Social Icons

Pages

Tuesday, May 8, 2012

Saidia Kutatua Tungo Hii......


                                                             
BABRA MIMI NI MWANAMKE WA KITANZANIA IMEOLEWA NA NINA MTOTO MMOJA  WA KIUME NA MUME WANGU JAPOKUA AMENIKUTA NA MTOTO MMOJA WA KIKE. TULIKUBALIANA NA HANA TATIZO LA KUMLEA BINTI YANGU.
MAHUSIANO YETU YALIANZA KAMA UTANI, MUME WANGU NILISOMA NAYE SHULE YA MSINGI! LAKINI TUKAJA KUPOTEZANA KWA MIAKA MINGI, LAKINI NIKIWA WAKATI WA MCHANA NA RAFIKI YANGU  KWA AJILI YA CHAKULA CHA MCHANA AKAPITA. NIKAMWAMBIA RAFIKI YANGU! "MH HUYU KIJANA NAHISI NAMFAHAMU"  AKATUPITA BILA KUJUA. ALIPOFIKA MBELE KIDOGO, NIKAMWITA NA KUMKUMBUSHA, AKAFURAHI KWELI. NILIPOTAKA KUJUA ANAKOELEKEA, AKANITAJIA JINA LA OFISI YETU, NIKAMUULIZA KULIKONI? AKAJIBU AMEAJIRIWA HUKO.
BASI MAISHA YAKAENDELEA KAMA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI MOJA, WAKATI HUO NILISHAACHANA NA BABA WA MTOTO WANGU WA KWANZA.BASI BINADAMU AMEUMBWA NA HISIA! TUKAANZISHA MAHUSIANO YA KIMAPENZI. LAKINI KATIKA KAMPUNI HIYO HIYO KUNA MWANAMKE ALIKUA ANATAFUTA MTOTO, BILA KUTEGEMEA KWA SIRI WAKAANZISHA UHUSIANO! LAKINI MTU HAKUNYIMI NENO, NIKATONYWA, WALAKINI SIKUTILIA MAANANI NA WAKATI HUO MIPANGO YA NDOA ILIKUA INAENDELEA, SO NILIJUA NI NJAMA NA HILA ZA WALIOKUWA HAWANITAKII MEMA, KUMBE KWELI.
BASI, WAKATI NDOA INANUKIA NAMI NLIKUA NI MJAMZITO, NIKASIKIA YULE DADA NAYE MJA MZITO, SI NIKAULIZA KWA MUME? AKAKATAA KATA KATA, NIKAMWAMBIA NI BORA UWEKE MAMBO SAWA SASA HIVI, AKAENDELEA KUSHIKILIA MSIMAMO WAKE. NIKAACHANA NALO. KUMBE WENZANGU WANAENDELEA KWA SIRI NA MTOTO AKAZALIWA WA KIUME KAMA WANGU NA ANAFANANA NA BABA YAKE NA NIKASIKIA TENA HUWA ANA KWENDA KULE NA HULALA PIA!
