Social Icons

Pages

Thursday, March 8, 2012

Tatua Thursday....

                                        


Happy women's day kwenu wooooteee...
Nina a friend of mine, nilikua sijamuona siku nyingi. Nimeonana naye juzi kati alikua na mengi ya kusema. Imeniogopesha sana. Imenifanya ni rethink about getting married na kuogopa mahusiano in general.
Huyu dada got into a relationship na a very potential bachelor, mwenye vigezo vyote ambavyo huyu dada alikua anatafuta in a man. Relationship kwa kawaida mwanzoni ilikua taamu na nzuri hadi watu wa nje wakawa wanaionea wivu. Wakaendelea vizuri tu. Waka move in, na kuishi kwenye nyumba moja.
Baada ya muda jamaa akaanza kumsema sema huyu dada - mara chakula hakijaiva, mara nyumba chafu, mara vyombo vinanuka sabuni na kadhalika. Dada yetu akawa anavumilia na kuendelea kujaribu to please the man. Jamaa akaenda kujitambulisha kwa kina huyu dada na kumvisha pete ya uchumba. Dada akaona - eeh kweli nimepata. Baada ya muda jamaa akawa harudi nyumbani, dada akampigia anamwambia - hujui kupika wala kutandika kitanda so nitakula na kulala huku huku nijuako mie. Mmmhhh.. Visa na mikasa vikaanza upya na kuwa zaidi.
Baada ya musa si mrefu, jamaa akawa anarudi nyumbani yuko chakari anampa kisago cha uhakika huyu dada. Heeeee dada akastuka! Yamekua hayo!!! Yule dada hakukubali, akipigwa na yeye anapiga, ngumi kwa ngumi, teke kwa teke. Kumbe yule jamaa hasira ndo zinaongezeka. Akiona kuwa yule dada anajaribu kuwa the man kwenye relationship. Ila wakaendelea kuishi together.
Siku ya siku dada wa wenyewe kalala mwanamume karudi usiku wa manane na kuanza kumvamia yule dada. Kwa vile huyu dada alikua bado usingizini hakuweza kukurupuka na kujihami. Alipigwa hadi basi. Alipokua yupo tika tika kajikunja hapo chini kwenye floor, jamaa akaenda kufuata kisu jikoni, akamchoma choma mwili mzima. Kisha akaondoka. Yule dada hawezi tena kulia wala kunyanyuka, hawezi kutafuta simu wala kuongea. Jamaa akapigia simu ndugu wa yule dada na kuwaambia "Nendeni mukachukue maiti yenu" Kisha akakata simu.
Ndio ndugu kushtuka wakakimbia hadi kwa yule dada. Wakakmkuta hajiwezi kabisa. Wakambeba na kumkimbiza hospital. Yule dada kwa kweli aliponea kwa kudra za Mungu.
But ni nini hasa kinampelekea mwanamume hadi kutaka kumuua kabisa mwanamke aliyekua anaishi naye, anampenda, analala naye, amemchumbia?

                                    
                                           
Pinga na kataa kabisa Ukatili dhidi ya Wanawake

kwa maoni email - barbshassan@gmail.com
au sms - +255 759 008500

2 comments:

  1. Hap women's day!i don know hawa wanaume huwa wana mapepo r tamaa cjui inakuwaje inafkia kumfanyia k2 kam hcho kwa m2 uliyempenda had kumchumbia.Dada amshukuru Mungu kwa kumuonyesha kuwa ham2p mja wake n wat next anaitaj ku move on and amuonyeshe huyo mwanaume how strong woman she iz.

    ReplyDelete
  2. aah hao ndio wanaume huwa hawana formula unaweza kujiona umepata right man kumbe siyo.ila sisi wanawake tusiwe tunawavumilia wanaume kufikia hatua ukiona mambo siyo mazuri fanya maamuzi mapema.ubaya wa wanawake siyo wepesi kuchukua maamuzi hii inatucost sana.sasa angemuua je au ndio kupenda huko kupenda gani huko?pole yake sana siku hizi hakuna wanaume wanawake tujifunze kusimama kwa miguu yetu mbona tunaweza tu tusijibweteke unampenda mtu uliyekutana nae ukubwani unampenda nn!!!!!

    ReplyDelete

 

Sample text

Sample Text

Sample Text