BABRA MIMI NI MWANAMKE WA KITANZANIA IMEOLEWA NA NINA MTOTO MMOJA WA KIUME NA MUME WANGU JAPOKUA AMENIKUTA NA MTOTO MMOJA WA KIKE. TULIKUBALIANA NA HANA TATIZO LA KUMLEA BINTI YANGU.
MAHUSIANO YETU YALIANZA KAMA UTANI, MUME WANGU NILISOMA NAYE SHULE YA MSINGI! LAKINI TUKAJA KUPOTEZANA KWA MIAKA MINGI, LAKINI NIKIWA WAKATI WA MCHANA NA RAFIKI YANGU KWA AJILI YA CHAKULA CHA MCHANA AKAPITA. NIKAMWAMBIA RAFIKI YANGU! "MH HUYU KIJANA NAHISI NAMFAHAMU" AKATUPITA BILA KUJUA. ALIPOFIKA MBELE KIDOGO, NIKAMWITA NA KUMKUMBUSHA, AKAFURAHI KWELI. NILIPOTAKA KUJUA ANAKOELEKEA, AKANITAJIA JINA LA OFISI YETU, NIKAMUULIZA KULIKONI? AKAJIBU AMEAJIRIWA HUKO.
BASI MAISHA YAKAENDELEA KAMA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI MOJA, WAKATI HUO NILISHAACHANA NA BABA WA MTOTO WANGU WA KWANZA.BASI BINADAMU AMEUMBWA NA HISIA! TUKAANZISHA MAHUSIANO YA KIMAPENZI. LAKINI KATIKA KAMPUNI HIYO HIYO KUNA MWANAMKE ALIKUA ANATAFUTA MTOTO, BILA KUTEGEMEA KWA SIRI WAKAANZISHA UHUSIANO! LAKINI MTU HAKUNYIMI NENO, NIKATONYWA, WALAKINI SIKUTILIA MAANANI NA WAKATI HUO MIPANGO YA NDOA ILIKUA INAENDELEA, SO NILIJUA NI NJAMA NA HILA ZA WALIOKUWA HAWANITAKII MEMA, KUMBE KWELI.
BASI, WAKATI NDOA INANUKIA NAMI NLIKUA NI MJAMZITO, NIKASIKIA YULE DADA NAYE MJA MZITO, SI NIKAULIZA KWA MUME? AKAKATAA KATA KATA, NIKAMWAMBIA NI BORA UWEKE MAMBO SAWA SASA HIVI, AKAENDELEA KUSHIKILIA MSIMAMO WAKE. NIKAACHANA NALO. KUMBE WENZANGU WANAENDELEA KWA SIRI NA MTOTO AKAZALIWA WA KIUME KAMA WANGU NA ANAFANANA NA BABA YAKE NA NIKASIKIA TENA HUWA ANA KWENDA KULE NA HULALA PIA!
DUH! BASI SIKUAMINI! MARA ZIKAANZA SAFARI ZA KWENDA MARA HUKU AU KULE! AMA ANASINDIKIZA MSIBA, MARA OH NILIKAMATWA NA POLISI ANARUDI ALFAJIRI, MARA ANIRUDIE NA T-SHIRT TOFAUTI UKIULIZA OHH NLOVAA ILIMWAGIKIWA NA KITU NIKANUNUA NYINGINE YA MTUMBA. SAWA SASA HIYO CHAFU IKO WAPI TUFUE, OH NILIITUPA! UKIWA MUONGO UWE NA KUMBUKUMBU, SIKU INGINE ALIPOKWENDA KULE AKAACHA ALICHOVAA AKARUDI NA ILE TSHIRT ALO DAI KAITUPA! NIKAMUULIZA! NIKAZUNGUUSHWA! NIKASHIT
MBAYA ZAIDI MAMA MKWE ANA MSHADIDIA YULE WA NYUMBA NDOGO! NIKAWA NAZIDIWA NA TAARIFA ZA MUME WANGU KUA ANAZIDI KWENDA KWA HUYO DADA MPAKA WALIOKUA WANAMUONA WANANIONEA HURUMA! NIKAITWA TENA NA TENA NIKAAMUA KWENDA. NIKIWA NJE NASUBIRI ATOKE NIMDHIHIRISHIE KUWA ULICHOKUA UNAKATAA MI NAJUA UKWELI WOTE, KULE NDANI NIKAWA NAPEWA TAARIFA ZOTE ZA KINACHOENDELEA, SASA WAPO SITTING ROOM,SASA WAMEINGIA CHUMBANI, SASA WAKO BAFUNI, SASA WAMETOKA SEBULENI,MARA NIKAELEZWA NDO WANATOKA HIVYO NIWE TAYARI. BASI NIKASOGEA KARIBU NA MLANGO NIKASIKIA WANAVYO AGANA,KWA MABUSU TELE TELE, MTOTO NAYE AKAWA ANAELEKEZWA KUMBUSU BABA YAKE ANAONDOKA! YOTE NAONA NA KUSIKIA JAPOKUA WAO WALIKUA HAWANIONI.
NIKAONA INATOSHA NATAKA WOTE WAJUE NINAJUA KILA KITU, WALISHTUKA NUSU WAANGUKE! MTOTO AKAKIMBIZWA NDANI, MUME ALIKUA HAAMINI MACHO YAKE, NIKAMWAMBIA MUME WANGU HAPA NDIPO ULIPO AGA KUA UNAKWENDA? MAJIBU YALIKUA MAGUMU.
NIKAAMUA KUWAACHA NIKAONDOKA ZANGU, KIUKWELI HAIKUA RAHISI NILIKUA NALIA KILA SIKU NA KULA CHAKULA HAKIPITI. PRESSURE NA KILA KITU KIBAYA KILINIELEKEA MIMI. ILA NILIYASHINDA YOTE. KWA SASA NA JIONEA KAWAIDA TU AENDE AMA ASIENDE POA TU, NA TAARIFA ZAKE NAPATA ZOTE NAPATA.
LUCY
PS - Rukhsa kumshauri Lucy. Ingekuwa wewe Ungefanyaje????
Ukiwa na story yako nitumie - email -
barbshassan@gmail.com
au SMS - +255 759 008500