Social Icons

Pages

Wednesday, May 2, 2012

Ulikutana na Mume au Boyfriend wako wapi?

Mambo,
Pole sana kwa kuwa kimya for a while.. It's a long story.... Ila naomba radhi kwa hilo... I was thinking, unajua jinsi mashangazi na wazazi wetu wanavyotulazimisha kwenda maharusini? Especially kwa sie ambao hatujaolewa. Wakiamini kuwa huko ndio tutakutana na "potential husbands" Sijui kama kuna ukweli wowote ndani ya hili. Anyway nikaona si vibaya tupeane advice kuhusu wapi tunaweza kukutana na hao "potential husbands". Na tunaweza kufanya hivyo kwa wewe ku share ni wapi ulikutana na aliye mume wako au boyfriend wako kwa sasa... I believe itasaidia sana.. Hehehehhehe
Je mulikutana club au bar? Ila hua wanasema eti ma boyfriend utakaoanzana nao club hawadumu


Au harusini?

Courtesy of www.8020fashions.blogspot.com

au kwenye funeral?

         
Airport?Ndani ya bus au train?

                             
Au ofisini?

                                           

Fungukaaaaa.. Hehehehehe..

For a private neno niandikie - barbshassan@gmail.com
or SMS - +255 759 008500

much love
xoxo

17 comments:

 1. hi! na kweli bora utuwie radhi cz tumemis story za huku sana. yaani we ni mkali kwa kuibua mijadala tata lkn mizuri na inatupa challenge sana. mimi na mume wangu tulikutana college ambako tumesoma pamoja, alikua one yr ahead tukawa kwa r/ship kwa kama 5 yrs na mwishowe last yr tukafunga ndoa......
  sidhani sana kama unaweza kukutana na jamaa club ama harusini mkawa na serious r/ship kwani ni ngumu kujua tabia ya mtu ghafla, na wengi huishia kusema "aah, si mipombe tu ilinifanya nikutokee...." ni mtazamo tu
  and so on! labda tupate na maoni ya wengi hapa ndo tujenge hoja///

  ReplyDelete
 2. mimi nilikutana na hubby getini kwetu hahahhahaha aliniona tu akanipenda akanifukuzia hadi akanipata hahahahhaha was fun kwa kweli

  ReplyDelete
 3. thanx kwakutukumbusha mwanzo wetu ulikuwa vp, mimi nilikutana na mume wangu(baba twins) kituoni naelekea msibani nikiwa na kanga zangu mbili nasubiri daladala, nilikuwa na rafiki yangu mwingine ambaye ndio walikuwa wanafahamiana na honey wangu, wakasalimiana na mm nikamsalimu tukawa tunakoenda na yeye ndio anaelekea badala yakupanda gari ikabidi tutembee kwani hakukuwa mbali tukawa tunapiga story za hapa na pale, from there akanipenda tukawa marafiki kwa 4 yrs na hatimaye ndoa na inamiaka 3 tumebahadika kupata twins girl & boy . we still in deep love!

  ReplyDelete
 4. kha jamani acheni tu mie hubby wangu nilikutana nae bank nipo kwenye foleni yeye yupo officn akaniona basi hapo hapo alijitaidi akapata no yangu baada ya kunihudumia nimeshaondoka huku nyuma akafungu account yangu akakuta ile fomu tunayo jazaga mpaka no ya simu basi hapo akapata no yangu kirahiisiiii....

  ReplyDelete
 5. kwikiwkwiwkwiwiw huwezi amini niliunganishiwa na best wangu wa a level yy alikuwa na bf wake na bf ana best wake basi jamaa akamwambia nampenda bst wa gf wako mdada akanambia nikadengua mwisho wa cku nikaingia line he is my hubby for 21 years got three boys!!!!

  ReplyDelete
 6. Nilikutana naye chuo yeye alikuwa mwaka wa tatu (mwaka wa mwisho) na mie nilikuwa mwaka wa kwanza yaani ile nimefika chuo tu ndo kuonana naye and from there tukawa marafiki alimaliza chuo akaondoka na kuniacha chuo ila tukawa tumepeana ahadi zetu....I never dated any guy nikiamini yule ndo atanioa na kweli from Oct, 2004 tukaja kuoana Oct 2011.....miaka mingapi hiyo, Mungu ni mwaminifu ukimshirikisha kwenye maswala mazima ya mahusiano.

  ReplyDelete
 7. jamani hamna wa kanisani, msikitini etc..........

