Social Icons

Pages

Friday, December 23, 2011

Season Greetings...

Hellow wapendwa,
Nina uhakika utakua unajua fika kuhusu kinachoendelea Dsm... Hali ni tete but Mungu anasaidia. Sina mengi ya kusema ila - Tushukuru kwa Yote na tusikate tamaa plus tuendelee kuombeana...
Wakati wa msimu wa Krismasi ni wakati wa kutoa zaidi ya kupokea - kutokana na hali inayoendelea dar - wanawake na watoto wengi wakikosa malazi, chakula na hata nguo - ni muhimu kujitolea. Wakati wa kipindi hiki cha krismasi gawa ulicho nacho na wahitaji....
Tuendelee kuwaombea waliofikwa na janga hili la Mafuriko na kuwasaidia kadri tuwezavyo. Kumbuka leo kwako - kesho kwangu na Kutoa ni moyo....
Mimi nitatoa - wewe je?

Ps - Roho za marehemu wote waliopoteza maisha wakati huu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa Amani. Amina.

Nawatakia heri na nafaka katika msimu huu wa Chrismas and a Happy New Year 2012.



1 comment:

  1. Japo ishapita.........Asante saaana. Nadhani na wewe ulisherehekea vizuri tu!

    Elmmy

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text