DUH! BASI SIKUAMINI! MARA ZIKAANZA SAFARI ZA KWENDA MARA HUKU AU KULE! AMA ANASINDIKIZA MSIBA, MARA OH NILIKAMATWA NA POLISI ANARUDI ALFAJIRI, MARA ANIRUDIE NA T-SHIRT TOFAUTI UKIULIZA OHH NLOVAA ILIMWAGIKIWA NA KITU NIKANUNUA NYINGINE YA MTUMBA. SAWA SASA HIYO CHAFU IKO WAPI TUFUE, OH NILIITUPA! UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBU, SIKU INGINE ALIPOKWENDA KULE AKAACHA ALICHOVAA AKARUDI NA ILE TSHIRT ALO DAI KAITUPA! NIKAMUULIZA! NIKAZUNGUUSHWA! NIKASHIT
MBAYA ZAIDI MAMA MKWE ANA MSHADIDIA YULE WA NYUMBA NDOGO! NIKAWA NAZIDIWA NA TAARIFA ZA MUME WANGU KUA ANAZIDI KWENDA KWA HUYO DADA MPAKA WALIOKUA WANAMUONA WANANIONEA HURUMA! NIKAITWA TENA NA TENA NIKAAMUA KWENDA. NIKIWA NJE NASUBIRI ATOKE NIMDHIHIRISHIE KUWA ULICHOKUA UNAKATAA MI NAJUA UKWELI WOTE, KULE NDANI NIKAWA  NAPEWA TAARIFA ZOTE ZA KINACHOENDELEA, SASA WAPO SITTING ROOM,SASA WAMEINGIA CHUMBANI, SASA WAKO BAFUNI, SASA WAMETOKA SEBULENI,MARA NIKAELEZWA NDO WANATOKA HIVYO NIWE TAYARI. BASI NIKASOGEA KARIBU NA MLANGO NIKASIKIA WANAVYO AGANA,KWA MABUSU TELE TELE, MTOTO NAYE AKAWA ANAELEKEZWA KUMBUSU BABA YAKE ANAONDOKA! YOTE NAONA NA KUSIKIA JAPOKUA WAO WALIKUA HAWANIONI.
NIKAONA INATOSHA NATAKA WOTE WAJUE NINAJUA KILA KITU, WALISHTUKA NUSU WAANGUKE! MTOTO AKAKIMBIZWA NDANI, MUME ALIKUA HAAMINI MACHO YAKE, NIKAMWAMBIA MUME  WANGU HAPA NDIPO ULIPO AGA KUA UNAKWENDA? MAJIBU YALIKUA MAGUMU.
NIKAAMUA KUWAACHA NIKAONDOKA ZANGU, KIUKWELI HAIKUA RAHISI NILIKUA NALIA KILA SIKU NA  KULA CHAKULA HAKIPITI. PRESSURE NA KILA KITU KIBAYA KILINIELEKEA MIMI. ILA NILIYASHINDA YOTE. KWA SASA NA JIONEA KAWAIDA TU AENDE AMA ASIENDE POA TU, NA TAARIFA ZAKE NAPATA ZOTE NAPATA.
LUCY
PS - Rukhsa kumshauri Lucy. Ingekuwa wewe Ungefanyaje????