  ReplyDelete
 8. Du si tulikatana o-level yeye yuko form three mi form two mwaka 1996 tukaendelea kuwa wapenzi mpaka tukaoana mwaka 2005. Tumebarkiwa watoto wawili sasa. Kweli mungu ni mkubwa ukimshirikisha anafanya.

  ReplyDelete
 9. TULIKUTANA KAZINI, NILIMPENDA TOKA SIKU YA KWANZA ALIVYOHAMISHIWA OFISINI KWETU. ILA NIKAJIKAUSHA MTOTO WA KIKE NDOA INAMIAKA 6 NAMSHUKURU MUNGU.

  ReplyDelete
 10. sisi tulikutana kwenye harusi, nilikua msimamizi na nilikua nacheza mziki akamind mamove akaanza kunifatilia heheh. ndoa ina 6 yrs next month na we have 2 kids

  ReplyDelete
 11. hahahahaha, ngoja nimuongelee mdogo wangu. alikutana na mume wake kwenye sendoff ya rafiki yake. alikuwa anamsindikiza bb harusi kwenye sendoff yule aliyekuwa mpambe wa bwana harusi si akampenda, wakawa marafiki na mwaka jana walifunga ndoa mwezi wa tano na leo wana mtoto wa kiume. mm sitaki kujiongelea coz mpaka leo najiuliza ilikuwaje?

  ReplyDelete
 12. mi nilikutana na mume wangu alikuwa mpiga picha kwenye ubatizo wa mfanyakazi mwenzie cha ajabu sikualikwa nilienda kwa aunt yangu ambaye alikuwa ndugu na mama wa mtoto anayebatizwa nikafika home wote wakawa wameenda nikakutana na dada ss niliingia chumbani kupumzika wkt narudi geto kwangu nikasahau funguo nikawa sina jinsi nikampigia aunt yangu akaniambi kuwa yeye harudi mida hiyo hivyo niende kwenye sherehe wakimaliza nitaenda nao hom ndipo wanipe fungo kufika kule kumbe mr alikuwa shuta akaniona akanipenda nakutangaza ndoa now 11 years 3 children boy 2, i daughter ilove youu so much

  ReplyDelete
 13. hii tamu haswa me nilikutana nae soon baada ya kumaliza six,nilikuwa nauza duka la kuku akaja kununua pale so akawa mteja wangu mzigo ukiingia tu nishampigia cm anakuja kuchukua mwisho wa siku tukaanza kudate n this year mwezi wa kumi ndo ndoa!amaizn!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 14. mimi nilikutana na mume wangu njiani nikiwa natoka sokoni, hapo hapo jamaa akapenda vibaya mno, mpaka sasa ndoa ina miaka saba na tuna watoto wawili wakiume na wakike.

  ReplyDelete
 15. Jamani mungu akipanga kapanga!mm nilikutana na mume wangu officen kwake nilienda mtembealea rafiki yangu nikiwa mapokezi namsubiri shoga yangu aje si ndo hubby akapita akanisalimia!nikajikuta roho inaongea yenyewe daah huyu kaka angekuwa mume wangu daa!basi kidogo shoga yangu akaja nikamwambia kuna mkaka kapita apaa daah!shoga akaniambia kavaaje uyo kaka aliokuchanganya nimjue na mm nikamwambia alivyovyaa basi tukacheka tukaendelea na yetu.nilipoondoka tu ata dk 5 hazijapita shoga yangu ananipigia simu ananiambia yule kaka ashamjua coz jamaa amemfuata amemuulizia abt mm na akaomba namba yangu ya simu akaniuliza kama ampatie nikamkatalia asimpe!basi baada kama ya miaka miwili yule kaka akawa anawasiliana na rafiki yangu anamuulizia habadi zangu mpaka rafiki yangu akasema ampe no awe ananisalimia mwenyewe basi shuguli ndo ilipoanzia hapo na mpaka leo ni mume wangu na tunamiaka mi 5 ya ndoa na watoto wawili.

  ReplyDelete
 16. mimi wa kwangu nilikutana nae kupitia best friend wangu nikiwa high school 2007 until now we are married and have a lovely son....3yrs of marriage and am hapi...God is able
  regards
  Winne

  ReplyDelete
 17. It сertainly isn't merely the most have causes other than spinal anaesthesia heart beginning encroachment. With training, possibilities of causing el efecto es el dolour f�sico, mental, emocional o espiritual. The intelligence Tantric Massage in a higher place his bosom peculiarly in the evenings Piece he was restful.

  Check out my homepage :: tantric massage London

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text