Social Icons

Pages

Thursday, March 15, 2012

Tatua Thursday....

                                 
                                                


Habari yako Barbara,
Nina tatizo ambalo ningependa kuliweka mezani katika Tatua Thursday kwenye blog yako.. Naomba ushauri..
Mimi ni mdada wa miaka 28 na nashukuru nina kazi nzuri tu na nina mtoto mmoja wa kiume nje ya ndoa. Bado sijaolewa na mimi na baba mtoto tulishaachana. Nilibahatika pia kukutana na mkaka mzuri, mtanashati mwenye qualities zote ninazo penda awe nazo mwanamume. Ana miaka 35. Nilitambulishwa kwake na marafiki zangu. Tulitokea kupendana sana na tumedumu kwa mwaka mzima. Ameshanitambulisha kwa marafiki zake wote na akanipa ahadi nyingi tu ikiwemo ya kunitambulisha kwa wazazi wake. Pia amekuwa mkweli sana kwangu na alinitamkia kuwa ana watoto wawili ambapo mmoja anakaa na bibi yake na huyu wa pili anakaa na mamake.
Nimekuwa nikienda kwake mara kwa mara na pia kuna vitu vyangu vipo kwake (nilihamia nusu nusu) , kwa kweli nampenda sana. Tulikuja kugombana mwezi jana, kwa sababu alianza kubadilika, akawa anaweza asipokee simu siku nzima na hata sms hajibu. Nikiwepo kwake anatoka nje kupokea simu,  Nikimwambia nakwenda kwake anasema hayupo na kuwa amesafiri kikazi. Kila siku kusafiri au anasema atarudi nyumbani usiku wa manane kwa sababu ya kazi anazofuatilia. Kwa mazingira ya kazi anayofanya nilimuelewa. Ila nikawa navumilia tu. Sasa juzi hapa tukarudiana ila kwake hataki niende tena. Kila siku anakuja na story mpya, mara kasafiri, mara wadogo zake wako pale nk.
Jana nimepata habari kuwa kuna mwanamke nyumbani kwake - huyu sijui kama ni mpya au ni yule yule mama mtoto. Anapika na kupakua hapo nyumbani. Kinachoniuma zaidi ni kuwa ananificha mimi. Inaniuma kwa nini asiniambie ukweli, wakati tulipoanza alinambia kila kitu.  Najiuliza maswali mengi sana hapa nilipo. Niliamiini kua huyu ndiye atakuja kuwa wangu wa maisha, je, ameniweka wapi katika maisha yake, je, niifanyeje? Sitaki kumuacha na pia sitaki ku share... Nimechanganyikiwa sana... Na nampenda sana na najua hata yeye ananipenda. Nishaurini jamani...

Anna wa Dodoma...

Ukitaka kuelezea story yako email me - barbshassan@gmail.com
au SMS - +255 759 008500

6 comments:

 1. Pole dada n usijidanganye kuwa anakupenda kama u unavyompenda coz mapenz ya kwel cyo ya kufichana,fikiria from no where akukataze kwenda kwake ikiwa mwanzo ulikuwa unaenda n if ts true kuwa hapo kwake kuna wadogo zake zat was the rt tym for u know ur in-law so fatilia if u can kujua kip anakufcha then kama kwel kuna mwanamke mwngne u just go on wit ur lyf i know at frst it hurts but zats how men they r.U have ur gud job n mtoto ambae ni faraja kwako endelea kuwa strong Mungu ni mwema Inshaallah n u atakubaliki kupata yule mkwel n akupendae

  ReplyDelete
 2. huyu hakupendi kabisa angekuwa anakupenda asichukua mwanamke na kumuweka ndani,pole sana dada

  ReplyDelete
 3. hakupendi hata robo alikupenda zamani tu plz usilazimishe penzi nakushauri base ktk kufanya mambo yako maana huyo alikuwa anakutumia tu, usidanganyike na kutambulishwa kwa marafiki watu wanavishwa engagement mbele ya wazazi na wanaachwa, ushauri wa bure tumia mda wako kumlea mwanao sababu ndio faraja yako milele hawezi kukuacha.

  ReplyDelete
 4. soma alama za nyakati sio lazima uambiwe mimi na ww basi.

  ReplyDelete
 5. hakupendi, usiusemee moyo wake. bibi weee anza life yako all alone. maisha bila mwanaume wa kumfulia yanawezekana.

  ReplyDelete
 6. It's unmanageable to imagine what price ruined that I got the message that my ancestors was sending me. therefore disease is seen as a state of disharmony, where tantric massage, whether you believe or not. How practically Didactics Is saan makikita mo ang mga masahista nila. The rest of my wife and emotionally, devising the journey into maternity more joyous and memorable.

  Stop by my page - london tantra

  ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text