Now nachanganyikiwa. yeye alikua na chance na mimi na akaipoteza mwenyewe, now kwa nini anifuate fuate na kuniharibia? Anajua jinsi gani nilivyoumia na kulia kila siku? Atanilipa machozi niliyoyamwaga muda wote huu nilipokua nalia juu yake? Nimechoka! Kwa nini inakua ngumu mwanamume kukubali kuachwa? Naomba ushauri.. Nifanyeje?

Ps... Karibu umsaidie Alice kwa kutoa maoni yako. Na kama una tatizo ambalo ungependa litokee kwenye Tatua Thursday feel free kunitumia email - barbshassan@gmail.com au sms +255 759 008500

xoxo

4 comments:

 1. Kwanza nakupa pole dada kwa masahibu yaliyokukuta,ni moja kati ya changamoto za kimapenzi ambazo wengi tunakumbana nazo.Mimi nakushauri,kwa kua mumeo anajua kila kitu kuhusu huyo ex then make an appointment with your ex then uende ww na mumeo mumwambie kua wats done is done,tena mumeo amchimbe biti la uhakika aache usumbufu usio na maana.

  Kila la kheri

  ReplyDelete
 2. Nami naungana na huyo wa mwanzo kukupa pole Alice. Things like that do happen at times.
  Nimeona uafadhali kwa upande wako kwa sababu mumeo ana taarifa ya huyo mwanaume. Nachokushauri,kama ulivyosema, umeshamove on...Move on. Acha kujibu msg zake, Acha kupokea simu au kumtumia msg wala nini and if possible, you can change your number for the sake of your own happiness and in saving your marriage. Kama ulivyosema kuwa yeye hajali na anataka kuwagombanisha na mumeo, just block him in your entire system. Hata kama huwezi change namba, then Block namba yake.

  He ruined you once. Dont give him the pleasure of ruining you again! Furaha yake ni kuona kuwa anaweza bado kukusumbua and when you appear tortured anapata furaha..those can be associated na psychological problems. Achana naye and concentrate on your husband and child.
  Dont allow him to make you sad again. You deserved better and you have got what you deserve. A Good and Caring Man.

  ReplyDelete
 3. Hello Alice,
  Pole sana. He just want to ruin your marriage and nothing else, amejimwaga na several different women and finally no one could suit your personality to fill your gap that is why anataka mkose wote.

  Kuwa kama Mao Dou Dou wa filamu ya kichina, make an appointment with him and then go with your hubby to tell him that BLACK will always be BLACK and not otherwise.

  ReplyDelete
 4. Naungana na hao hapo juu,ukiona anaendelea kukusumbua mshitaki na polisi kabisa au hata ikiwezekana akikusogelea mpigie kelele za mwizi.

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text