Ukiwa na story yako nitumie - email - barbshassan@gmail.com
au SMS - +255 759 008500

11 comments:

 1. pole sana mpz wangu, wanaume wabaya sn wanaumiza sana na wamekuwa wasaliti kupitiliza. nawanachofanya siku hizi ni kutafuta mwanamke wakuoa na kutunza familia, kisha anatoka kutafuta wakustarehe nae. we mpotezee tu lea mwanao na kama huduma anatoa vizuri basi inatosha, kuwa bizy na nyumba yako na wala usijiumize kwa mawazo mwishowe ufe mwanao abaki mkiwa na uwape nafasi yakufunga ndoa. kama mume ni wako na huyo mshenzi anachezewa tu na ataroga usiku na mchana ila hawezi tena kuvaa shela.
  ndoa ni uvumilivu na ustahimilivu, simama km mama wakiafrika hayo ni mapito tu atatulia tu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. kweli dada, nimeipenda sentensi yako ya mwisho kwani mama zetu wamevumilia mengi! true african women!!!
   mama s.

   Delete
 2. aisee dada nikupe ushauri, tayari upo kwenye ndoa na ilikua ndoa halali yenye mashahidi, hapakua na siri na labd hata huyo kimada alishuhudia so anatamani ingekua kinyume chake!
  wewe tulia muombe Mola akuepushe na mabaya hasa maradhi, mume huyo ni wako na atarudi tu, so far hakutegemea kama umejua sasa wataendelea lkn atakua makini kidogo.
  pili usimuweke mama mkwe wako mbali, unajua huyo kimada atakua anajigonga kwa mama mkwe anapeleka vzawadi nk. ili apendwe yeye lkn mama mkwe hawezi vunja ndoa yako, muheshimu usimuoneshe ubaya wowote na muoneshe mumeo kuwa unamjali mama yake hata kwa ku-"pretend" tu. mama mkwe ndio anakupotezea mume hapo,cz hawa nao mh! na ina maana mumeo ameegemea sana kwa mama na ndio anamshauri na sasa anaambiwa yule ndo anafaa just because of vijizawadi. soo kaa karibu na mama mkwe, na mumeo atarudi, it works, dont dispair, alichokiunganisha Mungu mwanadamu hawezi tendanisha!
  pole sana tena rafiki, hiyo ndio mitihani, inakukomaza zaidi!

  ReplyDelete
 3. Ni rahisi kumshauri mtu lakini nikivaa uhusika
  Mi naona siwezi jamani,siwezi kabisa eti nijue anaenda huko???
  Nikimfumania kama hataonesha kujutia kosa lake nadhani Dunia itaninyooshea kidole kwa kukosa uvumilivu ila nafsi yangu itakua na amani.........
  Yaani sijui nisemeje jamani

  ReplyDelete
 4. kwa kweli ni ngumu sana lakini uvumilivu nao unahitajika kwani hawa watu ndivyo walivyo kikubwa ni kumtegemea sana Mungu atakupa nguvu za kakabiliana na hiyo hali na kila jambo lina mwisho yataisha tu utashangaa mumeo anarudi kwako na mnaishi kwa amani, furaha na upendo.

  ReplyDelete
 5. mh! kweli wanaume wanaumiza.

  ReplyDelete
 6. mm sijui nisemaje, ila natumaini kila mtu anahitaji furaha, amani na upendo. ukiona hivyo hazipo tafuta njia ya kuvipata.maradhi ni mengi angalia asijekukuletea ukaanza kuteseka.wanawake tumepewa hekima na busara sana.jitahidi usonge mbele!!!!

  ReplyDelete
 7. Adui wa mwanamke ni mwanamke akisaidiwa na mwanaume. Mimi nilishakama mwizi wangu lakini ndoa inaendelea kwa kuwa jamaa katubu na amempiga chini huyo muhuni mwenzie. Nina makachero hivyo nina hakika na ninachkisema. Angekuwa anaendelea kwa kweli pride yangu isingeniruhusu kuishi uke wenza. Maana mume akiwa na kimada na wewe unamjua fika ni nini kama si uke wenza??? Lazima achague mimi au yeye.

  ReplyDelete
 8. pole sana dada wanaume wengi ndo walivyo,wanatamani kotekeote,hatqa kwa nduguzo waweza fanya hivyo pia.kama unampenda endelea kuvumilia,mwombe Mungu ambadilishe.la kama hamjafunga ndoa ya kanisani basi tafuta usitaraabu mwingine.kama bado anamapenzi na wewe endelea kumwombea tu,aweza kubadilika.ila wewe usiwe mkali kwake wala usimuulize just take it easy,upendo kama kawaida ili umsute.ukiwa mkali atapata sababu.wanawake wenzangu tuwe wavumilivu na tuongeze upendo wakati wa matatizo ili waume zetu waone aibu ya kutoka nje ya ndoa.Unabahati Mungu kakupatia mtoto kama yeye alivyopata,sasa zidisha tu upendo utaona yeye mwenyewe anachenji.pole sana jipe moyo Mungu atakusaidia.

  ReplyDelete
 9. fifty-fifty one Tantric massage cаn chаnge uѕ
  and our relаtіonѕhips and help und F�rѕoгglichkеіt
  unԁ hat einе Sеvеre ωеіblich
  sіnnlіch, аbеr auch m�tterliche Komponentе.  Feel free to surf to my web blog - Erotic Massage In London

  ReplyDelete
 10. I really like it when people come together and share views.
  Great blog, continue the good work!

  Also visit my blog post - グッチ 時計

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text