Social Icons

Pages

Thursday, March 1, 2012

Tatua Thursday....

                                  
                                             


Mambo Babra,
Naitwa Neema ni mkazi wa Arusha. Naomba tusaidiane kujadiliana kuhusu swala la wanaume zetu kuangalia wanawake wengine wakati tukiwa nao. Boy friend wangu ndo zake. Yaani utakuta nimekaa naye sehemu labda tunakula au tunakunywa. Asipite demu - awe mweupe au mweusi, mnene au mwembamba, shape ya 8 au ya 7, lazima ageuke. Amtizameeee kisha ndo anigeukie mimi. Inaniuma sana kwa sababu nahisi kama anajuta kuwa na mimi na ni kama namkatizia kufanya mambo yake. Akiwa anaendesha gari pia mambo ni yaleyale. Kuna siku almanusura agonge gari iliyokua mbele yake. Kisa? Kuna demu alikatiza kafungushia mzigo wa haja!!!
Kiukweli najiamini hata mimi ni mrembo. Ni mrefu, mwembamba juu na hips kubwa. Nyororoo mwili mzima na miguu ya bia. Ila sasa huyu boy friend anasabaisha confidence yangu ipungue. Na nikimuuliza anasema ananipenda na yeye ni wangu tu. Sasa kama ni hivyo why aangalie wanawake wengine hata mimi nikiwepo. Si afanye siri basi. Aangalie akiwa na washkaji zake au aangalie kimpango nisishtukie. Na akipita mrembo kweli kweli my boy friend kabisa anatamka - Duuuu yule demu ni mremboooooo.. daaaaaaaa....
Nimechoka kweli... Please nisaidieni...
Neema...


Toa maoni yako...
Kwa maswali au kama ungependa kutoa maoni yako au kuchagua wimbo wa Wimbo Wednesday au story yoyote niandikie
Email - barbshassan@gmail.com
SMS - +255 759 008500

Maoni yangu? Ningekua Neema ningefanya hivi....Hahahhahahahahahhahhahahhahha.....
                                    
Have a good day
xoxo

6 comments:

 1. Stay with your confidence even if inauma na inakera sana. Wanaume wengi wapo hivyo akikupenda sio kwamba amekuwa kipofu hataona tena. Jiamini hivi atapenda wangapi duniani humu? Naamini ameona wengi ila wewe ndio chaguo lake.

  Jipende, Jiamini, macho hayana pazia!!!!!!!!!!!!

  Mama Alice wa Ukweli!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 2. Ukweli unauma ila dear hiyo ni dalili ambayo siyo nzuri saana. Maana kama ni Boy friend tu anadiriki kufanya hivyo akiwa mume atafanya makubwa.......! kama ushamwambia kutopendezwa na hiyo tabia na bado hajajirekebisha hiyo inamaanisha kuwa anadharau/hathamini feelings zako, na hiyo mamii ni HATARI SANA kwa maisha ya kimapenzi.
  Kwa kuwa bado upo nae/unampenda mimi nakushauri kwa sasa ujaribu kufanya hivi kama utaweza; Mkiwa wote kwenye lunch, dinner....akipita Mwanaume mkali na wewe geuka mtizamee halafu unasema "duuh jamaa mkali". Utaona huyo Boy friend wako atakavyochukia. Ila ukifanya hivyo jiandae kwa yote maana wanaume wengine watata.....
  Elmmy

  ReplyDelete
 3. dah ningekuwa mimi akikatiza mwanaume tu namsifia mpaka basi,tena angekoma maana tungetoka ngoma droo,

  ReplyDelete
 4. macho hayana pazia...hahahah napita tu!

  Gluv

  ReplyDelete
 5. Wadau wa hapo juu mmenivunja mbavu lol....yan hata mm ningeanza kuwasifia wanaume mahandsome mpaka ningekuwa natoa na udenda makusudi au navunja glass kabisaaaaa ili akome!mjifunze kuridhika nyie migumeme shxxxxxxy

  ReplyDelete
 6. Riсhard C. Fiallo, tantrіc masѕаgе Schoolmaster, vοlitіon be of psyсhоlogy and
  nеuroscience аt the University of Michigan, agreeѕ.


  My web blog :: tantric massage london

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text